Mpango wa kucheleweshwa au kutopatikana kabisa kwa katiba mpya waanza kubainika - Mtazamo wangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpango wa kucheleweshwa au kutopatikana kabisa kwa katiba mpya waanza kubainika - Mtazamo wangu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tankthinker, Sep 2, 2011.

 1. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #1
  Sep 2, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF, kwanza kabisa natumaini mmekuwa na mapumziko mema ikiwa ni pamoja na kusheherekea sikuku vizuri. Nimeona nilete hapa jamvini jambo ambalo nimeliona ndani ya maelezo ya hotuba ya Mh. Rais ambalo kwangu hotuba hii imenipa kuuona mpango wa kimakusudi wa ucheleweshaji au kushindikana upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Kabla sijaendelea naomba ni weke nukuu ya hotuba iliyo nipa kuuona mpango huo;

  "napenda kurudia rai au taadhari niliyo itoa wakati wa mkutano wangu na maaskofu, walio wajumbe wa jukwaa la wakristo Tanzania 22/07/11 jijini Dar es salaam, niliomba tujitahidi kuhakikisha kuwa mjadara wa katiba haugeuki kuwa mdahalo au malumbano kati ya wakristo na waislam kuingiza maslahi yao katika katiba tukufikisha hapo kutatokea mivutano ambayo ni migumu kuipatia majibu na kuna hatari ya katiba mpya kushindikana kupatikana au kuchelewa sana na hata amani kuvunjika............." Gazeti Mwananchi la 02/09/11. ukurasa wa 7.

  Sababu ya mimi kuwa na mtazamo huo;
  1. Hakujawahi kuwa na mdahalo au malumbano ya wakristo na waislamu juu ya Katiba wakati wowote hivyo isingehitajika Mh. JK kulizungumzia.

  2.Katika ilani ya CCM 2005, Swala la kadhi lilikuwemo na hivyo JK aliiwahidi waislamu kulishughulikia, sasa iweje ghafla anasema swala hili ni lao wenyewe na yeye na chama chake na serikali yake hawahusiki?

  3.Mh. Rais anajua kabisa kuwaambia Waislamu kuwa swala la Kadhii walishughulikie wenyewe ni ltazua mtafaruku na ndiyo sababu ya mazingira yatakayo halarisha kuchelewesha upatikanaji wa Katiba mpya kabla ya 2015.

  Kwakweri haya ni mazingira ya kutengenezwa ili yatumikie makusudi yaliopangwa. Huo ni mtazamo wangu.
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yawezekana ukawa sahihi lakini ninachokiona kama katiba mpya haitapatikana mapema Tanzania itakuwa kama Libya.
   
 3. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Suala la ilani ya CCM kusema juu ya mahakama ya kadhi halihalalishi serikali kuianzisha, wala wahitaji wake kuilaum serikali kwa kutoianzisha.
  ile ilikua ni ccm na sasa unazungumzia serikali. serikali ni mojatu ya mihimili mitatu inayounda taifa.mingine ni bunge, na mahakama.
  suala la kdhi limepita katika bunge??
  je kimahakama/sheria na hapa nikimaanisha katiba (kama sheria mama) inaruhusu??
  jibu hayo maswali utaona ni kwa nini JK akawaruhusu waisla kanzisha mahakama ya kadhi wao kama wao na sio serikali!
  mahakama ya kadhi hata ikianzishwa haitakua na tofauti yoyote na taasisis nyingine za kiislama unaozijua.
   
 4. S

  Shiefl Senior Member

  #4
  Sep 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK anakosea. Aliweza kutujaza maneno na imani ya kuwa kuna udini na sasa anaanzisha hili la watu kuanza kulumbana kuhusu mambo ya waislam na wakristu kwenye mikakati ya kuanzisha katiba mpya. Alichotakiwa kusema yeye ni kuwa katiba ya nchi yetu inatakiwa kufuata mfumo wa nchi isiyofungamana na dini yeyote...Secular state finished.

  Haya makandokando ya kuvaa mahijabu na roman color bungeni nayo angeyakemea huyu mh. hi inchi haina dini sasa iweje wabunge watuvalie kidini?
   
 5. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #5
  Sep 6, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu hawa viongozi wetu hawalioni hilo, au sijui wameamua tu kulifumbia macho kwa sababu ya tamaa ya madaraka. Hawjui kuwa yakitokea yaliotokea Libya ni nani atakuwa na muda wa kufurahia madaraka yake tena? "Mungu apishie mbali hatari hiyo"
   
 6. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #6
  Sep 6, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu maelezo yako yanaeleweka na yako sawa kabisa. Ila nilicho point katita thread niliyoiandika hapo juu ni kwamba katika hotuba ya Mh. Rais imeonyesha kuwa uko mpango wa kuchelewesha upatikanaji wa Katiba mpya au kutokuwepo kabisa kwa katiba mpya. Sababu ni kwamba, swala la mahakama ya kadhi kuanzia sasa litachukua sura mpya ambayo italeta mtafaruku kati ya waislamu na wakristo. Waislamu watadhania, Rais ameshinikizwa na wkristo kutoa maamuzi hayo, na hali wakristo watakuwa wakiendelea kumpongeza Rais kwa kufanya uamuzi huo na ndipo mtafaruku huu unatumiwa kuahirisha upatikanaji wa katiba hadi usuruhishi wa hoja utakapo patikana. Na hii ni kwa makusudi tu kwamba uchaguzi mkuu wa 2015 ufanike bila Katiba mpya. Mimi naona mpango huo upo na ndiyo maana Rais ametangulia kuutengenezea mazingira.
   
 7. m

  mtoto wa mama Senior Member

  #7
  Sep 8, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwani kuwaambia kuwa mahakama ya kadhi iwe chini bakwata si kulishughulikia hilo?!yaani kuna watu wanafiki nchi hii..ndio maana hatuendelei..
   
 8. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #8
  Sep 12, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tumia kichwa kuelewa wazo lililoletwa humu jamvini badala ya kukimbilia kuita watu wanafiki. Mbona unajidharirisha kwa kuonekana mwenye matatizo ya kuelewa wewe!!!!!!
   
Loading...