Mpango Uzazi (Majira)Unavyoiangamiza CCM Zanzibar

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Katika uchaguzi wa mwisho zama za ukoloni, "Ukawa" wa ZPPP na ZNP uliweza kuiangusha ASP kwenye sanduku la kura kwa kupata viti vingi zaidi kama sheria ya uchaguzi wakati huo ilivyotaka; na hivyo kupewa ridhaa ya kuunda serikali.

Lakini ASP pamoja na kushindwa walikuwa na mtaji wa watu ambao ulizidi idadi ya watu wa vyama hivyo viwili kwa pamoja kwa watu 10,000, ijapokuwa ilidaiwa ongezeko hilo lilikuwa ni la mamluki kutoka bara na ndio maana walijikusanya kwenye majimbo rafiki tu.ASP chini ya Field Marshall John Okello waliiutumia mwanya huo wa umma na kuiangusha serikali ya Moh'd Shamte.

Tokea ilipoanza siasa ya vyama vingi na vuguvugu la kujitawala tena likijirudia na kupamba moto, upinzani unaonekana kuja na mkakati mpya wa muda mrefu ambao unaonekana kuzaa matunda. Mkakati wenyewe ni kuhakikisha kuongeza wapiga kura kwa kuongeza idadi yao kwa njia za asili, yaani uzazi.

Kwa vile wakazi asili wa Zanzibar karibu wote ni waislamu, inakuwa rahisi kuwa hamasisha wananchi kuupinga mpango wa kupanga uzazi kwa vile njia zake pendekezwa zinakwenda kinyume na desturi, silka na mafundisho ya dini yao.

Ukiiangalia Zanzibar (unguja) maeneo yenye muamko mkubwa wa dini ni mjini na kaskazini na ndio majimbo yanayo watu wengi na ngome ya Upinzani (CUF). Inasemekana na ndio ilivyo kuwa CUF ina wapiga kura wengi zaidi Unguja kuliko Pemba.

Kusadikisha haya chunguza maelezo yafuatayo yaliofanyiwa utafiti wa kina!
1. Katika kila mtu mzima mmoja kutoka Pemba ( @ every given time ) ana sawia ya watoto wa nne ( wapiga kura watarajiwa)
2. Katika kila mtu mzima mmoja mwenye asili ya Pemba mwenye uwezo wa wastani na wa juu ana Wake wawili hadi wanne
3. Asilimia zaidi ya 60% ya Watu wenye asili ya Zanzibar, ima wana uhusiano wa kidamu, udugu wa karibu au wameoleana ( mchanganyiko maalum)
4. Katika kila uchaguzi asilimia ya wapiga kura wanapigia CUF inaongezeka kidogo na ile tswira ya 50 - 50 sasa inaondoka.
5. Unathubutu kutabiri kuwa uchaguzi wowote ambao utakuwa huru, uwazi na haki, chama cha upinzani hususan CUF kitashinda.
6.Kama CCM inataka kudumisha maendelezo yake ya ushindi wake usiokuwa na utata siku za usoni lazima wabadilishe mbinu za kukabiliana na ongezeko kubwa la wapiga kura halali,chama cha CUF kinavyowazalisha.
 
Back
Top Bottom