Moyo Ulojeruhiwa, Kupenda tena ni kazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moyo Ulojeruhiwa, Kupenda tena ni kazi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 20, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Moyo ulojeruhiwa, kuponywa kwake ni kazi,
  Hasa ulodhulumiwa, kutwa hujaa majonzi,
  Ule ulosalitiwa, hutiririka machozi,
  Moyo ukijeruhiwa, huponywa kwa dawa gani?


  Moyo ulojeruhiwa, daima huwa na kovu,
  Kila ukishituliwa, huwa kama nyumba mbovu,
  Nyumba inapovujiwa, ndivyo uzidi ubovu,
  Moyo ukijeruhiwa, huponywa kwa dawa gani?

  Moyo ulojeruhiwa, hauishi maumivu,
  Huhisi kukataliwa, hukwepa tonesha kovu,
  Hofu ya kukatiliwa, huwa kama gari bovu,
  Moyo ukijeruhiwa, huponywa kwa dawa gani?

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  haya Mzee Mwanakijiji..........................karibu
  hizi broken hearted zimekuwa nyingi kweli nowadays,
  hebu wasiliana na Mbu, nae amekuja na ''KUHARIBIWA MAISHA''
   
 3. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Thanks, It has come at the right time.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Especially to YOUTH
   
 5. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Moyo ukijeruhiwa , dawa yake hii hapa

  Ukijeruhiwa moyo wako unakuwa very devastating na ukijaribu kuwa sawa tenaaaa can seem almost impossible, unakuwa hauwezi kumwamini mtu tena na sometimes unajiuliza "Is there anybody worthy of loving?" Ni kweli kabisa kama utakuwa muwazi kwako mwenyewe na open yourself up for healing and refrain from bitterness

  1. Take time to heal, uhusiano ukiisha ni vizuri ukae single for a bit until you can put all the pieces of what happened
  to relationship in perspective. Give youself time to mourn the loss of the relationship and figure what was done.
  Time will take away the pain if you just wait it out.

  2.Usijilaumu kabisa kuwa uhusiano umekufa, uhusiano umefail sababu wote wawili hamjakubaliana na matakwa yenu
  ukijilaumu sana itakupa unnecessary grief, kwa hiyo acha kabisa kujilaumu mwenyewe

  3.Ongea na marafiki na ndugu waliokaribu sana na wewe, waeleze kuhusu uhusiano na kilichotokea kwako chote,
  Sometimes you are too close to the situation to see what is really going on and close friend and family could
  offer a differing opinion...unaweza kuongea hata na watu wazima waliopitia mambo mengi katika maisha na ukapata
  ushauri
  4.Na usi generalise all relationships eti ziko sawa, hii hata humu kwetu MMU ipo mtu analaumu group fulani na kuwaungani
  sha wote,kuwa positive na open to new things, na ujue kuwa watu wote hawafanani kabisa, jua kabisa mtu mwingine
  atakayekuja katika maisha yako atakuwa tofauti na hatakuumiza hisia zako kama aliyepita. Ganaralization only keeps
  you from ever and forever happiness

  5.Believe in love, love is real na ina exist na sababu you had heart broken once haimaanishi itatokea ten kila mara
  unapokutana na mtu. kumbuka mtu wako atakayekupenda na kukufanya uwe happy yupo mahala katulia tuli
  anasubiria muda tu ufike, Optimism is key

  6.Date for the sake of dating. have fun, go out ,screw up and never regret and do not pressure yourself to
  find love, Sio kila uhusiano will turn into love. Furahia maisha na watu wengine na u relax your mind and body,
  You cant get your heart broken if you just having fun and feeling out the relationship

  Sorry MM sijakujibu ki malenga malenga ngoja nijipange
   
 6. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Thanks for the tips, nakubaliana na zote isipokuwa hiyo ya sita, maana katika kuscrew up unaweza kujikuta unapoteza hata reputation yako.

  Nafikiri jambo la msingi ni kuruhusu pain, maana that is what makes us human, we feel happiness, pain, love.

  With time, the pain will go away, only the scar will ramain.
   
 7. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ndio wataalam wa saikologia sasa, na unaposema screw sio ile tu uanyofikiri, hilo neno lina maana nyingi mkuu
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mzee Mwanakijiji
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  kuna mijitu huku kitaa inajiita ''the heart breaker'' sijui inafikiri sifa!!
   
 10. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  As im going through this, nina imani itanisaidia sana, uko juu gaga
   
 11. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unachosema ni kweli, mzee mwanakijiji
  Inaumiza akili, na ni vizuri umehoji
  mwanadamu kwa asili, kujeruhiwa hakubali
  Moyo ukijeruhiwa, dawa yake kusamehe.

  Ni vigumu kuponyeka, ukigoma kuachilia
  Nasema kwa uhakika, kwani nimeshuhudia
  Wale walofadhaika, waweza kufurahia
  Moyo ukijeruhiwa, dawa yake kusamehe

  Namkumbuka Asia, jinsi alivyoumizwa
  Alipotoswa na kulia, mtaa ulishangwazwa
  kathubutu kwachilia, leo moyo umepozwa
  Moyo ukijeruhiwa, dawa yake kusamehe
   
 12. Mvua Ya Kiangaz

  Mvua Ya Kiangaz JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33

  kwa nyongesa tu yero.................
  WHAT SHOULD WE DO?
  What should we do​
  If love is dead​
  And trust buried?​
  As people love today​
  And hate tomorrow as they alway:​
  Should we say allas!​
  Whence our pride divorce?​
  A man likes a woman and woo​
  A woman loves a man through​
  A priest stands for God as to vow​
  Today's matrimonial​
  Is tomorrow's break-up proposal​
  Should I had a toast​
  For today's divorce?​
  What do you mean​
  When say you love someone​
  Tenderly like a shinning moon​
  A huge wedding party in vain​
  A costly honey moon​
  Why to do all these​
  While the end is divorce?​
  As in thy heart no love​
  Dig not thy own grave​
  To be as docile as a slave​
  If not patient​
  Nor tolerant​
  Leave it, don't force​
  For it will end up by divorce​
  Your love is but hate​
  Its foe is but jealousy​
  Yours is not love, but desires​
  Why wed if love isn't there​
  And why promise, is not life?​
  Fool not the heavens with thy passion​
  Since to God divorce is not written. ​
  12/01/2005​
  Dar Es Salaam, Tz​
   
 13. Mvua Ya Kiangaz

  Mvua Ya Kiangaz JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Kuumizwa kubaya....nyie acheni,hebu ona hii.....................

  THE LIE:
  The little maiden in the dark room ready to die​
  Bitter and desperate for the denay:​
  Her love squeezed her for the lie​
  The day and night long, dreams and cry​
  For she was blinded by the lie:​
  10/02/2005​
   
 14. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yote maisha
   
 15. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uko juu sana malenga
   
 16. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Umeiweka vizuri sana!
   
 17. charger

  charger JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ila wapo wazee wa kufariji wajane anaweza akakusahaulisha ndani ya muda mfupi na ukajilaumu why hukumjua mapema.
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nafurahi kama umefurahia
   
 19. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kumbuka mapenzi si mtihani useme ukifeli kuna kusupliment.muhimu ni kujifunza kusahau
   
 20. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dawa ya penzi ni penzi,tafuta wako mpenzi,
  siwe kama yake inzi,yalonuka kuyaenzi,
  panda mpaka kimawenzi,tafuta wako kipenzi,
  Moyo ukijeruhiwa,dawa yake ndio wewe,

  Akija kumwaga mboga,na wewe mwaga ugari,
  wako kama kwenye mbuga,mwaga sera kifahari,
  wenye shingo ka ya twiga,watanashati mahiri,
  Moyo ukijeruhiwa,dawa yake ndio wewe,

  Usitafute mchawi,mganga wake mapenzi,
  siende hata malawi,sera zako tegemezi,
  mwimbie sandakalawi,lazima kwite mpenzi,
  Moyo ukijeruhiwa,dawa yake ni wewe,

  Ngoja nilitue nanga,usiniite mbeya,
  Nikamuone ma manga,kule aliko kyeya,
  Nitapita hata Tanga,mwanakijiji oyeya,
  Moyo ukijeruhiwa,dawa yake ni wewe.........
   
Loading...