Mpango mkakati wa kuhakikisha wapinzani wanapata anguko kubwa uchaguzi Serikali za mitaa wabainika Iringa

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Katika zoezi linaloendelea wakati huu la kujiandisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.Imebainika kuwa ni wazi sasa Sirikali kupitia viongozi wake wote wa Mikoa na Wilaya wamepewa maagizo na mikakati thabiti ya kuhakikisha wapinzani wanashindwa kwa njia yoyote ile.Bahati nzuri jana na juzi nilikuwa hapa Mkoani Iringa Mjini na katika pita pita yangu ikiwa ni pamoja na kujifanya kada wa chama tawala haya ndio nimeweza kuyaona na kuyashuhudia kwa macho yangu: Katika kikao cha mwisho cha kuwapa maelekezo wasimamizi wa uandikishaji hapa mjini kilichoongozwa na katibu wa chama hapa mkoani na maelekezo yalikuwa ni lazima wasimamizi wa uhandikishaji wafanye yafuatayo a) Hakikisha kunakuwepo jitihada za makusudi za kuwatambua wapinzani wakati kujiandikisha (walipewa mbinu mbadala) mojawapo ni kumuhoji kwa kujaribu kukejeli chama tawala au kama anafahamika kwa wawakilishi wa chama tawala (yaani wasimamizi wa kituoni) basi akishajiandikisha jina lake linawekewa alama fulani.Lengo ni kwamba zoeozi likimalizika wanayawekea dosari majina ya upinzani kwa.mfano mtu kama umeandika jina "Juma" wao wataandika "luma" watakapotoa majina ya mwisho kabisa.Sasa ukija kuhakiki jina utakuta limekosewa na utazungushwa na hutopiga kura au ukija siku ya uchaguzi ukija utafukuzwa kwani sio jina lako.(b) viongozi wa vituo wanapelekewa majina yasiyopungua kumi kila siku "fake". Mwisho kabisa ni endapo mpinzani atashinda asitangazwe mshindi bali atangazwe wa chama tawala.
 
Back
Top Bottom