Mpaka sahihi ya Pinda inagushiwa bado wanacheka cheka, kweli hii serikali ni legelege kupitiliza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka sahihi ya Pinda inagushiwa bado wanacheka cheka, kweli hii serikali ni legelege kupitiliza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtz Halis, Jul 28, 2011.

 1. M

  Mtz Halis New Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Saini ya Pinda yaghushiwa bungeni [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Mwananchi, Wednesday, 27 July 2011 21:32 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Neville Meena na Habel Chidawalo
  VITUKO vya wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimezidi kuongezekana; sasa baadhi ya wabunge wanadaiwa kugushi sahihi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa malengo ambayo bado hayajafahamika.

  Kitendo cha kugushi sahihi ya Waziri Mkuu ndani ya ukumbi huo kunawaathiri zaidi wabunge wa upinzani, hasa wa Chadema ambao wamekuwa wakipelekewa ‘meseji’ za kuwadanganywa kuwa wanaitwa na Waziri Mkuu.

  Juzi jioni kabla ya kikao cha Bunge kuahirishwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alialazimika kuomba mwongozo wa Mwenyekiti kukemea kitendo hicho alichokiita kuwa ni cha kihuni.

  Lukuvi asimama mara tu baada ya Bunge kumaliza kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ambayo yalikuwa yalijadiliwa kwa siku mbili mfululizo.

  “Naomba mwongozo wako kwamba, humu ndani imejitokeza tabia ambayo naona imezoeleka kidogo. “Kuna watu wanawaandikia wenzao meseji za kuwasumbua kwamba wanaitwa na mtu fulani halafu wanaweka sahihi na wakati mwingine haitokei,” alisema Lukuvi na kuongeza:

  “ Nimeisikia hayo wiki iliyopita, lakini leo Mheshimiwa Joseph Selasini (Chadema) ameitwa kwa meseji inayodaiwa kuwa imesainiwa na Waziri Mkuu na hii nyingine ameitwa Mheshimiwa Leticia Nyerere (Chadema) kwamba anaitwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wakazungumze maneno ya maana, lakini Waziri Mkuu hana habari na wamegushi sahihi yake,’’ alisema Lukuvi.

  Waziri huyo wa Sera, Uratibu na Bunge alitaka mwongozo wa Mwenyekiti kama jambo hilo linaweza kufanywa na Wabunge, ndani ya Bunge kwa wabunge kugushi taarifa ambazo alisema nyingine na zinatisha.

  Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alikiri kuwepo kwa tabia hiyo ndani ya ukumbi wa bunge ambayo imekuwa ikifanywa na baadhi yao na kamba inaonekana kuota mizizi.

  “Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri, ni kweli kuna mtu amefanya hivyo na karatasi aliyoiandika ipo hapa, Kwa kweli siyo nzuri haionyeshi kama tupo serious (makini) na kazi,” alisema Simbachawene na kuisoma:

  “Amemwandikia hivi, Mheshimiwa Joseph Selasini Mbunge, samahani nakuomba mara moja tuje tujadili suala moja muhimu ambalo ningependa kujua kutoka kwako. Ahsante. Mizengo Peter Pinda na sahihi”.

  Simbachawene alisema Selasini alipokwenda kwa Waziri Mkuu alishindwa kusaidiwa kwa kuwa wakati huo Waziri Mkuu alikuwa makini kusikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika majumuisho yake.

  Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema uongozi wa Bunge utafanya kila liwezekanalo kubaini ni nani mwenye tabia hiyo na kwamba ili kukomesha vitendo hivyo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Magamba propagandaz at their best
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nashindwa kuelewa hawa viongozi wetu akili zao ziko makalioni au sijui vipi!! Hapo kwenye RED, Huyu mwenyekiti anazo taarifa kwa muda mrefu lakini ameendelea kuzikalia tu kama vile ni jambo dogo sana hilo la kugushi, tena sahihi ya PM, pia kusababisha usumbufu kwa wengine. Amenyamaza tu.... ina maana Lukuvi asingeongea basi ujinga huu ungeendelea.

  Mkiambiwa kuondoa viti maalum na wabunge Ma naunga mkono asilimia mia hamtaki. sasa ndo kazi hiyo tuliyowatuma na kuwalipa posho
   
Loading...