Mpaka kufikia tarehe 22 january 2017 kwenye uchaguzi wa madiwani wengi watakuwa wamefukuzwa kazi.

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,266
2,000
Niwatakie nyote kheri ya mwaka mpya.Kumekuwa na mtindo wa kutengeza ajenda feki ili kubadili upepo wa mijadala kwenye taifa.Mfano ni ile ya machinga, ambayo wakuu wa wilaya wa Nyamagana na Ilemela waliwaamuru machinga waondoke tena kwa matangazo mbali mbali na taarifa za habari. Rais,waziri mkuu,mawaziri wahusika,mkuu wa mkoa na wabunge wote wakiwa kimya. "Eti walikuwa hawajui". Machinga wakaondolewa kwa hasara kubwa ya mali zao. Badaye kwa kuona kuwa wapinzani watawambia machinga wadai fidia,serikali ya CCM, ni wazi,wakamtuma mbunge wa tume ya uchaguzi(stanslaus mabula) aje na porojo ya kujifanya anawatetea machinga wapewe fidia. Fidia hiyo ni wazi hawajapewa na hawatapewa!Leo, yanatokea ya TANESCO kutuma maombi EWURA halafu waziri Sospeter Muongo anajifanya alikuwa hajui! Mpaka EWURA wamekubali kupandisha umeme ndipo anatokea na kudai ETI "anaipiga marufuku TANESCO kupandisha umeme!" Kwa nini hakuwambia waondoe hayo maombi EWURA?! Hatimae mkurugenzi Mramba amefukuzwa kazi. 22.1.2017 NI UCHAGUZI WA MARUDIO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom