Mpaka Lini Tutaendelea Kujipendekeza huku hali za watu wetu ni kama hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka Lini Tutaendelea Kujipendekeza huku hali za watu wetu ni kama hizi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Falcon, Aug 4, 2012.

 1. Falcon

  Falcon JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefatilia mijadala mingi na kusoma magazeti pamoja na Blogs za watu mbali mbali hapa Tanzania ,nilichokigunduwa wengi tumekuwa tunawasamini watu kutokana na uwezo au hali waliyo nayo ikiwa ni ya kimazingira au kwa sifa walizo nazo ,Leo utajiuliza kwanini Tanganyika inajitwisha mzigo wa Zanzibar kwa hali yeyote ile wakati watu wake katika mikowa mingi waishi maisha ya kubahatisha? au unaweza kusema wanaishi maisha ya wanyama pori ,kinacho nishangaza zaidi hata wale ambao wametoka katika mikowa hiyo au makabila hayo huwasahau watu wao au makabila yao na badala yake utawaona wanapigia debe mambo ya Zanzibar na Tanganyika, nafikiri wakati umefika tuelekeze nguvu na kekele zetu katika kuwasaidia ndugu na makabila tunayotoka ili nawao waonje raha ya maisha tuwachane na fikra za kuji force na kujipendekeza tuwe pamoja na Zanzibari
  watoto wa mrima.JPG Wanafunzi wa shule ya msingi Etaro wakiwa darasani.Shule hii ipo wilaya ya Musoma vijijini.JPG
   
 2. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Mi sitaki kuingilia huko kwenye Uzanzibar na Utanganyika maana tunaweza kuuongelea muungano na bado tukawajali Wananchi wetu, naongelea hili la maisha ya ndugu zetu huko vijijini ukweli hali ni mbaya sana, nashukuru mleta mada umeweka na ushahidi kabisa maana haiwezekani wakati viongozi wetu wanaimba uchumi umeimarika na Wabunge kuimba sifa za serikali huko bungeni lakini hali ipo hivi, na hizi ni chache katika mikoa iliyo mingi ambayo wabunge wake wanatoka mapovu kuitetea serikali wanapoambiwa serikali haiwajibiki ipasavyo kwa wananchi wake.
  Swali langu kwa Wabunge na Serikali ni kwanini wananchi wa kawaida tuweze kuiona hii hali ila nyinyi hamuioni au mkienda huko majimboni kwenu munafumba macho musiuone ukweli wa maisha ya wapiga kura wenu?
   
 3. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mpaka CCM itakapotoka madarakani
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  serikali haina hela
   
 5. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nilitembelea shule yangu ya msingi niliyosomea, machozi yalinitoka!
  Mwaka uliopita wa fedha shule ilitengewa bajeti ya Tsh 45,000/= tu (elfu arobaini na tano).
  Hapo sijui ni makasha mangapi ya chaki au ni bao ngapi zitapigwa rangi, au ni paa gani litafanyiwa marekebisho liache kuvuja.
   
Loading...