“mpaka kifo kitutenganishe” – wanawake sasa wakataa kiapo hicho!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,436
127,460

Hivi sasa wanandoa wa Marekani hawako tayari tena kujiapiza kwamba, wataishi na mume hadi kifo kije kiwatengenishe. Badala yake, wengi hutaka kujiapiza kwa kusema, "tutaishi kwa shida na raha, uzima na maradhi, kama tu penzi litaendelea kuwepo."

Kwa sababu maandiko ya dini ya Kikristo kwa mfano, hayawezi kubadilishwa katika jambo kama hilo, wanandoa wengi wameamua kutofunga ndoa zao kanisani na badala yake hufungia mahali pengine.
Hii ni ili kukwepa kutamka kwamba, wataishi hadi kifo kiwatenge, wakati wanaona kabisa watu wengi wamechanganyikiwa na hawajui tena maana ya kupenda.

Kila bibi harusi anaogopa kujiapiza kwa kauli hizo zenye kumfunga. Inaelezwa kwamba, woga huo unatokana na kile kinachoonekana majumbani, kwamba, ndoa nyingi hazina kuaminiana na zinatisha kwa visa na mikasa. Inaelezwa na watu wanaopenda kuyachukulia mambo kimkabala na mila na desturi kwamba, utaratibu huu mpya wa kukwepa kusema, "hadi kifo kitutenge," wakati wakufunga ndoa na badala yake kusema kitu kama, "naahidi kuwa mwaminifu kwako, kama tu penzi bado lipo," huenda utadhoofisha ndoa nyingi.
Raisi wa Muungano wa Makanisa Katoliki na haki za binadamu, William Donahue, amesema, kubadili kiapo hicho na kusema, "kama tu penzi litaendelea kuwepo," ni sawa na kuweka masharti kupenda, jambo ambalo litafanya kupenda kupoteze maana yake ya asili. Amesema kupenda hakuwezi kuwekewa masharti. Kiongozi wa utafiti huu Mary Jo Gallegos amesema, kwa hivi sasa ambapo watu wa mila na imani mbalimbali wanakutana na kuoana, mambo ya kuambiana hadi kifo kitutenge, hayawezi kuwa na nguvu.Mama huyo ameendelea kusema, hakumbuki kwa mara ya mwisho ni lini alimsikia mwanamke mwenye kufunga ndoa, akiahidi kwamba, atampenda mumewe hadi kifo kije kiwatenge.

Anazidi kusema, hakuna jambo kama hilo kwa sababu, wengi wamegundua kwamba, huko ni kujitwisha mzigo ambao mtu hawezi kuubeba.
Amezidi kusema kwamba, watu wengi sasa wanaiona hali halisi na wanajua ukweli mkubwa zaidi katika ndoa. Amesema wale walio kwenye ndoa ya pili au ya tatu, wanajua ukweli mkubwa zaidi kuliko wale walio kwenye ndoa ya kwanza au ambao hawajaingia kwenye ndoa kabisa. Jambo la maana anasema, ni kwa wanandoa wote kuamini kwamba, wataishi kwa amani hadi kufa, lakini wakijua lolote linaweza
kutokea.

Huko Marekani, nusu ya ndoa huishia kwenye talaka.
Hata hivyo kiwango hicho kimeshuka, baada ya wengi kuamua kuwekana kinyumba au kuwa vimada badala ya kufunga ndoa. Hivi sasa wapenzi huishi pamoja kwa miaka mitatu au zaidi kabla hawajaamua kama wafunge ndoa au hapana. Kila mmoja anamwogopa mwenzake, haamini kwamba, anampenda.Sharon Naylor, ambaye ni mtunzi wa kitabu cha Your Special Wedding Vows (Kiapo Maalum kwa Ndoa Yako) anasema amewahi kusikia bibi harusi akiapa siku ya ndoa yake kwa kusema, "hadi pale muda wetu wa kuwa pamoja utakapoisha."

