Movies kali za weekend hii (Session 06)

Ni matumaini yangu mko poa. Ni ‘weekend’ sasa, muda ambao tunapata mapumziko, hivyo basi si vibaya kama tukipata wasaa wa kupakua na kutazama filamus kadhaa kwa ajili ya burudani na pia kujifunza.

Bila kupoteza muda, tuzame kwenye hizi hapa ambazo naamini hautajutia ukizipatia muda na bundle lako:

WAR OF THE ARROWS ya 2011.

Hapo kale Uchina ilikuwa ikitawaliwa na familia/koo ya kifalme yenye nguvu, kwa jina Qing, utawala almaarufu kwa jina la ‘Qing Dynasty’, ambao ulipata kudumu toka mwaka 1644 mpaka miaka ya 1912 ulipokuja kurithiwa na Ming Dynasty.

Katika utawala huo, taifa la Uchina, kutokana na sababu fulani za kisiasa, zikaivamia Korea ya kusini ambayo kipindi hiko ilikuwa chini ya Joseon Dynasty. Walituma majeshi yao yenye nguvu pamoja pia na majenerali wao vinara kuhakikisha ushindi unarudi nyumbani.

Katika vita hiyo baina ya pande hizi mbili, mengi ya kutisha yanatokea kama iwavyo kwenye vita yoyote ile. Lakini habari inakuja kuingia chumvi pale ambapo familia moja inapojikuta inahusishwa na vita hii pasipo kutaraji kabisa.

Na ghafla vita inageuka kuwa ya pande tatu! Ni nini kilitokea? …

Bwana mmoja anayeitwa Nam Yi pamoja na dada yake aitwaye Ja, wanampoteza baba yao ingali wakiwa wadogo kabisa kwa kutuhumiwa kuwa msaliti wa nchi. Kutokana na hilo, rafiki wa marehemu baba yao anawachukua na kuwalelelea kama watoto wake mpaka wanakua kabisa.

Lakini kutokana na historia ya baba yake kutuhumiwa kama msaliti wa nchi, bwana Nam Yi anashindwa kupata ajira ya maana popote pale hivyo analazimika kufanya tu shughuli ya uwindaji ambayo inampelekea kuwa mtaalamu mzuri wa kutumia silaha ya upinde na mishale, wakati huo akitumai pia na maisha ya dada yake yatakuwa vema hapo mbeleni.

Mungu si Athumani, dada yake akaja kupata mchumba aliyekuwa na dhamira ya dhati ya kumuoa. Kila mtu akafurahi na kushangilia. Lakini katika mchakato wa ndoa, siku hiyo ndipo mambo yanapogeuka kabisa na maisha yao yanachukua upili wa mchakamchaka wa kifo ama uhai!

Jeshi la Qing Dynasty ambalo limeivamia Korea, linajiri katika eneo hilo na kuanza kutumia mapanga yao kukatisha uhai wa watu lukuki waso na hatia. Kama haitoshi wanateka pia na wengine wapate kurudi nao Uchina wakawatumie kama watumwa.

Miongoni mwa mateka hao, anakuwemo bibi na bwana harusi! Yani siku yao ya ndoa, na wao ndo wanageuzwa watumwa!

Sasa Nam Yi ambaye yeye hakuwa kwenye sherehe bali yu milimani akisaka kitoweo, anasikia vurugu za uvamizi kutoka mbali. Anapata na shaka. Upesi anarejea sehemu ya tukio na kukutana na maiti nyingi, mojapo ikiwa ni baba yake mlezi! Kama haitoshi anakuta na dada yake pia hayupo!

Bwana Nam Yi alishampoteza baba yake mzazi. Amempoteza sasa na baba yake mlezi. Kwake hii inatosha. Hawezi kumpoteza na dada yake. Anajitazama na kuona kitu pekee anachoweza kukitumia kwa ufasaha ni mkono wake ukiwa umeshika upinde na mshale … sasa mkono huo anaupa jukumu moja tu, kupambana na jeshi, bila kujali la ukubwa gani, kumuokoa dada yake kabla muda haujamtupa mkono!

Bwana Nam Yi akiwa hayupo upande wa yeyote yule, jeshi la mtu mmoja, ataweza kuukwea mlima huu kwa ajili ya dada yake?

View attachment 1510041
View attachment 1510042
GREEN ROOM ya 2015.

Kama wewe ni mpenzi wa ‘survival movies’, filamu ambazo watu hupambania uhai wao dhidi ya mazingira ama watu katili, basi hii hapa ni yako. Escape Plan, SAW na Wrong Turn ni baadhi ya vielelezo vizuri vya Survival Movies, kama utakuwa umezitazama basi hautakuwa mgeni kwenye hili.

Katika movies hizi, unafanya lolote lile lililopo ndani ya uwezo wako kuhakikisha unabakiza pumzi ndani ya mwili wako. Swala la kusema lipi ni haki na lipi ni dhambi, huwa havipo. Hivyo utavijadili baadae endapo ukifanikiwa kuwa hai.

Katika filamu hii, kuna mabwana wadogo wanne wenye malengo ya kuwa maarufu kupitia muziki wa aina ya rock. Ni ‘ma underground’ ambao pesa hawana, na pia sababu vilevile umaarufu hawana wanalazimika kufanya vijitenda ama ‘vijishow’ vya hapa na pale kudunduliza pesa.

Wakiwa kwenye harakati hizo, mmoja wao anapata ‘koneksheni’ ya kutumbuiza kwenye moja ya klabu ndogo ambapo anaamini watapata pesa angalau kidogo zaidi kuliko hizo zingine wanazozichanga kwengine.

