Mpaka sasa, JPM kawatandika vibaya sana wapinzani

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Hivi ndivyo walivyoanza tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwezi mei mwaka 2015.

1. Ndani ya CCM hakuna wa kumkata LOWASSA, akakatwa.

2. CCM hawawezi kumpitisha Dr. Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Akapitihswa.

3. Kipindi cha awamu ya nne walilalama sana kuwa Rais anasafiri sana, Dr. Magufuli akaona isiwe tabu , akakata kiu yao, KIGEUGEU haishi kulala, wakamtuma SUGU kurapu Bungeni.

4. Baada Magufuli kupitishwa kuwa mgombea kupitia CCM, wakasema "TATIZO SIYO MTU, TATIZO MFUMO" leo wamekaa kimya.

5. Baada ya kuanza kutumbua majipu, wakasema ni Nguvu za Soda, mpaka leo yanatumbuliwa.

6. Walipoona siyo nguvu za soda, wakasema Magufuli anatekeleza ilani ya chama chao na huku wakisema wanaoisoma namba ni wana CCM, mara wakaanza oh, wafanyabiashara waliosaidia Kampeni zao wananyanyaswa, mara oh, watumishi wanasimamishwa kazi bila kupewa nafasi ya kujitetea. Hao si wana CCM wanaoisoma namba, wapinzani kwanini wanaweweseka badala ya kufurahi?

7. Haya wametaka mshahara wa rais, ni mil. 9.5, rais mwenyewe alipiga Simu TV clouds kutangaza mshahara wake, sasa wanataka Posho na Marupurupu yake, wanatapatapa tu.

Prof. Kitila Mkumbo alishawatahadharisha kuwa "WASIPOBADILIKA NA KUENDELEA KUSUBIRI CCM IHARIBU, KWA UTAWALA WA JPM WANAWEZA KUWA NA WAKATI MGUMU".

Dr. Slaa naye kawatahadharisha juzi akiwa Canada.
 
Hivi ndivyo walivyoanza tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwezi mei mwaka 2015.

1. Ndani ya CCM hakuna wa kumkata LOWASSA, akakatwa.
2. CCM hawawezi kumpitisha Dr. Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Akapitihswa.
3. Kipindi cha awamu ya nne walilalama sana kuwa Rais anasafiri sana, Dr. Magufuli akaona isiwe tabu , akakata kiu yao, KIGEUGEU haishi kulala, wakamtuma SUGU kurapu Bungeni.
4. Baada Magufuli kupitishwa kuwa mgombea kupitia CCM, wakasema "TATIZO SIYO MTU, TATIZO MFUMO" leo wamekaa kimya.
5. Baada ya kuanza kutumbua majipu, wakasema ni Nguvu za Soda, mpaka leo yanatumbuliwa
6. Walipoona siyo nguvu za soda, wakasema Magufuli anatekeleza ilani ya chama chao na huku wakisema wanaoisoma namba ni wana CCM, mara wakaanza oh, wafanyabiashara waliosaidia Kampeni zao wananyanyaswa , mara oh, watumishi wanasimamishwa kazi bila kupewa nafasi ya kujitetea. Hao si wana CCM wanaoisoma namba, wapinzani kwanini wanaweweseka badala ya kufurahi?
7. Haya wametaka mshahara wa rais, ni mil. 9.5, rais mwenyewe alipiga Simu TV clouds kutangaza mshahara wake, sasa wanataka Posho na Marupurupu yake, wanatapatapa tu.

Prof. Kitila Mkumbo alishawatahadharisha kuwa "WASIPOBADILIKA NA KUENDELEA KUSUBIRI CCM IHARIBU, KWA UTAWALA WA JPM WANAWEZA KUWA NA WAKATI MGUMU". Dr. Slaa naye kawatahadharisha juzi akiwa Canada.
Mbona unaichukulia siasa kama mchezo wa ngumi au mpira wewe???vyama vya upinzani vipo kikatiba,kutoa mawazo yao yapo kikatiba ,kusimamia serikali na kuikosoa ipo kakatiba .Sasa wewe unataka waseme tunavunja vyama??mpinzani hana chapa hata wewe yanaweza kukufika ukajiunga upinzani
 
Tanzania hakuna vyama vya siasa, unavyoviona ni vikundi tu vya wasaka pesa ni vigumu sana kuvitofautisha na NGOs! Hapa kwetu mtu anaanzisha chama kwa kukopa hela benki unategemea nini!
 
Jiulize utakula nini leo mchana, mambo mengine yako nje ya uelewa wako. We unafikiri kudhibiti wapinzani ndo kazi aliyotumwa? Watanzania tuna matatizo yetu na yanajulikana, kama wapinzani wakiona jambo na wakalipigia kelele likarekebishwa bado mnaendelea kuwaona hawafai?

Kama utaweza kutulia na kuangalia mambo bila ushabiki utaona kuwa bila wapinzani kuwepo tungekuwa bado tunatembea na kandambili. Mwache Rais atumbue majipu na waache wapinzani wapige kelele ili hatimae nchi isonge mbele na wananchi tuishi vizuri.
 
Tanzania hakuna vyama vya siasa, unavyoviona ni vikundi tu vya wasaka pesa ni vigumu sana kuvitofautisha na NGOs! Hapa kwetu mtu anaanzisha chama kwa kukopa hela benki unategemea nini!
hivyo vikundi unavyosema ni NGO ndo hivyo vimepewa umiliki wa JIJI KUU LA DAR na utatii amri zao bila shuruti.
 
Jiulize utakula nini leo mchana, mambo mengine yako nje ya uelewa wako. We unafikiri kudhibiti wapinzani ndo kazi aliyotumwa? Watanzania tuna matatizo yetu na yanajulikana, kama wapinzani wakiona jambo na wakalipigia kelele likarekebishwa bado mnaendelea kuwaona hawafai?

Kama utaweza kutulia na kuangalia mambo bila ushabiki utaona kuwa bila wapinzani kuwepo tungekuwa bado tunatembea na kandambili. Mwache Rais atumbue majipu na waache wapinzani wapige kelele ili hatimae nchi isonge mbele na wananchi tuishi vizuri.
Kwa mara ya kwanza , naona mmenyooka.
 
Wapinzani ni wa muhimu sana, ila tu kwa sasa sijaona hoja ya msingi wanayoitoa kuisaidia serikali wamebaki ni blabla tu, ni kweli JPM kawachanganya mno, tunataka iupinzani wenye hoja za msingi si upinzani wasaka tonge.
 
Lumumba acheni kujadili historia, kakatwa Membe ndugu wa JK itakuwa Lowasa? sasa hivi habari ya town ni ccm kukumbatia rushwa mnawaambiaje wananchi? Magufuli kajitandika mwenyewe ndio maana kajipa likizo kabla hata hajamalizaa mwaka ofisini nae ni JIPU.
 
Hujamaliza bado.

Kwamba uhusiano wa kidplomasia na nchi za nje umeimarika na uwezo wa kukopesheka uneongezeka na wahisani wa bajeti yetu finyu wameongeza utayari wao kusaidia (MCC, UK na EU).

Wananchi kugundua kuwa wabunge wa vyama vya upinzani hususani wa "Chadema" ni wala rushwa wakubwa baada ya wanne kuoelekwa mahajamani na wengine 18 wako njiani.

Wafanyabiashara wakubwa ambao ni wafadhili wa "Chadema" kujulikana kuwa ndio wakeepaji wakuu wa kodi na uvujaji wa makontena.

Endelea kuonyesha ubora wa ccm bila kusahau habari ya magazeti Leo kuwa Ulaya "imefurahishwa sana" na jinsi ccm inavyo dumisha demokrasia na hizo Trilioni 2.1 ilizokuwa imetenga kusaidia maendeleo ina mpango wa "kuziongeza"
 
Wananchi Je Wamepata Huduma Nzuri ya Afya?Wananchi Wamekula Milo Mitatu na Kushiba?Elimu Inayotelewa Imekidhi?Haki Inatolewa kwa Wakati Mahakamani?Kilimo cha Jembe la Mkono Kimeisha?Ajira za Viwandani Zipo?Umeme na Maji Vijijini Vinapatikana?Barabara na Reli Za Kubebea Mizigo Bandarini Kwenda D.R.C,Uganda,C.A.R zipo?Kenya Wako Mbioni Kutunyang'anya Wateja wa Bandari Yetu Wanaotukimbia Kwenda Beira na Durban,na Hivyo Bandari Yetu Kukosa Mapato,Serikali Imefanyaje?MAGUFULI AKIMALIZA HAYO,UPINZANI LABDA UTANYAMAZA!NA MAENDELEO YATAKUWA YASHAPATIKANA AMBALO NDILO LENGO LA UPINZANI
 
Hujamaliza bado.
Kwamba uhusiano wa kidplomasia na nchi za nje umeimarika na uwezo wa kukopesheka uneongezeka na wahisani wa bajeti yetu finyu wameongeza utayari wao kusaidia (MCC, UK na EU)
Wananchi kugundua kuwa wabunge wa vyama vya upinzani hususani wa "Chadema" ni wala rushwa wakubwa baada ya wanne kuoelekwa mahajamani na wengine 18 wako njiani.
Wafanyabiashara wakubwa ambao ni wafadhili wa "Chadema" kujulikana kuwa ndio wakeepaji wakuu wa kodi na uvujaji wa makontena.
Endelea kuonyesha ubora wa ccm bila kusahau habari ya magazeti Leo kuwa Ulaya "imefurahishwa sana" na jinsi ccm inavyo dumisha demokrasia na hizo Trilioni 2.1 ilizokuwa imetenga kusaidia maendeleo ina mpango wa "kuziongeza"
mkuu mtoa mada ni mmoja wa makada wanao fanya siasa mihemko!na ndio mmoja wa wanaccm ambao GENTAMYCINE aliyowaita kuwa ni CCM JUHA!
 
Hawana athali yeyote juu ya jiji na kwa kifupi hutawasikia!
wewe utaijuaje athari wakati ni mpolipoli.... wenzio wanajianda kukata rufaa kwa kuogopa hizo athari afu wewe unakuja na ulugaluga wako eti asali:mad:

...athali ndo nini???
 
Back
Top Bottom