Moyo sasa abanwa z’bar kauli yake ya muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moyo sasa abanwa z’bar kauli yake ya muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Na Mwinyi Sadallah

  Baraza la Wazee wa CCM na UVCCM, wameitaka jamii kuyatahadhari matamshi yanayotolewa na Waziri wa zamani wa Serikali ya Muungano, Hassan Nassor Moyo, kuhusu mwelekeo na hatma ya Tanzania.

  Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti, Wazee na UVCCM walimtaka Mzee Moyo kuyatafakari maoni yaliotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere, Profesa Issa Shivji.

  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar (BWCZ), Makame Mzee Suleiman, alisema matamshi ya Shivji yana msingi ili kulilinda Taifa lisibomoke kinyume na mtazamo wa Moyo.

  Akiyazungumzia matamshi ya Mzee Moyo alidai yanaweza kutafsiriwa na wana jamii kama yanayotaka kulisambaratisha Taifa ambalo limejengeka kwa misingi ya umoja wa kitaifa.

  Mwenyekiti huyo wa Wazee Zanzibar, alisema hatakiwi kuyakebehi mawazo ya waasisi wa Muungano ila kuuheshimu uoni wa kitaalam wa Shivj kwa utulivu na historia.

  "Mzee mwenzangu hapaswi kuponda mawazo ya waasisi wetu, ana wajinu na ulazima wa kuyatafakari kwa kina maoni ya Shivji kuhusu hatma ya Muungano wa Serikali mbili," alisema.

  Akieleza kwa upole, alisema maoni yasiozingatia chimbuko, asili na sababu ya kiungwana kwetu anaweza kulizamisha Taifa lake katika dimbwi la mivutano badala ya kuliokoa Taifa alioitumikia kwa heshima na uaminifu.

  Mzee Suleiman ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar kwa miaka kadhaa, alisema kusudio la Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume ni kupata Taifa moja lenye umoja, nguvu za kiuchumi na kisiasa.

  Alisema nia ya Mzee Karume na Nyerere ilikuwa ni kujenga Taifa moja la mfano Afrika Mashariki ambalo halitakuwa athari zilizopandikizwa na wakoloni za ubaguzi wa rangi, dini na ukabila.

  "Hapa Zanzibar wakoloni walitugawa kwa matabaka, Karume alichukia sana ubaguzi, ubwana, umwinyi na ukabila, Moyo ajaribu kuweka akiba ya maneno yake, amaana akiba haiozi," alieleza.

  Kwa upande wa UVCCM Zanzibar, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wake, Jamal Kassim, alisema maelezo ya Mzee Moyo yameligawa kundi ya vijana katika mtazamo wa utengano.

  Alisema hilo si jambo jema kwa mtu kama yeye anaeheshimika kutokana na utumishi wake katika Serikali zote mbili za SMZ na SMT kuhesabika hivyo.

  Kassim alisema akumbuke anapotoa matamshi ya mkanganyiko ni sawa na kujaribu kumwaga maji ardhini akitarajia anaweza kuyazoa hapo baadaye.

  "Mzee Moyo atambue maji yakimwagika hayazoleki, hasara yake itakapochomoza haitachagua jina la mtu, kundi au chama cha siasa, hasara huwa ni hasara milele, aliasa.

  Aidha, Kiongozi huyo wa UVCCM Zanzibar aliwataka wanachama wa CCM kuzizungumzia kero zilizopo katika Muungano na ikibidi baadhi ya mambo ya Muungano yaondolewe bila ya kuutikisa Muungno uliopo.

  "Muungano ni kama moyo wa amani na utulivu wetu, nje ya Muungano kunaweza kutokea mtikisiko mkubwa, kwanini tusizungumzie kuziondoa kero ila kutaka Muungano wa mkataba, hapa lipo jambo gani?," Alihoji.

  Tangu kuundwa kwa Tume ya kuratibu maoni ya Muungano, kumeibuka kikundi Zanzibar kinachofanya kampeni za Zanzibar kujitenga katika Muungano wakiungwa mkono na baadhi ya viongozi wa chama na serikali Zanzibar.

  Chanzo: Nipashe


   
 2. a

  ahally Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Enyi watu acheni kuyafanya mawazo ya hao munaowaona nyinyi kama wazee wa CCm na UVCCMZ kama maandiko matakatifu !!!!!
  Kuna mengi wameyafanya hao wanaogopa kufahamika na pia wanahisi watakuja kudaiwa maelezo ya vp watu wa Zanzibar walipotea kutoka ndani ya nchi yao na hadi leo hawaonekani.

  Ama kwa kweli ni story ndefu sana na yoyote ambae anataka apate angalau nusu ya picha halisi basi aende kweye youtube na atafute clipes zenye jina Zanzibar 1964 au Revolution Zanzibar 1964 halafu aone pia anaweza kuangalia mass graves zanzibzr ataona nn kilitendeka na nani alitenda halafu aje atuambie je kwa namna hii tutakuwa na nusra ya Jalali?

  au mwenye masuali zaidi ani PM
  Nawasilisha
   
Loading...