Mpaka leo bado sijajua nafasi ya mbunge std 7 katika kutunga sheria

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wasomi,wanazuoni, wanaharakati na wadau wengine nisaidieni katika hili.

Bunge ni mhimili mkubwa sana nchini ambao kazi yake kuu ni kutunga sheria ili zitumiwe na jamii pamoja na watawala kuendesha taifa, Sheria hizi zikishatungwa na kupitishwa na bunge ndio mahakama hufanya kazi ya kuzitafasiri! Vyombo vingine vya dola huhakikisha sheria hizi zinafuatwa ipasavyo.

Swali: Je, mwandaaji wa sheria hizi awe darasa la Saba kweli? Hivi watanzania tinaliwaza hili kweli? Kuwapa std 7 kazi ya kutunga sheria halafu wakili au hakimu msomi akazitafsiri sio matusi haya jamani?

Only in Tz.
 
huwa wanajua kuwa ni ngumu wote watakuwa la 7,ikitokea mwaka fulani wote wakawa la 7 ndio watatia akili.

ila kiukweli wabunge atmost 100 tu wanatosha kufanya shughuli zote za bunge. N akama wabunge hao ni kariba ya Tundu Lissu basi wanahitajika atmost 30
 
Almost chama tawala ndo wanalea huu utaratibu, ni nadra sana kuona upinzani mbunge ni std 7! Labda kidogo form 4 ndo unaweza kusema wako wengi.Sijui ni nini haijulikani hapo kwa karne hii ya 21 eti tuende kwenye uchumi wa kati. Ndio maana ushabiki bungeni hauishi.
 
Kwani Sheria zinatungwa kutokana na madarasa au hekima na weledi wa mhusika?????
Zamani malaigwanani wa kimasai walikuwa hawajaenda shule lkn walikuwa na Sheria nzuri tuu zilizokuwa zinafuatwa na jamii husika.
Wewe bhana!unajua kuna sheria tafsiri zake husababisha mpaka kesi kuahirishwa kwa sababu ya ugumu wake? Std 7 atajulia wapi terminologies za kisheria? Inawezekana kabisa na wewe ni std7.
 
katiba ya wananchi iliondoa mbunge darasa la saba lakini katiba ya CCM imekubali hata asiyejua kusoma,kuandika na kuhesabu
 
Wasomi,wanazuoni, wanaharakati na wadau wengine nisaidieni katika hili.

Bunge ni muhimili mkubwa sana nchini ambao kazi yake kuu ni kutunga sheria ili zitumiwe na jamii pamoja na watawala kuendesha taifa, Sheria hizi zikishatungwa na kupitishwa na bunge ndio mahakama hufanya kazi ya kuzitafasiri! Vyombo vingine vya dola huhakikisha sheria hizi zinafuatwa ipasavyo.

Swali: Je, mwandaaji wa sheria hizi awe darasa la Saba kweli? Hivi watanzania tinaliwaza hili kweli? Kuwapa std 7 kazi ya kutunga sheria halafu wakili au hakimu msomi akazitafsiri sio matusi haya jamani?

Only in Tz.

Kwani ni mbunge yupi elimu yake ni ya darasa la saba?
 
wabunge hawatungi sheria wewe, miswada wanaletewa wanaijadili inapita. Wanaoondaa miswada ndio wanatunga, kwa hiyo hata darasa la VII wanaweza kuchangia
 
Wasomi,wanazuoni, wanaharakati na wadau wengine nisaidieni katika hili.

Bunge ni muhimili mkubwa sana nchini ambao kazi yake kuu ni kutunga sheria ili zitumiwe na jamii pamoja na watawala kuendesha taifa, Sheria hizi zikishatungwa na kupitishwa na bunge ndio mahakama hufanya kazi ya kuzitafasiri! Vyombo vingine vya dola huhakikisha sheria hizi zinafuatwa ipasavyo.

Swali: Je, mwandaaji wa sheria hizi awe darasa la Saba kweli? Hivi watanzania tinaliwaza hili kweli? Kuwapa std 7 kazi ya kutunga sheria halafu wakili au hakimu msomi akazitafsiri sio matusi haya jamani?

Only in Tz.
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi. Hivi itakuaje kama mbunge katokea jimbo ambalo hakuna aliyemaliza darasa la saba endapo mtaweka sheria ya kiwango cha elimu kwa mwakilishi? Kwanza nataka tuelewane hapa. Sheria ni kama mwongozo. Hivyo hata mtu hana darasa hata moja, anauwezo wa kutunga sheria kutokana na jamii inayomzunguka
 
katiba ya wananchi iliondoa mbunge darasa la saba lakini katiba ya CCM imekubali hata asiyejua kusoma,kuandika na kuhesabu
Ila nyie bwana. Yaani mnataka sheria itungwe na msomi alafu itumike na mjinga? Acheni mambo yenu bhana. Basi msilalamike kuona katiba imechujwa na wachache alafu itumike na taifa zima
 
karne hii hatutaki watu wa ndiooooooo
 
Kwani Sheria zinatungwa kutokana na madarasa au hekima na weledi wa mhusika?????
Zamani malaigwanani wa kimasai walikuwa hawajaenda shule lkn walikuwa na Sheria nzuri tuu zilizokuwa zinafuatwa na jamii husika.
Kibaya ni kwamba hata hao wabunge wasomi wa siku hizi wamekosa hekima na busara

Ila hata hivo kwa dunia ya sasa ni muhimu kuwa na wasomi
Mambo ya kiuchumi kwa dunia ya sasa yanahitaji yasimamiwe na sheria nzuri na makini huwezi fananisha mambo ya siasa za leo na utawala wa malaigwani.. Tofauti kabisa
 
Back
Top Bottom