#COVID19 Hadi sasa hakuna mkakati wa matumizi ya bima ya afya na mpango kuwasaidia wagonjwa wa Corona kupunguza gharama za matibabu

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Kama tunavyojua kuwa wimbi la tatu la ugonjwa wa korona linatupiga ipasavyo na japokuwa serikali inaendelea kupokea misaada ya fedha kutoka WHO na mashirika mengine lakini cha ajabu hakuna mikakati yoyote ya kupunguza gharama za mgonjwa wa Korona.

Kwa mfano dozi moja ya korona mpaka sasa si chini ya laki na nusu na mgonjwa anatakiwa kupata dozi si chini ya kumi, kwa upande wa mtungi mmoja wa gesi ya oxygeni ambao unatumika kwa masaa 24 tu unagharimu laki moja moja ya masharti ya misaada inayotolewa na Shirika la Afya la Dunia yaani (WHO) ni kuwapunguzia makali ya gharama wananchi katika kupambana na ugonjwa korona, lakini kwa hapa Tanzania yaani ni kama vile serikali haijui chochote kuhusu hili. Wananchi wanateketea kila saa kwa ugonjwa huu.

Serikali inabidi kuliangalia hili ukizingatia pia tozo za miamala nazo zinatuminya ipasavyo.
 
Na baadhi ya hospitali hazipokei wagonjwa kwa sasa, na kama wakikubalia kukulaza utaambiwa uweke kuanzia 1m ili wakuanzishie matibabu
 
Kunahaja ya kuchukua tahadhari zote asee.
corona is inavetable!!huwezi kuikwepa oga nawa vaa barakoa jipikie mwenyewe nyumbani au jifiche chini ya uvungu usitoke itaufata huko huko. Hutaamini macho yako umeipataje!tuombe mungu tuu maana mi hadi hapa siamini huu ugonjwa ni wa hewa!labda upo kwenye maji yote tunayokunywa au kuyaoga
 
Niko kitandani nikiugua huu ugonjwa. Mwenyezi MUNGU anisimamie/atusimamie.
Pole sana mkuu. Ilianza kuugua rasmi kuanzia lini? Na ni zipi hasa changamoto(dalili) zinazokupata mwilini kwa sasa ambazo unaamini zimeletwa na corona?
 
Kama tunavyojua kuwa wimbi la tatu la ugonjwa wa korona linatupiga ipasavyo na japokuwa serikali inaendelea kupokea misaada ya fedha kutoka WHO na mashirika mengine lakini cha ajabu hakuna mikakati yoyote ya kupunguza gharama za mgonjwa wa Korona.

Kwa mfano dozi moja ya korona mpaka sasa si chini ya laki na nusu na mgonjwa anatakiwa kupata dozi si chini ya kumi , kwa upande wa mtungi mmoja wa gesi ya oxygeni ambao unatumika kwa masaa 24 tu unagharimu laki moja moja ya masharti ya misaada inayotolewa na Shirika la Afya la Dunia yaani (WHO) ni kuwapunguzia makali ya gharama wananchi katika kupambana na ugonjwa korona lakini kwa hapa Tanzania yaani ni kama vile serikali haijui chochote kuhusu hili , wananchi wanateketea kila saa kwa ugonjwa huu.

Serikali inabidi kuliangalia hili ukizingatia pia tozo za miamala nazo zinatuminya ipasavyo.
CCM haiko kwa ajili ya kuwatetea walala hoi, CCM ni Chama tetezu Cha matajiri wakubwa
 
Pole sana mkuu. Ilianza kuugua rasmi kuanzia lini? Na ni zipi hasa changamoto(dalili) zinazokupata mwilini kwa sasa ambazo unaamini zimeletwa na corona?
Nina siku 5 sasa, changamoto ni maumivu mwili mzima, mafua, kikohozi, kifua kuuma/kubana, kuchoka, mdomo kupoteza test yani hauhisi ladha wala harufu!
 
bima inatumika kwa UTI na MALERIA
Bima ya Afya ni kichochoro cha mapato ya serikali its fullsh busness, hamna kitu pale ukiangalia katika nchi mbalimbali duniani hakuna Bima feki kama ya Tanzania imejaa propaganda na usanii mwingi ni Bima ya kutibu kichocho , malaria , kipindupindu na UTI
 
third part insurance!
 
Back
Top Bottom