Mpaka Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, uchumi wa Tanzania ulikuwa ni mkubwa kuliko wa Kenya. Marais waliomfuatia walikwama wapi?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Kuna shida mahali.

Pamoja na watu kumnanga (very incorrectly and unfairly) Mwalimu Nyerere (RIP mzee wetu) kuhusu sera zake za uchumi, inaonekana dhahiri kuwa alikuwa akifanya vizuri zaidi kiuchumi kwa kuchukulia nchi ya Kenya kama benchmark. Nimeichukulia Kenya kama benchmark kwa vile ndiye mshindani wetu mkubwa kiuchumi kwenye EAC na mara zote Tanzania tumekuwa tukifanya kila jitihada kutaka kuwa juu yake.

Mnyonge mnyongeni lakini...

Sasa ukiangalia graphic trend kwenye video clip hii hapa chini utagundua kuwa wakati mwalimu alipokuwa anaondoka madarakani, Tanzania ilikuwa always juu ya Kenya kiuchumi (GDP) miaka ya 80s hadi anaondoka ofisini 1985. I mean pamoja na changamoto nyingi sana zilizopelekea mdororo wa kiuchumi kwenye late 70s (kuvunjika kwa EAC, vita vya Kagera, nk), bado Tanzania ilibaki kuwa ni "economy giant" kwenye EAC.

Sasa embu angalia performance ya marais waliofuata (ukimuondoa mzee Ruksa) vs Kenya kuanzia 1996:

Mkapa:
1996 aliingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $6B
2005 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $2B
Alijitahidi kupunguza GDP gap, so tunaweza kumpongeza kwa hilo lakini alishindwa kufanya alichokifanya Mwalimu (yaani kuifanya TZ iwe economically superior to KE)!

JK:
2006 aiingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $8B
2015 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $17B
JK aliruhusu gap lipanuke zaidi, pamoja na kwamba alijitahidi ku boost per capita kwa kiwango kikubwa kuliko Mkapa ($480B vs Mkapa's $330B).

JPM:
by 2016 Kenya walikuwa wametuzidi GDP kwa $20B
by 2020 Kenya tayari wameshatuzidi GDP kwa $44B
JPM is the worst performer vs Kenya. Sijui itakuwaje tukimpa tena nchi October - tunaweza kujikuta Kenya wametuzidi kwa $100B!

Kazi kwenu Watanzania. October hiyo yaja!

 
Hii kama ina kigezo cha kuhesabu safari za viongozi kupishana angani wakitumbua fedha za walipa kodi wao, Kenya wanayo kila sababu ya kutushinda awamu hii.
 
Upo sahihi Kenya kwasasa wametuzidi ila sio kwa 44B ni kwa 37B.

Lakini JPM naona hakuna tofauti na JK cha kuangalia ambacho haujaangalia Je, GDP yetu imeshuka au imepanda?
Jibu ni imepanda.

Mfano tu 2010 kipindi cha JK ilikuwa 32B akaikuza hadi kufikia mwaka 2015 akaacha ya 47B..hivyo toka 2010 hadi 2015 iliyokua ilikuwa ni 15B.

JPM akaikuta ipo 47B lakini leo 2020 ni 62B. Amekuza ile ile 15 B aliyokuza Jk.

Ila naamini awamu ya pili miundombinu inayoendelea hadi kufikia 2024 tutawapumulia Kenya begani. Na tusikatae mfumo wa ujamaa bado tunapambana nao... Dunia ilipobadilika Kenya walibadilika nayo mapema na waka take advantage ya region maana Mtanzania mjamaa hawa wengine kutwa vita.

Utagundua aliyekua ni Kenya.
 
Na hii GDP ya tz imepikwa kwenye vile vyungu maalum vya kupikia data kule machakani(chato)
 
Mwalimu hakuacha uchumi wowote sema Mwalimu kaondoka wakati Moi na mwenyewe keshavuruga uchumi wa Kenya!

Kilichowasaidia Wakenya na ndio maana wakatupiga gap ni kwa sababu tayari uchumi wao ulikuwa kuwa kwenye private sector!

Sasa wakati sisi tuna-struggle kuondokana na uchumi hodhi ambao ulikuwa umeshavurugika kuanzia mwishoni mwa miaka ya 70, na hatimae kuuingiza kwenye private sector, Kenya tayari walishakuwa na misingi imara ya ya private sector.

Na ndio maana, hata wakati TZ inaingia kwenye soko huria, moja ya kampuni ambazo zilikuja kuwekeza sana TZ ni kutoka Kenya kwa sababu tayari walishakuwa na strong private sector!
 
Kwamba Ethiopia walikuwa na gdp kubwa kuliko Kenya? Really??
Ethiopia is massive and rich. Their problem was a prolonged wars.
Kenya assimilated most of the investors coming in this region because of their political approach to the economy.
Time is up now for others to catch up. Kenya is marred by corruption. The country is stinking corruption almost in every walk of life. Before we know , if they dont work to rectify the problems now, they will be operating in the world of shit
 
Upo sahihi Kenya kwasasa wametuzidi ila sio kwa 44B ni kwa 37B.

Lakini JPM naona hakuna tofauti na JK... cha kuangalia ambacho haujaangalia Je, GDP yetu imeshuka au imepanda?
Jibu ni imepanda.

Mfano tu 2010 kipindi cha JK ilikuwa 32B akaikuza hadi kufikia mwaka 2015 akaacha ya 47B..hivyo toka 2010 hadi 2015 iliyokua ilikuwa ni 15B.

JPM akaikuta ipo 47B lakini leo 2020 ni 62B. Amekuza ile ile 15 B aliyokuza Jk.

Ila naamini awamu ya pili miundombinu inayoendelea hadi kufikia 2024 tutawapumulia Kenya begani.

Utagundua aliyekua ni Kenya.
Kwa Tanzania uchumi wetu ulikuwa more stable kwenye Era ya Mkapa wakati Kenya bado ilikuwa kwa Moi ambaye nae hakuwa mzuri

Kikwete kaingia lakini hakuwa mzuri kwenye uchumi ukilinganisha na mkapa, kigezo kizuri tu ni control ya mfumuko wa bei na thamani ya shillingi dhidi ya dollar. Ukirudi kwa Kenya time hiyo ndio aliingia Kibaki nayo ikawa golden Era kwa Kenya

Kibaki kaacha msingi imara haswa kwenye miundombinu na demokrasia, fikiria tu mfumo wa kenya kwa sasa ambao serikali kuu imeachia uhusu serikali za chini kama mikoa kujiamulia baadhi ya mambo yake kama budget. Hiyo imechochea zaidi ukuaji wa Kenya

Sitegemei Uchumi ukue in figures kwenye Kipindi cha magufuli maana Sera zake za uchumi ni kama anarekebisha na si kuukuza na mbaya zaidi Private sector inapumulia mashine tu. So, Kenya kwa speed yao wapo vizuri though sisi bado tuna potential kubwa ya kukua kuliko wao
 
Ethiopia is massive and rich. Their problem was a prolonged wars.
Kenya assimilated most of the investors coming in this region because of their political approach to the economy.
Time is up now for others to catch up. Kenya is marred by corruption. The country is stinking corruption almost in every walk of life. Before we know , if they dont work to rectify the problems now, they will be operating in the world of shit
Ethiopia tatizo ni less resourceful ukilinganisha na nchi zingine ndio maana kwa sasa investment yao kubwa ni kwenye service industry ambayo ni muhimu pia...

Kenya itaendelea mbele zaidi sababu ya human resource na wanazidi kuinvest humo maana ndo point yao kubwa of Economic supremacy, Tanzania tukiweka nguvu hapa hatutoshikika
 
Azimio la Arusha ndilo lilisababisha wazungu na wahindi kibao walifunga virago Wakati Kenya wwaliwabakiza

Unachongea uongo uchumi uliharibika NYERERE AKIWA madaraka usisukumie maraisi wengine

Vita ya kagera pia ilichangia uchumi kufa

Nchi ilikuwa tupu Haina hata pesa za kigeni.Mwinyi alipokea uongozi kwa Nyerere nchi ikiwa hoi bin taabani kiuchumi

Mleta mada Kawadanganyeni wajnga wenzio
 
Uongo!

Tanzania haijawahi kuwa na Uchumi mkubwa klk Kenya, simple logic tu mpaka Nyerere anaondoka TZ yetu ilikuwa planned socialist economy wakati Kenya ni capiatalistic from day one, kwanza Uchumi wa Kenya ulikuwa mkubwa mara 2 ya Tanzania, bidhaa karibia zote zilikuwa made in Kenya, hivyo sasa hivi ndiyo pengo limepungua lkn si TZ wala Uganda zilizowahi kuwa na Uchumi mkubwa klk Kenya, ...
 
Back
Top Bottom