Mpambano mkali wa Mkuu wa mhimili wa Serikali na Bunge, ni "neema" kwa Vyama vya Upinzani

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Nimemsikiliza kwa makini Rais Samia Suluhu Hassan, akimpa "za uso" Spika Ndugai, kuhusu kile alichotufunulia ni kuwa ni mbio za Urais wa 2025, angalau kimebatizwa jina na hao mahasimu wake kuwa ni deni la Taifa linalohatarisha usalama wa nchi yetu kupigwa mnada.

Hoja pekee na ya nguvu niliyoisikia, ni pale aliposema kuwa mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais, alitembelewa na mtu mzito Sana wa CCM na kumnong'oneza kuwa Hongera zake na Pole nyingi.

Huyo mtu mzito akamfafanulia kuwa Hongera hiyo na Pole, ina maana kubwa, kuwa Kazi aliyonayo mbele ni ngumu Sana, kwa kuwa adui zake wa dhati, watakuwa ni wa upande wake wa kijani wenzie na wala siyo viongozi wa vyama vya upinzani!

Leo Mama katufafanulia kuwa ame-realize kuwa alichoambiwa na huyo mwanaccm mwenzie ni ya kweli kabisa na ndiyo yanayoendelea hivi sasa ndani ya CCM yake.

Ninachokiona Mimi ni kuwa mpambano huu mkali ambao kama nchi hatujawahi kuushuhudia, wa vita vya wenyewe kwa wenyewe maccm watupu, utawapa unafuu mkubwa na kupumua wa kuendesha shughuli zao za kisiasa, baada ya mateso makubwa ya muda mrefu, kwa vyama vya upinzani.
 
Wapinzani ambao hawajielewi watakumbilia kusupport serikali kuu na kama kawaida ya CCM watawavutia waya, badae wanawasafisha kama kawa
 
Kitu muhimu kabisa ni kwamba Samia kawagundua maadui zake tena ni wengi.

Kagundua kuwa sisi Wapinzani sio maadui zake very important.

Huyo mtu 'mzito wa makamo' aliyemshauri ndie amfanye mshauri wake wa kudumu wa mambo ya kimkakati.

Sisi Wapinzani tupewe Katiba mpya ya wananchi tu ili tunyamaze.
 
Kitu muhimu kabisa ni kwamba Samia kawagundua maadui zake tena ni wengi.

Kagundua kuwa sisi Wapinzani sio maadui zake very important...
Hakika ni muda muafaka wa Taifa hili kuipata Katiba mpya, badala ya hii Katiba iliyopo kupigwa viraka endlessly
 
Back
Top Bottom