Mpango wa Kikwete ni EPA 'namba mbili'

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
MPANGO wa Serikali wa kuhami na kunusuru uchumi dhidi ya mtikisiko wa uchumi duniani, uliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete, umetiliwa shaka na kambi ya upinzani ambayo imesema unaweza kuleta "EPA namba mbili".

Makombora dhidi ya mpango huo yalitoka Kambi ya Upinzani Bungeni kupitia kwa kiongozi wake, Hamad Rashid Mohamed. Kambi ya Upinzani imependekeza mpango huo kutungiwa sheria maalumu ya udhibiti kwa kurejea uzoefu wa baadhi ya nchi za Asia.

Mapendekezo hayo yanatajwa kulenga kuinusuru nchi na kile kilichoelezwa kuwa ni “EPA namba mbili”, hasa ikizingatiwa kuwa katika wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), takriban Sh bilioni 133 zililipwa kwa kampuni nyingine hewa. Ikihofiwa kuwa huenda katika kufanikisha mpango huo na hasa suala la kufidia hasara za baadhi ya kampuni, zipo kampuni hewa.

Katika hotuba yake bungeni wiki hii, mjini Dodoma , Hamad Rashid Mohamed, kwa niaba ya wabunge wenzake kutoka vyama vya CUF, CHADEMA na UDP, alihoji masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya fedha hizo za stimulus package, zipatazo Sh. trilioni 1.7, zilizotangazwa na Rais Kikwete.

“Tunataka sheria ya Appropriation Act iwe na Schedule maalumu ya Stimulus Package na iseme waziwazi nani atapata nini, kamati ya Fedha na Uchumi ya Bunge iwe inapata taarifa kila miezi 3 ya utekelezaji wa hiyo stimulus package.

“Ni ukweli uliowazi kuwa stimulus package inazinufaisha benki tu, kwa kuzipa mwanya wa kufanya biashara nzuri na Serikali kwa kutumia fedha za Serikali yenyewe, na ndio maana katika nchi nyingine serikali imelazimika kuwa na hisa ili kuhakikisha kuwa fedha iliyotolewa ambayo inatokana na kodi za wananchi inadhibitiwa na kurudi kwa walipa kodi na wapiga kura.”

Hamadi alisema katika bajeti ya mwaka 2007/08 na ile ya 2008/09 serikali ilijizuia kukopa kwenye mabenki, kwa kigezo kikubwa kuwa mabenki yaweze kufanya biashara ya kukopesha sekta binafsi na kuwa zuio hilo liliongeza ufanisi kwa mabenki kukopesha sekta binafsi kwani mikopo kwa sekta binafsi ilipanda hadi kufikia asilimia 40.

Stimulus Package itapunguza mikopo ya benki kwenda kwenye sekta binafsi, na yale mafanikio yaliyokwishafikiwa yatayeyuka, vinginevyo mabenki yawekewe viwango vya kufikia katika kutoa mikopo nje ya stimulus package.

“Kwa mujibu wa taarifa ya Sera ya Fedha ya BoT serikali itazikopesha benki Sh bilioni 270 kwa ajili ya kuzikopesha sekta binafsi. Itatoa Sh bilioni 205 ili kukopa kwenye benki hizo.

Je, benki hizo zikishindwa kutumia fedha zile ambazo serikali imeziweka ili kukopesha sekta binafsi kutumia fedha hizo kufanya biashara na serikali kwa fedha za serikali? Hili litadhibitiwa vipi? Waziri atueleze,”, alihoji Hamad na kuongeza kuwa;

“Mwaka huu wa bajeti ni ya kuongeza matumizi na madhara yake ni mpango huo wa kuhami uchumi kuongeza mfumuko wa bei.

“Serikali imeamua kufidia vyama vya ushirika na kampuni zinazonunua mazao ya wakulima na kuyauza kwa hasara. Katika soko huria kuna kupata faida na kupata hasara. Wafanyabiashara makini wa mazao hupanga bei zao za kununulia mazao kwa kuzingatia bei walioipata katika soko la baadaye.

“Hata hivyo wengine hawapendi kuchukua tahadhari kwa kutegemea kwamba bei itapanda na kwa hiyo watapata faida kubwa. Bei imeshuka kwa hiyo wamepata hasara.Ó Alihoji akisema; Je, hakuna wafanyabiashara wa mazao waliolipa mikopo waliokopa kwa kujibana. Serikali ina uhakika gani kuwa mikopo hii ilitumiwa vizuri?”

