Mpaka mwanamke aharibu, basi nyuma yake kuna mwanaume/wanaume walishaharibu

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,023
71,229
NB.. siandiki haya Kwa sababu labda nawapendelea Wanawake , au natafuta Wanawake, la Hashaa, Nina Mke na nina Wanawake zangu Kadhaa huku nje tunasogeza life bila stress !!.

Turudi kwenye Mada,. Unajua tangu ulimwengu kuumbwa, Mwanaume akapewa ,Ufalme, Uongozi ,Umiliki na Utawala Kwa Mwanamke na viumbe vyote hapa Duniani, Baharini n.k.

Unajua Adam alivyoumbiwa Mkewe, aliambiwa aambatane naye ,asimwachee, lakini Adam kwakua alinogewa na kazi ya kuwapa Viumbe majina, akajikuta kamuacha Hawa pekeake, naaaaam unaona anatoa Fursa ya Shetan kuingia Kwa Hawa, na Hawa anaingia mtegoni ( Funzo la kwanza, Mwanaume usimuache mkeo mbali, shetan Atamshinda maana wewe ndio umeruhusu).

Tuendelee, Dunia Kwa Sasa inapitia Kipindi ambacho kina mmonyoko mkubwa sana wa maadili , nahivo ikiwa SISI WANAUME TUTAUSAHAU UANAUME WETU, aisee tunaenda kua na kizazi Cha hovyo kupindukia., Sio Wanawake zetu ,sio watoto wetu yaaan hamna Mahali tutapata unafuu ....

Unaweza shangaa...

Ushoga ,unatetewa na wanaume.

Wanawake kusagana, wanatetewa na wanaume.

Habari za kubadili jinsia , zinatetewa na wanaume.

Yaan Kila jambo la kustaajabisha linatetewa na Mwanaume na wanaume tunalipigia chapuoo haswaa.

Sasa Tuje kwenye suala Zima la Mahusiano...

Ulishawah jiuliza kwann Mpenzio/ Mkeo anachepuka?....

Jibu ni rahisi wewe Mwanaume ulishaanza kuchepukaa kitambooo

Ulishawah jiuliza kwann Mkeo/Mpenzi anakudharau ,hakuheshim, ? Jibu nikwamba nyuma yake wewe kidume ulishaharibu yaan umeharibu kiasi Cha kumwondelea mwanamke uthamani wake..

Ipo Hivi, ubongo wa mwanamke regardless of her age, umekua programmed KUMTII MWANAUME WAKE... Yaan ni sawa na ubongo wa mtoto Mdogo , haijalishi huyo mwanamke ana Elimu gan, uchumi gan, mwonekano upi, wewe Jua ubongo wake umeumbwa kuongozwa Nawewe Mwanaume.

Sikatai kwamba hamna Wanawake wapumbavu, wapo na hata maandiko yameweka wazi kua "Mwanamke mpumbavu"....... Wengi neno hili tunalitafasiri kama lilivyo..

Andiko hili lililenga Upumbavu wa mwanamke licha ya UKAMILIFU WA MWANAUME WAKE.. ikiwa na Maana, wewe Mwanaume kwanza uwe mkamilifu ,Kiongozi, Mtawala, Mwenye mamulaka Kisha ndio tuone kama atakuwepo mpumbavu mwanamke ? Na akiwepo basi huyo ni lazima ataibomoa nyumba yake.

Wanaume tumekua waongoooo sana, Huu uongo umewafanya Wanawake nao waanze kua waongo sana.

Maisha yamejaa ujanja ujanja tuu , tumewafanya Wanawake nao waishi nasi Kwa kuogopana, yes , ndio maana nao Kwa Sasa Wana makoloni yao Kadhaa Kadhaa!!.

Kuna Mwanaume /Wanaume mnasoma hapa, miezi au miaka ilopota, mmeumiza Wanawake Fulani , hivi hao Wanawake mnadhan Leo wakoje ?. Na wao wanaumiza sababu waliumizwa, nawao hawapo serious sababu waliumizwa !!!.....

