Siamini macho yangu kama inafika kipindi mtu unafilisika mpaka mawazo, yaani hujui nini cha kufanya ili maisha yasonge mbele lkn ukweli mtupu haya ndo ninayopitia Mtanzania mwezenu.
Historia yangu kiufupi ni hivi, Mimi ni muhitimu chuo kikuu (UDSM) kada ya ualimu wa sanaa (Art), na kama mjuavyo hii fani ina changamoto katika ajira.
Nilihitimu mwaka 2018 na baada ya nilijaribu kutuma maombi shule mbalimbali bila mafanikio, lakini Mola hamtupi mja wake nilipata kibarua kimoja hivi ambacho nashukuru Mungu kilifanikisha kunivusha sehem A kwenda B japo nilifanya kwa muda wa miaka 2.
Niliweza ku-save kiasi cha sh mil 2 hivi ndani ya huo muda na kibarua kilikoma mwezi wa kumi mwaka huu (2020).
Mpaka sasa nna mwezi wa tatu huu niko tu ndani kiufupi nimenasa katika jela ya mawazo yani kila biashara ninayoifikiria nahisi haiwezekani mpaka imepelekea naugua ulcers kwa mawazo nilonayo.
Jamani jela ya kifikra ni mbaya mno, maana nafikiria hiki kitu nilichokitafuta kwa miaka 2 kikipotea itakuaje!
Bahati mbaya sina hata wazazi wa kunipa motisha kwamba wapo nyuma yangu kwani walifariki nikiwa mdogo.
Mpaka najuta kabisa kwanini nilitumia muda mwingi kwenye kusoma halafu nakuja kufanya kazi ambazo ni out of field.
Sasa basi naombeni ushauri wenu jamani nifanye nini mana dahhh hela nilonayo ndiyo inazidi kupukuchuka, maisha ya Dar kila siku ni hela yani nahisi kukata tamaa.