Anasema kiapo kama hiki ni sahihi kwani kuapa kwa kitu ambacho huna uhakika wa kukiweza au ambacho unajua siyo kweli, ni kujitendea haki.
Mabadiliko haya katika kuapa siku ya ndoa yanaashiria kwamba, taasisi inayoitwa ndoa inaendelea kupambana na mabadiliko ambayo hatimaye yataiporomosha na watu wataanza kuishi kama wanyama wengine. Inaelezwa pia kwamba, huenda ni kutokana na ubabe wa wanaume ambao umewabadili wanawake na sasa wameanza kuitazama ndoa kama kifungo.
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,771
23,038
ndiooooo......
Wanawake hawataki.....emagine mmeoana lakini kutwa kuletewa watoto wadogo kuliko umri wa ndoa yako.....daily kupigiwa simu na mahawara kutukanwa, au ndo kila leo kufumania......au mwanaume majukumu hagusi.........kipigo......akuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Zion Daughter

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
8,922
4,218

Hivi sasa wanandoa wa Marekani hawako tayari tena kujiapiza kwamba, wataishi na mume hadi kifo kije kiwatengenishe. Badala yake, wengi hutaka kujiapiza kwa kusema, “tutaishi kwa shida na raha, uzima na maradhi, kama tu penzi litaendelea kuwepo.”

Kwa sababu maandiko ya dini ya Kikristo kwa mfano, hayawezi kubadilishwa katika jambo kama hilo, wanandoa wengi wameamua kutofunga ndoa zao kanisani na badala yake hufungia mahali pengine.
Hii ni ili kukwepa kutamka kwamba, wataishi hadi kifo kiwatenge, wakati wanaona kabisa watu wengi wamechanganyikiwa na hawajui tena maana ya kupenda.Anazidi kusema, hakuna jambo kama hilo kwa sababu, wengi wamegundua kwamba, huko ni kujitwisha mzigo ambao mtu hawezi kuubeba.
Amezidi kusema kwamba, watu wengi sasa wanaiona hali halisi na wanajua ukweli mkubwa zaidi katika ndoa. Amesema wale walio kwenye ndoa ya pili au ya tatu, wanajua ukweli mkubwa zaidi kuliko wale walio kwenye ndoa ya kwanza au ambao hawajaingia kwenye ndoa kabisa. Jambo la maana anasema, ni kwa wanandoa wote kuamini kwamba, wataishi kwa amani hadi kufa, lakini wakijua lolote linaweza
kutokea.

Huko Marekani, nusu ya ndoa huishia kwenye talaka.
Hata hivyo kiwango hicho kimeshuka, baada ya wengi kuamua kuwekana kinyumba au kuwa vimada badala ya kufunga ndoa. Hivi sasa wapenzi huishi pamoja kwa miaka mitatu au zaidi kabla hawajaamua kama wafunge ndoa au hapana. Kila mmoja anamwogopa mwenzake, haamini kwamba, anampenda.Sharon Naylor, ambaye ni mtunzi wa kitabu cha Your Special Wedding Vows (Kiapo Maalum kwa Ndoa Yako) anasema amewahi kusikia bibi harusi akiapa siku ya ndoa yake kwa kusema, “hadi pale muda wetu wa kuwa pamoja utakapoisha.”

Anasema kiapo kama hiki ni sahihi kwani kuapa kwa kitu ambacho huna uhakika wa kukiweza au ambacho unajua siyo kweli, ni kujitendea haki.
Mabadiliko haya katika kuapa siku ya ndoa yanaashiria kwamba, taasisi inayoitwa ndoa inaendelea kupambana na mabadiliko ambayo hatimaye yataiporomosha na watu wataanza kuishi kama wanyama wengine. Inaelezwa pia kwamba, huenda ni kutokana na ubabe wa wanaume ambao umewabadili wanawake na sasa wameanza kuitazama ndoa kama kifungo.
Whats your take?????

Binafsi naona sikubaliani nao...Lazima ifike mahali watu waoane kwa kupendana na sio kwa faida fulani fulani..Kipimo kikuu cha upendo mara nyingi ni katika shida...sasa ukimkimbia mwenzi katika shida iwe maradhi au alosto hapo ndo itakuwa nini? Kuna nani asiyepata shida hapa duniani? utaachana na wangapi?
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,436
127,460
Mimi ni Mchagga wa Lyamungo Sinde Machame.
Watu wamekuwa wakitujaji vibaya, kama wapo wapendao pesa kuliko utu mimi siko hivyo kabisa.
Mimi nataka mwanamume ambaye nitaishi nae maisha ya taabu na raha, kwenye hali zote, uzima na kifo hadi hapo kifo kitakapo tutenganisha.
kwa kweli siungi mkono hoja ya viapo hivyo vipya kutoka kwa shetani

Umesema kweli.wanawake wa machame wanaogopeka sana kwa kuua waume zao
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,047
6,508
Eh! huo ndo usawa! Yatazuka mengi kabla ya Kristo kurudi. Kwa kuwa niko kwenye ndoa litakalojitokeza nitalipokea tu; ila kiapo tayari nilishamaliza.
 
