MOTOCHINI
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 27,778
- 30,748
MGOMBEA Donald Trump ameshatumia $55milioni kutoka mfukoni mwake kwenye kampeni za kusaka Urais wa Marekani, Novemba mwaka huu.
Kama akishindwa uchaguzi wa Marekani, Donald Trump atakuwa mgombea aliyepoteza zaidi.
Ni kwasababu hadi kutajwa kuwania urais wa mwaka huu kupitia chama chake cha Republican, bilionea huyo ametumia kitita cha mfuko wake mwenyewe kugharamikia kampeni zake bila ya kupewa msaada wowote.
Akiongea wiki hii, Trump amesema haoni tatizo iwapo atatumia tena fedha zake mwenyewe kugharamikia kampeni za uchaguzi huo mkuu ambapo anachuana na Bi.Hillary Clinton.
“Nimetumia dola 55 milioni kutoka mfukoni mwangu kufadhili ushindi wangu wa michuano ya awali kuwania tiketi za chama.
Hicho ni kiasi kikubwa cha hela ukizingatia sikusaidiwa na nafikiri huenda nikafanya hivyo tena kwenye uchaguzi mkuu” akasema.
Aliongeza kuwa pamoja na kwamba fedha aliyonayo ni nyingi na kutosha kufanya mwenyewe, ni vyema akapewa msaada na chama pia.
Hadi sasa Trump amekusanya dola milioni 1.3 huku mpinzani wake, Clinton wa chama cha Democratic akionekana kuwa vyema zaidi.
Hadi sasa Bi Clinton amekusanya zaidi ya dola milioni 42. Clinton na wadhamini wake wanatarajia kutumia dola milioni 117 kwaajili ya matangazo ya TV tu.