Pia alipendekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua kampuni zitakazopewa fedha kutoka katika mpango wa kuhami uchuni.

Alitaka CAG kwanza kuthibitisha kuwa hasara waliopata haikutokana na matumizi mabaya ya mikopo na kwamba, gharama ya ukaguzi huu ilipwe na benki zilizokopesha. Alionya kuwa, la sivyo serikali inaweza kuliingiza taifa katika EPA namba mbili.

Kwa upande mwingine, Hamad katika hotuba yake hiyo alihoji kama serikali iko tayari kusaidia wafanyabiashara, kampuni na benki zilizopata hasara lakini bia kuwapo kwa hatua zozote za kuwasaidia wakulima wanaopata bei mbaya ya mazao isiyorudisha gharama.

“Hivi sasa wakulima wa pamba hawavuni pamba yao kwa kuwa bei ya pamba ni ya chini sana na hakuna soko la uhakika. Si hotuba ya Rais wala ya Waziri wa Fedha iliyotoa matumaini kuwa walalahoi pia wanakumbukwa na watafidiwa hasara na athari walizozipata kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani.

“Serikali imeamua kutoa udhamini wa madeni ambayo wakopaji kwa sababu ya msukosuko wa uchumi wa dunia wanapata matatizo kulipa kwa wakati. Madeni hayo yanafikia Shs.270 bilioni.

“Kuna hatari ya serikali kujiingiza katika kudhamini madeni ambayo hatimaye yatabidi yalipwe na serikali. Serikali inajiongezea mzigo wa madeni yanayoweza kutokea (Contigent Liabilities).

Serikali imeamua madeni haya yadhaminiwe kwa miaka miwili na siyo mwaka mmoja ili shughuli za Uchaguzi Mkuu wa 2010 ziwe zimemalizika. Hii itatoa mwanya kwa wanaodhaminiwa madeni wachangie kwenye kampeni na baada ya uchaguzi mzigo wa madeni ubebwe na serikali.

“Kuna hatari ya EPA nyingine kuzinduliwa. Ukaguzi wa kina wa mahesabu ya makampuni husika ufanywe na CAG kwa gharama za mabenki yaliyokopesha kabla ya serikali kuyadhamini makampuni haya,” alionya Hamad.

Kutokana na maelezo yake hayo, katika mazungumzo yake na Raia mwema nje ya ukumbi wa Bunge, Hamad alisema endapo Waziri wa Fedha na Uchumi hatatekeleza mapendekezo hayo na hasa suala la kutungia sheria stimulus package, basi wataamini kuwa huo ni mpango wa kuchota fedha ili zitumike katika uchaguzi kama ilivyo mabilioni ya fedha za EPA.

“Endapo serikali haitakubali haya na hasa suala la kuwapo kwa sheria ya usimamizi wa fedha hizo Sh trilioni 1.7 na pia kama haitakubali kampuni zitakazopewa fedha za kufidia hasara kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ni wazi kuwa tutakuwa tumethitisha mpango huo ni “EPA namba mbili” alisema Hamad.

Waziri Mkulo anatarajiwa kutoa majibu ya hoja hizo pamoja na hoja nyingine za wabunge kesho wakati atakapokuwa akijumuisha mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010. Ijumaa wiki hii, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwasilisha bajeti kwa ajili ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2009/2010.



Source: Mpango wa Kikwete ni EPA 'namba mbili' - Mbunge
 
Last edited by a moderator:
Kwanini hao unaowaita wapinzani hulaumu kila kitu cha Kikwete?

Sio kila kitu, ila kila wanachoona kina mushkeli. Halafu rekebisha maneno yako, unamuelekeza nani unaposema "unaowaita wapinzani"? Unalielekeza gazeti ama aliyenukuliwa (Hamad Rashid) ama aliyepost?
 
Halisi,
Mkuu achana na huyu asojua kilichoandikwa maana inaonyesha wazi alichokiona hapa ni Upinzani badala ya hoja husika na uzito wake kwa jamii... Taabu kweli kweli!
 
Kwanza naungana na watu na wale wote wazalendo wa Tanzania, lazima Bunge kusimamia mambo kama haya na pia kuna haja kuwa na sheria kwa kuomba fedha na sio kama hivi ilivyo sasa hivi
 
Tanzania bila CCM inawezekana kabisa. kuna watu wana vichwa (akili) safi kabisa ya kuliongoza taifa letu. Tazama hotuba ya Mh Ahmad Rashid ilivyojaa point za maana.

Tanzania inabidi tufikie mahali tukubali kuchanganya mawaziri katika serikali kama Kenya. Tuwe na mawaziri toka vyama vingine (tofauti) vya siasa ambao tunaona wazi kuwa wanaweza kufanya kazi vyema kwa faida na manufaa ya Taifa.
 
Tanzania bila CCM inawezekana kabisa. kuna watu wana vichwa (akili) safi kabisa ya kuliongoza taifa letu. Tazama hotuba ya Mh Ahmad Rashid ilivyojaa point za maana.

Tanzania inabidi tufikie mahali tukubali kuchanganya mawaziri katika serikali kama Kenya. Tuwe na mawaziri toka vyama vingine (tofauti) vya siasa ambao tunaona wazi kuwa wanaweza kufanya kazi vyema kwa faida na manufaa ya Taifa.

Hiyo hotuba nzuri isikupe shida,Hata Kikwete mwenyewe anayfahamu yote hayo vizuri sana huyo unayemwita kichwa aliyoyaongelea.
 
Inaelekea kweli kuna kadalili ka kamchezo kachafu ndani yake , Kama wataalam hawakuweza kuishtukia deal ingekuwa ile ile ya kampuni binafsi kuchota ma bilion ndani ya lisaa limoja.

Jk atakuwa amejaribu kuandaa kale kamchezo ka last time ili ajiweke pazuri 2010 nini ?
 
Kwanini hao unaowaita wapinzani hulaumu kila kitu cha Kikwete?

Tatizo hizo pesa sio za Kikwete, ni za walipakodi watz na nchi wahisani. Serikali yetu (chini ya Kikwete) haionekani kujali kile kilichotokea kwenye EPA!
 
Tanzania bila CCM inawezekana kabisa. kuna watu wana vichwa (akili) safi kabisa ya kuliongoza taifa letu. Tazama hotuba ya Mh Ahmad Rashid ilivyojaa point za maana.

Tanzania inabidi tufikie mahali tukubali kuchanganya mawaziri katika serikali kama Kenya. Tuwe na mawaziri toka vyama vingine (tofauti) vya siasa ambao tunaona wazi kuwa wanaweza kufanya kazi vyema kwa faida na manufaa ya Taifa.

Ndugu yangu Kidatu, huyo unayemwita kichwa (Hamad Rashid) ni kibaraka wa RA & Co. Kwahiyo usitegemee chochote cha maana kutoka kwake. Issue ya hotuba nzuri isikutishe wanasiasa wote wako hivyo wanapokuwa kwenye harakati za kutafuta madaraka na subiri wayapate ndo utajua walivyo kihalisia. Yeye (Hamad) na Lipumba wamekuwa mstari wa mbele kumshambulia Mengi wakati wa ugomvi wake na RA.
 
mpango wa stimuli wa jiki ni wizi...kuna uchumi gani wa ku stimuli tanzania.....hatuna viwanda ..hatuna mashamba makubwa...na hata tuki stimuli hatuna miundombinu ya usafirishaji mazao na umwagiliaji....sasa hizo hela si amelenga kuwapa jamaa zake kina subash patel,rostam na wengine kupitia kwa rafiki yake peter noni...watanzania tusikubali kufanywa mafala this time ....tukikubali watoto na wajukuu zetu watakuja kufukia makaburi yetu wachezee ngoma juu yake....!!!....wizi wa kimachomacho tu...tunaiga kila kitu marekani ...ujinga huu...wenzetu wana uchumi ambao upo mechanised kiasi ukiweka stimuli kweli unaona uhai ......

nchi zenyewe tajiri nyingine kama china na france wanapinga mipango ya stimulus......sisi tunakuwa dodoki tu!!!..shida ya kuwa na rais kibaraka ....anakuwa kama BO wa white house bwana!!
 
Hilo ni changa la macho jamani..hiyo pesa itaishia mifukoni mwa mifisadi...Tz pesa itolewayo kwa ajili ya mradi fulani huwa ni 32% tu inatumika ktk mradi na the rest iko mifukoni mwa watu...wewe ulishaona wapi ujenzi wa darasa moja la shule ya msingi tena kwa matofali ya kuchoma eti wanakwambia limegharimu 100m..?? WIZI MTUPU...
 
Unajua uchaguzi Serikali za Mitaa umekaribia na Uchaguzi mkuu mwakani utakuwa mgumu sana kwa "Chama Twawala". Hivyo ilibidi Jiki na team yake waje na mkakati mpya" New EPA" utakaowasaidia kupata fund za kushinda chaguzi zilizopo mbele yetu.
 
Back
Top Bottom