MadameX

JF-Expert Member
Dec 27, 2009
7,802
3,840
Love conquers all, siku ambayo mapenzi yatapoteza hicho kiapo hakipo tena. Kwahiyo sitaki kuapizwa......
 
HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
912
859
Kusema kweli huo msemo hauko realistic. Ndio kuna shida na raha ambazo zinatokea kwenye safari ya maisha, lakini kama shida na mateso hutoka kwa mwenzako ya nini kuvumilia? Kupigwa, kutukanwa, kuletewa nyumba ndogo n.k Nadhani mungu ataelewa ukiamua kuachana na mtu wa namna hiyo uvumilivu ukikushinda. Ya nini kusubiri kuuawa?

Pamoja na hayo inawezekana mwenzako akaanza kuwafanyia watoto, ndugu, na hata majirani uovu. Sometimes it is for the best to go your separate ways usije ukaletewa kesi.
Hivi sasa wanandoa wa Marekani hawako tayari tena kujiapiza kwamba, wataishi na mume hadi kifo kije kiwatengenishe. Badala yake, wengi hutaka kujiapiza kwa kusema, "tutaishi kwa shida na raha, uzima na maradhi, kama tu penzi litaendelea kuwepo."

Kwa sababu maandiko ya dini ya Kikristo kwa mfano, hayawezi kubadilishwa katika jambo kama hilo, wanandoa wengi wameamua kutofunga ndoa zao kanisani na badala yake hufungia mahali pengine.
Hii ni ili kukwepa kutamka kwamba, wataishi hadi kifo kiwatenge, wakati wanaona kabisa watu wengi wamechanganyikiwa na hawajui tena maana ya kupenda.

Kila bibi harusi anaogopa kujiapiza kwa kauli hizo zenye kumfunga. Inaelezwa kwamba, woga huo unatokana na kile kinachoonekana majumbani, kwamba, ndoa nyingi hazina kuaminiana na zinatisha kwa visa na mikasa. Inaelezwa na watu wanaopenda kuyachukulia mambo kimkabala na mila na desturi kwamba, utaratibu huu mpya wa kukwepa kusema, "hadi kifo kitutenge," wakati wakufunga ndoa na badala yake kusema kitu kama, "naahidi kuwa mwaminifu kwako, kama tu penzi bado lipo," huenda utadhoofisha ndoa nyingi.
Raisi wa Muungano wa Makanisa Katoliki na haki za binadamu, William Donahue, amesema, kubadili kiapo hicho na kusema, "kama tu penzi litaendelea kuwepo," ni sawa na kuweka masharti kupenda, jambo ambalo litafanya kupenda kupoteze maana yake ya asili. Amesema kupenda hakuwezi kuwekewa masharti. Kiongozi wa utafiti huu Mary Jo Gallegos amesema, kwa hivi sasa ambapo watu wa mila na imani mbalimbali wanakutana na kuoana, mambo ya kuambiana hadi kifo kitutenge, hayawezi kuwa na nguvu.Mama huyo ameendelea kusema, hakumbuki kwa mara ya mwisho ni lini alimsikia mwanamke mwenye kufunga ndoa, akiahidi kwamba, atampenda mumewe hadi kifo kije kiwatenge.

Anazidi kusema, hakuna jambo kama hilo kwa sababu, wengi wamegundua kwamba, huko ni kujitwisha mzigo ambao mtu hawezi kuubeba.
Amezidi kusema kwamba, watu wengi sasa wanaiona hali halisi na wanajua ukweli mkubwa zaidi katika ndoa. Amesema wale walio kwenye ndoa ya pili au ya tatu, wanajua ukweli mkubwa zaidi kuliko wale walio kwenye ndoa ya kwanza au ambao hawajaingia kwenye ndoa kabisa. Jambo la maana anasema, ni kwa wanandoa wote kuamini kwamba, wataishi kwa amani hadi kufa, lakini wakijua lolote linaweza
kutokea.

