Mpaka Kieleweke Si Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka Kieleweke Si Mbowe

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Asha Abdala, Jul 10, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kuwa kauli mbiu ya hamasa ya Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke ilibuniwa na Mwenyekiti Mbowe wakati wa kampeni, nataka kukanusha hapa kwamba mtu anayejiita Mpaka Kieleweke hapa Si Mbowe. Pamekuwa na jitahida sana za kumhusisha mwenyekiti wetu na Majina mawili hapa mtandanaoni, wakati Chinga alianzisha uzushi kwamba Mbowe ni Philimom Michael, Bwana FMES yeye ameanzisha Mpaka Kieleweke ni Mbowe. Nimekuwa nikifuatilia mienendo na michango ya watu hawa wawili na napenda niweke wazi kwamba hakuna Mbowe kati ya watu hao wawili.

  Philemon Michaeil ni mwanahabari ambaye mpaka sasa yuko Dar es salaam.

  Mpaka Kieleweke ni kada wa CHADEMA anayezunguka kati ya Dar es salaam na Dodoma.

  Hata wakati ambapo mwenyekiti Mbowe akiwa nje ya nchi hawa mabwana wawili wameendelea kutoa michango yao kutoka Dar es salaam. Mathalani kwa sasa Mwenyekiti Mbowe yuko kikazi mashariki ya kati lakini bado mpaka kieleweke anaandikia michango yako toka Dodoma.

  Kwa mchambuzi yoyote wa michango ya watu humu atagundua kuwa michango ya Mpaka Kieleweke haiendani kabisa na maoni na misimamo ya Bwana Mbowe katika masuala mbalimbali na kwa ujumla bwana Philemon Michael hana undani wa masuala ya kisiasa hususani yale yanayoihusu CHADEMA.

  Nawakatia kheri

  Asha
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  nani anayetaka kujua nani ni nani? Huu mtindo wa kujaribu kufuatilia hoja baada ya kujua msemaji ni nani unapoteza sana ladha ya hoja. Maana unasoma hoja huku ukiwa na preconceived ideas na prejudice tayari.. kumbe unayemfikiria ndiye kumbe siye!
   
 3. kkiwango

  kkiwango Senior Member

  #3
  Jul 10, 2008
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sasa tunaanza kupekuana wenyewe kwa wenyewe, tutafika kweli? tusaidiane tu katika kutokomeza ufisadi, then baada ya siku tutajuana na kupongezana. Mbowe, Mwinyi Makamba, Cheyo, Mtikila karibuni tu! ili mradi mfuate sheria za JF.
   
 4. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli bwana! Walizidi hawa kila siku mpaka kieleweke ndio Mbowe, mpaka kieleweke ni Mbowe mpaka watu wataelewa kuwa ni ukweli. Naona haja Jmushi nae amedakia huu uzushi na sasa ameanza kutazama mtu badala ya hoja.

  Mod, mko wapi mkemee hii hali?

  Asha
   
 5. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bi asha nae!!!!!!
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Sijatazama mtu badala ya chochocte!

  Ngoja nikuulize..Jmushi sema or to be more specific lets say anatumia jina lake hajaficha.Hilo ni chaguo lake kama wengine kina Zitto nk.

  Na pia kuna uhuru wa kuficha ama kutumia jina lako.

  Ila kuna mijadala mingine ama arguments inabidi kweli Mods waingilie ili kuwe na uwiano wa haki.

  Nitakupa mifano miwili..

  1)Mjadala wa MKJJ kuhusu wachagga ulionyesha wazi kuwa kuna watu wako radhi kusema chochote kwasababu majina yao ni feki na hivyo huwezi kujuwa kabila lao.

  2)Kama siku mimi kama Jmushi nilipotukanwa na Jasusi...Je kama na mimi Jmushi ningemtukana Jasusi ingemake sense?

  Jibu hapa ni BIG NO kwasababu kama jasusi ana mfahamu jmushi basi matusi yake yatakuwa yanamake sense lakini kama Jmushi hamfahamu jasusi then kurudisha matusi kwa mtu anayejiita "Jasusi" Ni upungufu wa akili!

  Najuwa wengi wenu mnafahamiana hapa jf!

  Na hivyo mara nyingi mnaangalia mchango base on that!

  Mimi hapa naenda na maandishi!

  Na hivyo basi kama mjadala ukibaki kuwa mjadala na tukakubaliana na kutokubaliana bila kwenda mbali zaidi ya hapo..Basi hakuna haja ya mtu kumjuwa mtu!
   
 7. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Good point MMJJ. If Mpaka Kieleweke is Mbowe or not what is the point Asha? Why treat Mbowe so godly? Can't Mpaka Kieleweke or Mbowe, if necessary, be answarable to their postings??
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Hii ina maana hata huyo mtumishi wao anayeitwa mpaka kieleweke wamemshusha sana.
  Sasa kwani michango yake ni mibaya kiasi cha kudai si Mbowe?
  Ama na yeye hapiganii maslahi ya chama kama mwenyekiti afanyavyo?
  Na kwanini thread hii asingeianzisha kieleweke mwenyewe?
  Ama kielewe naye licha ya kutokuwa Mbowe bado ana wawakilishi wa kumsemea ndani ya chama?
  Basi yeye kama si Mbowe lazima atakuwa mtu kubwa!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Jamani, kuna principle moja hapa ambayo hatuna budi kuiheshimu sana. Kama mtu anataka kutumia jina lake yuko huru kufanya hivyo na hawezi kulazimishwa vinginevyo na mtu yeyote. Kama mtu hataki kutumia jina lake hata akutukane vipi hilo ni lwake na wewe ukitaka kumtukana umtukane kwa jina alilokutukania (na wote wawili suffer the consequences of your actions).

  Kama wewe umetangaza jina lako na watu wanakutukana kukujibu kwa jina hilo huo ni uchaguzi wako. Kama humjui mtu unayejibizana naye na hauna jinsi ya kujua yeye ni nani, usianze kumbambikizia majina ya watu wengine kwa kufanya hivyo unaweza kuharibu sifa za watu wengine kwa sababu ya wewe kujaribu kuscore point.

  Kama hutaki kuitwa kwa jina lako na inakusumbua kwa sababu watu wanakujua, the choice is very simple!...

  lakini haya ya kupachika watu majina yasiyokuwa ya kwao ili uonekane unawajua siyo tu ni makosa ya hapa lakini ni kinyume na vipengele vyote vya uungwana kwani unaweka jina, hadhi, sifa ya mtu yeyote matatani.

  Binafsi labda naweza kudai nawajua wengi hapa kwa majina yao halisi na nafasi zao wale hata ambao hawajui kuwa nawajua. Hata siku moja sijaashiria kuwa nawajua, au ninapojibizana nao kuwataja hata kama tuko kwenye msimamo tofauti au wananirushia madongo (wakiamini siwajui). Kwanini? naheshimu chaguo lao la kuwa anonymous na ninalilinda to the penalty of relevant judicial sanctions.

  Vinginevyo, kama unamjua mtu fulani ni fulani hapa JF kaa nayo wewe mwenyewe!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Asha unasema eti mimi nimeanzisha kuwa Mpaka Kieleweke ni Mbowe? Vipi ukitoa ushaidi mkuu ili nikubali kukosolewa,

  Ninasubiri ushahidi wa mimi FMES, kuanzisha kuwa Mpaka Kieleweke ni Mbowe, ukiuonyesha mkuu nitakubali kosa, ila kama huna ushahidi naomba useme wazi kuwa huna na ningewaomba Mods wakushughulikie kwenye hili iwapo huna ushahidi na ukiwa nao naomba Mods pia wanishughulikie ipasavyo, maana si unajua mimi ni jina moja hapa na siku zote huwa niko responsible na kila ninalosema, sijawahi kukimbia kivuli changu au maneno yangu!

  Otherwise, sisi wote hapa ni watu wazima kama Mpaka Kieleweke sio Mbowe, hivi ni kweli wewe Asha ndiye uliyepaswa kumuongelea? Yaani yule mtu mzima hawezi kusema mwenyewe? Halafu mbona ni wengi hapa JF waliowahi kusingiziwa majina na mimi nikiwa mmoja wapo mbona hukujitokeza kutetea, WHy huyu Mpaka Kieleweke?

  Mkuu hivi kweli nia na madhumuni yako on this topic hasa ilikuwa ni nini, kutuambia au kutotuambia? Maana mkuu sio siri kuwa nimeshitushwa mpaka kwenye mifupa knowing aliyeko nyuma ya hili jina la Asha, lakini nasubiri ushahidi mkuu! Ili baadaye nikuonyeshe jinsi Chinga alivyoitwa godoro la muungwana, jinsi Chinga alivyoitwa kifaa cha muungwana, aliponitumia huu ujumbe niliwamuambia kuwa mezea tu kuna siku yatageuka haya!
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Naona mnazunguruka tuuu!

  Lakini highlights zimesha highlight ni kwanini mmeanzisha thread hii!

  Unataka kuimply nini?

  Eti kujidai nawajuwa!

  Kumjuwa nani...?

  MBOWE?

  We unafikiri mi mtu wa kujipendekeza?

  Kama ni kujipendekeza ningejipendekeza kwa baba yangu mzazi ambaye hata Mbowe anamfahamu!

  Sina haja ya kujipendekeza na kama kuna mtu anatowa kauli zenye kufanana na watu flani flani basi watahusishwa tu!

  Kudai kwamba kuna mtu anajaribu ku score point nayo ni PUMBA TU!

  Na pia ujuwe kuwa huna haja ya kuusema MSIMAMO WAKO KWANI TAYARI UNAJULUKANA NA ULISAPOTI KUTUKANWA KWANGU LICHA YA KWAMBA HUKUPENDA HATA KUSAMEHEWA KWANGU MARA BAADA YA WEWE KU COMPLIN KUWA NIFUNGIWE KWA KUMUITA KIKWETE MAFIA!
  SASA WEWE UPANDE UPI?
  WA KIKWETE AMA MBOWE?
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jul 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  yaani wewe baba yako hadi mbowe anamfahamu.. duh! tuna watoto wa wakubwa humu!
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu wangu maneno yako ni mazuri sana tena mazito, ila yamekuja very late kwa sababu the damage has been done kwa watu wengi sana hapa JF na hii tabia, ambayo imekuwepo hapa kwa muda mrefu sana,

  Nashangaa leo kwa mara ya kwanza umekuuma sana vipi kwani mkuu? Hivi unajua kuna watu mapka waliacha kuingia hapa kwa kutajwa majina yao? Mbona kwenye kusema jina la Chinga na kazi yake Foreign wakati fulani hapa kuna hata watu wanaoheshimika hapa walishiriki na hukulalamika? Why leo mkuu?

  Unajua ninahisi kuwa leo hapa JF kuna jambo, lakini binafsi nimeshitushwa sana na haya ya leo! Msimamo wangu mkuu siku zote uko wazi tena very clear, kuwa anayeanza ni lazima nimjibu na huwa ninatoa tahadhari mapema, kuwa kama huna hoja acha maana ukianza matusi ya nguoni kwa huwa sina tatizo kujibu, kwa sababu baaada ya kulazimishwa sana kuhusu my ID, nikajifunza dawa ni moja tu nayo ni kutafuta ID za wale wanaonichokoza na believe me ninazo, kwenye hilo I have no respect,

  kama ni sheria iheshimiwe kwa wote sio akisemwa jina Chinga ni sawa ila akisemwa Kileweke basi iwe tatizo
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  FMES,
  Wazungu wanasema better late than never. Labda sasa umuhimu wa kutotajwa majina umeonekana zaidi ya ilivyokuwa hapo awali. Au?
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikuulize swali moja MKJJ...
  Wewe ulikuwa hautaki mimi nizungumzie habari za Anna Muganda Ballali eti kwasababu kuna ndugu zake hapa kina "JASUSI"
  Sasa na mimi nikitake serious na kusema Hili jasusi ni kama jasusi lile lile Tanzania NZIMA ilipokuwa ikilitafuta ni makosa?
  Kwasababu si ni fake name?
  Jasusi..Jasusi...Eeerrr OK lets say JASUSI NI BALALI!
  WEWE UTABISHA KWASABABU UNAMFAHAMU!
  Mimi simfahamu...Ila nitampima na kummemorize based on mchango wake hapa na si vinginevyo!
  Tukibaki kwenye hoja mikwaruzano kama hii itakwisha.
  Ahsante.
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Wewe Hadi Mbowe anakufahamu?
  Basi wewe si mtoto wa MKUBWA...WEWE NI MKUBWA!
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mushi1,'
  Jasusi ni mimi, na si mwingine. Ila imeshabainika kuwa nina undugu na marehemu Ballali, hilo siwezi kulikwepa. Lakini bottom line ni kwamba tupo hapa kukata issues. Period. Tuachane na personalities, ingawa mara moja moja haziwezi kuepukikwa.
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  MKJJ AMA WEWE NI MBOWE?
  Maana jamaa toka aache kuchangia hapa wewe umetake over!
  Lakini typing yako si necessarily similar to maongezi yako RADIONI.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Mimi I am ready for whatever.
  Niko hapa kwa maslahi ya Taifa na si vinginevyo!
  Mimi ni mtu mwenye PRINCIPLE!
  Ni MTU HURU NA MIMI MWENYEWE NDIYE WA KUHOLD RESPONSIBLE KWA MCHANGO WANGU HAPA!
  Kule kwenye THREAD YA KICHOCHEZI YA MKJJ YA WACHAGGA..ALIRUHUSU MAKABILA YOTE TANZANIA KUMTUKANA MCHAGGA MIMI BILA YA MIMI KUJUWA MAKABILA YAO!
  Hili kidogo liniingize kwenye mtego mbaya!
  Lakini kama kawa..Nili handle situation.
  Sasa ngoja niseme something...MKJJ alisema...Kama unajuwa hili...Na mwenzako anajuwa lile!
  SO I AM READY.
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Jasusi,

  Heshima mbele, unajua mkuu mimi huwa sipendi unafiki hapa JF, kama mkuki unauma kwa nguruwe basi pia uume kwa bina-adam pia, sisi wote hapa ni watu wazima hakuna mtoto mdogo hapa, hivi karibuni nimeona mambo mengi yakifanyika hapa yanayoashiria baadhi yetu kuona sisi wengine ni either watoto wadogo au ni wajinga, ninasema hivi tuheshimiane na wote tuheshimu sheria,

  Siku Chinga alipotajwa hapa alinililalamikia sana kwenye PM, na ninaweza hata ku-produce zile PM za malalamiko yake ya kutajwa jina na kazi yake tena na watu wanaoheshimika sana hapa JF, sasa nashangaa sana leo kuona kumekuwa na tatizo kutajwa member mwingine what is it yaani member wengine ni bora kuliko wengine? au?

  Lakini ninakubali maneno yako kuwa better late than never, ni sawa 100%!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...