Moyo wangu umekuwa na kiherehere jamani nisaidieni, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moyo wangu umekuwa na kiherehere jamani nisaidieni,

Discussion in 'JF Doctor' started by BLISS, Mar 31, 2011.

 1. BLISS

  BLISS Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mimi naomba msaada, ninaujauzito wa wiki kumi sasa, lakini moyo wangu umekuwa unaenda mbio sana kwa muda then unarudi katika hali ya kawaida, na hii hunitokea mara ninaposimama, kufanya kitu chochote, au nikiwa nataka kuamka, je hii inatokana na nini? na nini cha kufanya? nimejaribu kutumia juic ya ukwaju lakini naona bado haipiti siku bila kusikia hali hii..

  naomba ushauri wetu naamini mtanisaidia jamani maana kuna wataalamu wengi huku akiwepo mtaalamu RIWA.

  ASANTENI,
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  pole dada BLISS...hiyo kitaalam inaitwa 'postural hypotension' (postural - something to do with position, hypotension - low blood pressure), yaani ni mabadiliko ambapo pressure ya damu mwilini hupungua ikisababishwa na kubadilisha mkao. Hali hii inaweza ikatokea kwa biandamu yeyote awe mgonjwa wa moyo au la, awe mja mzito au la. Inasabishwa na ukweli kwamba unapokuwa katika mkao fulani kwa muda mara nyingi ukiwa umekaa kitako au umelala, moyo unakuwa umezoea kupiga katika hali hiyo. Unaposimama ghafla na moyo kunotice kuwa position imechange, basi moyo unajaribu kucompensate hayo mabadiliko, na hivyo pressure inashuka na mapigo ya moyo yanaongezeka, wakati mwingine inaweza ikawa mbaya zaidi hata ukazimia. Hali iyo inadumu kwa muda mfupi tu mpaka moyo utakavyoweza kuaccomodate hiyo position mpya basi dalili zinaacha.

  Kwa kawaida wakati wa ujauzito, wingi wa damu mwilini (blood volume) huwa unaongezeka, na mabadiliko hayo yanaweza tokea haraka haraka wakati moyo ukijitahidi kucope na hiyo hali. Kwa hiyo uwezekano wa kuwa unapata postural hypotension ni mkubwa zaidi ukiwa mjamzito, sana sana uja uzito mkubwa. ni hali ya kawaida kidogo,yaani sio ya kukufanya uogope kuhusu afya yako au maendeleo ya mtoto.

  Cha kufanya: Kuwa makini unapobadilisha position/pozi, sana sana ukiwa unasimama toka kwenye kulala au kukaa kitako (wakati mwingine hata kugeuka unapokuwa umekaa au kulala). Inabidi usimame/ugeuke taratibu ili kuupa moyo muda wa kucompensate hizo changes za position bila pressure kushuka, moyo kwenda mbio au wewe kuzimia. Unapoona moyo unapiga mbio try to relax, take a deep breath iiin..and ooout, na tulia katika pozi moja mpaka mapigo yanavyopotea Yaani huyasikii tena), basi endelea kubadili position taratibu.

  Ukiona hii hali inazidi, basi jaribu kuonana na daktari wa moyo 'cardiologist' kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
   
 3. BLISS

  BLISS Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru kwa ushauri mzuri, nitaufanyia kazi..

  ubarikiwe RIWA
   
 4. U

  UNIQUE Senior Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zaidi ya hapo tumia bio water yanayotengenezwa na bio disc. tembelea Amezcua. kama utahitaji maelezo zazidi niandikie private mail
   
 5. U

  UNIQUE Senior Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tumia bio disc kutengeneza bio water na uyanywe. soma Amezcua
   
 6. kamikaze

  kamikaze JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  yaani dada Blis tatizo ulilonalo ni kama langu, mimi ni mwanaume na siku si chache nimejigundua kuwa na tatizo hilo, inatokea sometimes moyo unapiga haraka haraka inaweza kuwa usiku au mchana, nimeenda hospitali na nimepima vipimo tofauti tofauti na nimeonekana sina tatizo la moyo, kwamba moyo huko normal, ila nikaambiawa inawezekana ni matatizo ya nerves au yawezekana kuna mabadiliko ya hali ya hewa.Kama kuna mtu liishawahi kupata tatizo kama hili tunaomba atujuze kwa kina hasa kuhusu hili.
   
 7. BLISS

  BLISS Member

  #7
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru kwa ushauri, asanteni na mungu awabariki..

  pole sana kaka, kama unatatizo kama langu..
   
 8. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2013
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Punguzeni uzito/unene kwa mazoezi, chakula bora na unywaji wa maji kwa wingi na tatizo litakwisha kabisa.
   
 9. k

  kokwemage Member

  #9
  Dec 19, 2013
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ,

  mimi ilinitokea nikatumia artic c ya forever living nikapona, piga 0718 754 694 kwa maelezo zaidi
   
 10. j

  josephmasamaki Senior Member

  #10
  Dec 19, 2013
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kaka ni kama vile umefunga thread!!

  Joseph Masamaki likes this..
   
Loading...