Huko Marekani, nusu ya ndoa huishia kwenye talaka.
Hata hivyo kiwango hicho kimeshuka, baada ya wengi kuamua kuwekana kinyumba au kuwa vimada badala ya kufunga ndoa. Hivi sasa wapenzi huishi pamoja kwa miaka mitatu au zaidi kabla hawajaamua kama wafunge ndoa au hapana. Kila mmoja anamwogopa mwenzake, haamini kwamba, anampenda.Sharon Naylor, ambaye ni mtunzi wa kitabu cha Your Special Wedding Vows (Kiapo Maalum kwa Ndoa Yako) anasema amewahi kusikia bibi harusi akiapa siku ya ndoa yake kwa kusema, "hadi pale muda wetu wa kuwa pamoja utakapoisha."

Anasema kiapo kama hiki ni sahihi kwani kuapa kwa kitu ambacho huna uhakika wa kukiweza au ambacho unajua siyo kweli, ni kujitendea haki.
Mabadiliko haya katika kuapa siku ya ndoa yanaashiria kwamba, taasisi inayoitwa ndoa inaendelea kupambana na mabadiliko ambayo hatimaye yataiporomosha na watu wataanza kuishi kama wanyama wengine. Inaelezwa pia kwamba, huenda ni kutokana na ubabe wa wanaume ambao umewabadili wanawake na sasa wameanza kuitazama ndoa kama kifungo.
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,601
1,677
Umesema kweli.wanawake wa machame wanaogopeka sana kwa kuua waume zao

:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky: hahahaaaaa wanafanya hivyo ili neno litimie "MPAKA KIFO KITAKAPO TUTENGANISHA" halafu wanakuwa huru sasa:becky::becky::madgrin::becky::becky::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::becky::becky::becky:
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,436
127,460
Nini maana ya kuvumilia?
Unavumilia shida au unavumilia raha?
Au ndio yale mambo ya kupeana pole kwa starehe?
Kusema kweli huo msemo hauko realistic. Ndio kuna shida na raha ambazo zinatokea kwenye safari ya maisha, lakini kama shida na mateso hutoka kwa mwenzako ya nini kuvumilia? Kupigwa, kutukanwa, kuletewa nyumba ndogo n.k Nadhani mungu ataelewa ukiamua kuachana na mtu wa namna hiyo uvumilivu ukikushinda. Ya nini kusubiri kuuawa?

Pamoja na hayo inawezekana mwenzako akaanza kuwafanyia watoto, ndugu, na hata majirani uovu. Sometimes it is for the best to go your separate ways usije ukaletewa kesi.
 
HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
912
859
Kila mtu ana definition yake ya kuvumilia. Mimi naona ni kuvumilia yale unayoweza kuvumilia mradi maisha yako hayapo hatarini. Kuna wengine wanaweza kuvumilia vimada, watoto wa nje na vipigo. Haya yote yaweza kukuletea maradhi ya presha, ukimwi, au majeraha/kifo kutokana na vipigo.

Matatizo yanayokuja na outside forces, kwa mfano, ugonjwa, ajali, upungufu wa fedha (kuibiwa, uchumi, au kutoweza kufanya kazi) yanatakiwa yavumiliwe. Matatizo yote mnayaface kama familia.

Naweza kutoa list ndeeefu hapa, kwa kifupi kama wote mpo committed kuwa na ndoa yenye furaha mtaweza kusuluhisha mambo yenu. Ila kama ni mtu mmoja tu ambae anataka ndoa idumu wakati mwingine keshakanyaga nje na hana time na wewe, sioni sababu ya kung'ang'ania.Nini maana ya kuvumilia?
Unavumilia shida au unavumilia raha?
Au ndio yale mambo ya kupeana pole kwa starehe?
 
UKI

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
692
170
binafsi hata nakubaliana na hao wadada sio siri sina jinsi kwa sababu wazazi wamekulia kwenye dini harusi yangu itafanyikia huko ila ningekuwa niko kwenye hiyo nchi ni full raha masuala ya kusema tutavumiliana mpka kifo kitutenganishe mimi sikubaliani kabisa tupendane tukichokana tutaachana kama tulivyokutana maisha yanaendelea na kila mtu yupo free tunabaki kama mafriend masuala ya kuzeeshana mapema na stress siyataki kabisa haya maana wanawake ni mizigo jamani maisha ya girlfriend yananitesa hivi ya ndoa je?? dah
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom