Mpaka msimu wa kuandaa mashamba unafika, pamba ya msimu uliopita bado haijanunuliwa!?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,996
20,644
Nimeshtushwa sana na suala hili!

Naangalia TBC sasa hivi,namuona Waziri Mkuu akiwa na wanunuzi wa pamba wanapanga jinsi ya kukopa ili wanunue pamba ya wakulima!

Hii hali ikoje? Kama mazao yanayoleta fedha za kigeni, korosho na pamba yamekwama,zao lipi litaziba gepu? Kwa nini wafanyabiashara hawakununua pamba? Je wana sababu za kibiashara, lakini serikali imewaambia wanunue kwa sababu za kisiasa?Nani anadhamini mikopo ya wafanyabiashara hao katika mabenki?

Mkulima atabaki kuwa mnyonge na masikini
 
Hahaha wakulima wajinga sana, wanadanganywa na maneno ya wanasiasa nao wanafanya wanayoambiwa, hiyo hazinduliwi sio kipaumbele, jiwe la msingi litawekwa wapi?! wangelima karanga sasa hivi wengekua wanakaanga na kula, sasa pamba hata wakitengeneza yale magodoro yetu itabaki haina maana.
Ingekuwa chuma ningewashauri wakipeleke kwenye ujenzi as SGR au meli zetu, lakini Pamba wasubiri kwanza. Tanzania ya viwanda hao wakulima wameula wa chuya.
 
Hii sijuhi itakuwaje kwa wakulima. Juzi nilikuwa natoka kwenye Maonyesho ya nanenane pale Simiyu (Nyakabindi), pembeni mwa barabara tuliyokuwa tunapita kulikuwa na Maghala ya Pamba ambayo imejaa mpaka juu, ila kwa nje hakuna hata mtu mmoja, Kwenye gari wakaanza kautani kao ka kisukuma kwamba atokee Mlevi mmoja na kutondosha kipisi cha Sigara je hasara itakuwa kwa nani? Kwa mkulima ama kwa walip na ghala ya pamba.
Kiukweli kuna kitu hapa kinabidi kifanyike kuokoa jahazi na naona kwa hili kama wakina Musiba wakipiga kelele huko zinaweza sikilizwa
 
ha ha ha,chinembe umestaafu kusifu na kuabudu?,
anyway hali ni mbaya,watu wanaogopa kuchukua hla bank halafu ghafla sera inageuka,watalipaje mikopo?,inabidi wahakikishiwe,hakuna mfanyabiashara atarisk mabilioni kwa uwekezaji usio na hakika,
 
Tunajenga kwanza V! Wonder kisha tutatatua shida za wananchi.
Kura watatupatia tu, watake wasitake.
 
ha ha ha,chinembe umestaafu kusifu na kuabudu?,
anyway hali ni mbaya,watu wanaogopa kuchukua hla bank halafu ghafla sera inageuka,watalipaje mikopo?,inabidi wahakikishiwe,hakuna mfanyabiashara atarisk mabilioni kwa uwekezaji usio na hakika,
Kweli kabisa, kama mtu hujatembelea huku huwezi hamini, ila hivi ndiyo halia halisi. Je hata hawa wakina MO hawawezi kununua?
 
Jamaa wa stakabadhi ghalani hawapo huko?
Serikali ya ccm inaxhojua ni kuzindua ujenzi kujenga nk lakini waambie mna mkakati gani wa kupunguza maskini kwa miaka mitano? Kila mwaka mtapunguza watu wangapi na kwa mbinu gani? Hapo hutawaona sasa kujenga hata layman asiyeenda shule anaweza
 
Acha uongo kwa Wasukuma kipindi hiki ni msimu wa ngoma ya chagulaga. Maandalizi ya mashamba ni mwezi wa oktoba.
 
Muda wa kuandaa mashamba mwezi huu wa 8 mkoa gani?? Kilimo cha mitandaoni hiki
 
ha ha ha,chinembe umestaafu kusifu na kuabudu?,
anyway hali ni mbaya,watu wanaogopa kuchukua hla bank halafu ghafla sera inageuka,watalipaje mikopo?,inabidi wahakikishiwe,hakuna mfanyabiashara atarisk mabilioni kwa uwekezaji usio na hakika,
Tehe! Tehe! Nimewaza tu kwamba,kama biashara ya pamba ingekuwa inalipa,wasingesubiri mpaka waziri mkuu awaambie wakope,wanunue pamba,ninahisi wafanyabiashara hawa wanakopa benki,hawaweki dhamana ya mali zao,bali mdhamini ni serikali kupitia benki kuu,kwa hiyo wafanyabiashara hawatajihisi kwamba wanawajibika kufanya biashara hiyo,bali watajiona wao ni mawakala tu
 
Tuendelee kutembea vifua mbele
Hii ya kuweka vifua mbele imesababisha matatizo ya uti wa mgongo,mwili unakosa balansi,kifua kisilazimishwe kukaa mbele,kikae mahali pake
 
Inasikitisha sana... mipango siyo matumizi...

Hizi zote ni juhudi za serikali ya awamu hii...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom