Mpaka hapa nashindwa Elewa Wajapan sijui waliwaza nini kwenye hizi gari

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,357
11,503
Speed meter/Odometer inakuwa katikati kwenye dashboard. Ili iweje sasa? Mambo mengine ya hovyo tu mi naona.

Kuna gari za Japan nmeona zina hiyo kitu. Leo nlikuwa na jamaa yangu kaomba nimsaidie kumfikisha Dodoma kwa gari yake sababu nami nlikuwa naelekea huko. Nikamwambia hamna shida kwa kuwa mimi sitopata usumbufu wa Traffic njiani

Nmeshika usukani gari lake Toyota Rumion speed meter/odometer ni kama matangazo kila mtu anaona.

Nakanyanga ikifika 160 kms/hr jamaa akiangalia pale kwenye meter anakalia tako moja anashikilia kiti huku amekodoa macho. Mwoga.anasema amewahi kimbiza sana gari akafikisha speed 100 kms/hr.

Kiukweli imenifanya nikose amani sababu kwa watu waoga wanasumbua sana. Ni bora niwe najionea mwenyewe abiria asijue.

Tulifika salama na jamaa ameshukuru. Ila wajapan waache kuwaambia watoto wao kutengeneza magari. Wawe serious. Hi designing nyingine sielewi walifikiria nini.
 
Sasa mimi siyo dereva wako. Umeomba nikusaidie ku drive sababu huna uzoefu. Otherwise endesha na mwendo wako wa kinyonga. Hiyo gari ya 120km/hr unamshusha dereva ni gari gani? Mbona huo mwendo wa kawaida sana?
Nilipokua kijana nilikua nakaa 160 km/hr kama cruising speed, nimezeeka sasa regardless of type of vehicle max speed is 110km/hr
 
Speed meter/Odometer inakuwa katikati kwenye dashboard. Ili iweje sasa? Mambo mengine ya hovyo tu mi naona.

Kuna gari za Japan nmeona zina hiyo kitu. Leo nlikuwa na jamaa yangu kaomba nimsaidie kumfikisha Dodoma kwa gari yake sababu nami nlikuwa naelekea huko. Nikamwambia hamna shida kwa kuwa mimi sitopata usumbufu wa Traffic njiani

Nmeshika usukani gari lake Toyota Rumion speed meter/odometer ni kama matangazo kila mtu anaona.

Nakanyanga ikifika 160 kms/hr jamaa akiangalia pale kwenye meter anakalia tako moja anashikilia kiti huku amekodoa macho. Mwoga.anasema amewahi kimbiza sana gari akafikisha speed 100 kms/hr.

Kiukweli imenifanya nikose amani sababu kwa watu waoga wanasumbua sana. Ni bora niwe najionea mwenyewe abiria asijue.

Tulifika salama na jamaa ameshukuru. Ila wajapan waache kuwaambia watoto wao kutengeneza magari. Wawe serious. Hi designing nyingine sielewi walifikiria nini.
Napata Tabu kuelewa maudhui ya ujumbe ulioutoa
Samahani kwa usumbufu
 
Huwezi kuelewa mpaka ukiona Odometer za
Rumion
Oppa
😂😂😂😂😂sijui walifikiria nini yan
1627585445455.png
 
Back
Top Bottom