Mpaka Jana saa tano usiku CCM waliendelea na vikao vya kuwahakiki wapiga kura wao

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,502
2,046
Hii ni katika maeneo machache niliyofanikiwa kupitapita katika viunga vya jiji la DAR hasa kwenye ofisi nyingi za ccm, tofauti kabisa na hali kwenye Ofisi za Wapinzani ambako zilikua zimefungwa makufuli.

Pamoja na kutuhumiwa na wapinzani kwa kucheza rafu kwenye chaguzi mbalimbali, utamaduni huu wa ccm unawasaidia Sana kuhamasisha na kulidhibiti kundi la wapiga kura wenye upeo wa kawaida wale ambao kwao kupiga kura ni kile kitendo Cha kupiga tiki kwanye shahada ya kupigia kura.

Mimi Kama mwananchi wa kawaida naliona hili, je ni kwa nini viongozi wa upinzani hawalitafutii dawa!?
 
Back
Top Bottom