Unakuta Mwanaume mchepukaji Et nawee unalalama, Mke wangu vile, Mpenzi wangu vile 😂.... Weweeee Vumilia tu Ndugu yangu !!!

Tena, Kwa Mabadiliko haya ya kiglobalizeshen yanayoendeleaa , Shetan anapambana kupoteza nguvu ya Uanaume ., tusiposimama Ngangari , Duuuhh Sijui !!.
 
Kuchepuka kwa wanaume ni by nature, tangu zamani tumeona wanaume wakiwa na wake wengi na hakuna tatizo, pia tangu zamani pamekuwepo wanawake wanaochepuka, tumeona kwenye vitabu vya kale wakitajwa malaya.

Mwanamke a-promote ushoga kwa mahitaji gani sasa!?

Ninachotaka kusema, hakuna matendo mapya! Vyote vilikuwepo isipokuwa internet/utandawazi kwa sasa ndo shida.
 
Unahalalisha uchepukaji kwa wanawake.

Mchepukaji hakosi sababu ya kujitetea, mzinzi ni mzinzi tu hakuna upweke wala mwanaume hivi na vile.
 
Yaan ni sawa na ubongo wa mtoto Mdogo , haijalishi huyo mwanamke ana Elimu gan, uchumi gan, mwonekano upi, wewe Jua ubongo wake umeumbwa kuongozwa Nawewe Mwanaume."

UONGO.

Ukweli ni kuwa, ubongo wa mwanamke upo programmed kuongozwa na ubongo wa mwanaume unaomtatulia matatizo yake. Either ya Kifamilia, Kiuchumi, Kiulinzi n.k.

Sio kila mwanamke ww Carlos utaweza kumwongoza sababu ww ni mwanaume, kuna ambao watakuona wewe ni weak kulinganisha na mahitaji yao au uwezo wao wa akili na mambo anayofanya kulinganisha na yako.
 
Kuishi na mwanamke kwa akili( Kama jinsi tulivyoamrisha kwenye maandiko matakatifu) ndicho kitu muhimu kuliko vyote.

Kujaribu kumwelewa mwanamke Ni sawa sawa na kuupaka upepo rangi.
 
Kuchepuka kwa wanaume ni by nature, tangu zamani tumeona wanaume wakiwa na wake wengi na hakuna tatizo, pia tangu zamani pamekuwepo wanawake wanaochepuka, tumeona kwenye vitabu vya kale wakitajwa malaya.

Mwanamke a-promote ushoga kwa mahitaji gani sasa!?

Ninachotaka kusema, hakuna matendo mapya! Vyote vilikuwepo isipokuwa internet/utandawazi kwa sasa ndo shida.
Mkuu uko sahihi, ila uchepukaji wa mwanaume katika maandiko, hamna Mahali ulitajwa kua na faida zaidi ya hasea , ndio Sababu wote waliishia kuungama tu na Kwa sababu hiyo, ikaamlika Kila mwanaume awe na mwanamke wake . ( ni ubishi wetu tu ndio unafanya hata Leo tunachepuka ).


Mwandishi Mmoja humu anasema "Mwanaume Tunza Manii yako".
 
Unahalalisha uchepukaji kwa wanawake.

Mchepukaji hakosi sababu ya kujitetea, mzinzi ni mzinzi tu hakuna upweke wala mwanaume hivi na vile.
Sihalalishi Uchepukaji, maana mwenyewe Nina Mke .

Lakini kwa uzoefu naoushudia mitaani , jambo hili limekolezwa zaidi na wanaume .

Embu fikiria, Wewe unatongoza mwanamke X, hivi unadhan Mkeo yeye atakwepa mishale ??.
 
Kuishi na mwanamke kwa akili( Kama jinsi tulivyoamrisha kwenye maandiko matakatifu) ndicho kitu muhimu kuliko vyote.

Kujaribu kumwelewa mwanamke Ni sawa sawa na kuupaka upepo rangi.
Naaam nakubali, Huwa sipingi maandiko.

Na hiyo akili ndio mwisho itaturejesha kwenye Uanaume ninaozungumzia.
 
Back
Top Bottom