Mpangaji mwenzangu anahisi natembea na mkewe kutokana na mazoea

Kuna familia moja tumepanga wote ni vijana tu wana kama miaka 24 25 hivi wana mtoto mmoja ni familia yenye uchumi wa chini sana hii imefanya mtoto wao wa umri wa miaka kama mitatu hivi kua ana mendea chai kila siku asubuhi mida ya chai yupo kwangu

So hio ikafanya tukazoeana na mama yake. Maana mara nyingi mtoto wao anashinda kwangu, mumewe sina mazoea nae saana zaidi ya salam tu

Juzi kati hivi mida ya jioni huyu dada aliniita na akaomba nimkopeshe buku 5 me nikampa muda huo tunazungumza mume akawa kalejea home akakuta tunazungumza pale akapitiliza ndani bila salam

Kesho yake nikaja kuambiwa na mpangaji mwingine kua huyu dada alienikopa pesa alipigwa na mumewe, so moja kwa moja nikaunganisha dots

Nikaona ngoja nipunguze mazoea na huyu dada ijapokua ni mtu wa vimizinga mizinga sana

Baadae huyu kaka akawa anampiga mwanae akija kula kwangu but dogo hasikii akiamka tu huyu hapa so na sipendi kutia doa ndoa yao mda mwingine naweza kumpa chakula nikatoka nikakuta akabeba akaenda kulia kwao, na kiukweli hii familia msosi ni wa tabu,

Nakua na kamuunganiko fulani hivi jambo ambalo naliiona si zuri je niwe nafukuza huyu dogo ili nikate connection au nifanyaje?
Kaa mbali na huyo bidada,hata kama huna nia ya kula mzigo,Mumewe atakushuku tu,imeanzia kukopeshana pesa,itafika point huyo dada ataanza kukusimulia mambo yake,na Mumewe,zile siri za ndani zinazohusu Hari ya kipesa,na mateso anayopata,kabla hujashituka utaanza kumwachia pesa,Ili apike,dogo ale vzr,ikifika hapo Ngosha,unatafuta balaa la kupigwa panga,
Yameishawahi nikuta,
Mimi mpaka mke wa jamaa,alipochoka maisha magumu,ya kupigwa,akaniambia ana hama,na siku ana hama akataka nimsadie kubeba vitu vyake kwenye ndinga yangu,mie bila kujua,nikabeba,jamaa yake aliporudi usiku,akakuta ghetto patupu,majirani wakamuhuma sikio,kwamba huyu jirani yako mwenye Prado,ndio kampangia chumba na kumuhamisha mkeo.
Jamaa tulikuwa hatusalimiani kabisa,mpaka nilipohama,
 
Yeah jamaa anajisikia vibaya sana hata ungekua wewe, hapo ni kuzoena na kamanda mwenzio kama una cha kumsaidia mpe mwanaume mwenzio, unamshushia sana thamani yake! Huyo mwanamke mkiendelea hivyo mtakulana na hapo ndio litakua balaa la hatari
 
Back
Top Bottom