Wanakubaliana na kufika eneo la tukio. Ni klabu fulani ambayo inakaliwa na jamii ya ‘skinheads’, kwa kuweka habari vizuri Skinheads ni jamii fulani ya wazungu ambayo huwa na desturi ya kunyoa nywele zao kabisa ama kubakiza nywele kiasi kidogo kichwani.

Kiutamaduni Skinheads ni watu wakorofi na wahusishwa na milengo ya kiubaguzi wa rangi. Kama wewe ni mtazamaji mzuri wa movies basi lazima utakuwa umekutana na hawa jamaa pahala fulani. Mara nyingi wakiwa katika makundi makundi, wana michoro miilini na hupendelea kuvaa vijikoti fulani vya jeans vilivyyokatwa mikono.

Sasa mabwana wale wadogo wanne, kama ilivyokuwa imepangwa, wakapanda jukwaani kupiga show. Bahati mbaya kila wanachokiimba hamna kitu! Wanaishia kutazamwa tu kana kwamba wanajiimbia wenyewe. Lakini isiwe kesi, alimradi walikuwa wanalipwa, wandugu wakamaliza na kupewa chao.

Unaweza kudhani kwa wanamuziki hii siku ilikuwa mbaya, lakini huwezi amini yajayo ndo’ yalikuwa yanafurahisha zaidi. Huu ulikuwa ni mwanzo tu.

Wakiwa wanaondoka zao, mmoja wao, msichana, akakumbuka kuwa amesahau simu yake katika chumba cha kijani (Green Room). Mwenzake akajitolea kwenda kuifata, alipofika huko anastaajabu kuukuta mwili uliouawa kwa kuchomwa kisu! Anapagawa. Anapiga simu polisi lakini si punde mabaunsa wa klabu wanawapokonya wote simu na kuwageuza kuwa mateka ndani ya chumba cha kijani!

Sababu simu ilikuwa ishapigwa polisi, sasa inabidi mabwana hawa watengeneze tukio ili kuwapumbaza polisi wanaokuja. Hapa ndo’ utajua hawa watu wana roho ngumu. Mmoja anamchoma mwenzake kisu ili ionekane ilikuwa ni ugomvi tu wa klabu na si kingine.

Baada ya kuwapumbaza polisi, sasa inabakia kazi moja – kuwaua hawa jamaa ili kuteketeza ushahidi wote. Hapa sasa ndipo akili inapotumika na pia ujasiri wa hali ya juu. Nani atakayeibuka kuwa mshindi?

Wakiwa wamefungiwa ndani ya chumba tena ndani ya klabu yenye watu wa mrengo mmoja, wanakikundi hawa wanatokaje salama mbele ya mikono ya watu wanaodhamiria kuwaua? Aisee … ni jino kwa jino! Hapa ndipo utakapojua kuwa siku zote ulizoishi, hujawahi kufikia mpaka wa wema na utu wako ukageuka kuwa mnyama!

View attachment 1510043
View attachment 1510044
UNTRACEABLE ya 2008.

Tunajua kuna baadhi ya kesi zishawahi kutokea kuwasumbua sana wanausalama kiasi kwamba wakaamua kunyoosha mikono juu wenyewe, rejelea kisa cha D.B. Cooper. Lakini pia tunajua baadhi ya visa ambavyo vilisumbua sana wanausalama lakini hatima yake ikapatikana, katika mlolongo huo damu na jasho vikitawala.

Hii ni kwa ajili ya wapenzi wa mambo hayo. Movies aina ya thriller! Movies za ‘misako’, utumiaji wa akili, kimuhemuhe na taharuki!

Mambo ni haya … mwanamama aitwaye Jennifer Marsh ni afisa wa shirika la kipelelezi la Marekani, FBI, akiwa kati ya maafisa wa juu kabisa katika kitengo cha upambanaji na uhalifu wa mitandaoni ‘cybercrime.

Ni bayana, huenda amekuwa akikutana na kazi nyingi na za hatari. Ana uzoefu wa kila namna kupambana na maadui wa namna zote ambao wapo nyuma ya ‘keyboard’ ama ambao wapo kando na keyboard … lakini kwasababu dunia haiachi kutufunda, anakutana na kisa cha aina yake.

Kisa kinachomjuza kuwa dunia ni ungo ulobebelea kila aina ya uchafu!

Achilia mbali mitandao ya picha za ngono, picha ambazo hutazamwa na kupakuliwa kwa maelfu kila siku duniani, bwana mmoja anaibuka na mtandao wa aina yake, kwa jina Killwithme.com, ambapo humo kazi ni moja tu, unaalikwa kushuhudia kifo cha binadamu mwenzako! Kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake … Kadiri watu wanavyojiunga katika tovuti hiyo na kutazama, ndivyo mauaji nayo yanavyozidi kufanyika kwa upesi na ukatili!

Pengine unaweza dhani kazi ni rahisi tu. Wataalamu wa mtandao wakiingia tu kazini ku – shut down tovuti hiyo mambo yanakuwa yashakwisha, lakini naye muuaji alilifikiria hilo. Anatengeneza mfumo wa kipekee kabisa ambao unaruhusu ‘server’ yake kujizalisha kwa upesi pindi tu inapoathiriwa ama kulazimika kuzimwa!

Hivyo matangazo yanabakia palepale. Yakizidi kudaka watu wanaokuja kustaajabu, nao pasipo kujua wakizidi kuongeza mateso kwa wenzao waliokifungoni. Kila mtu anapoongezeka kutazama mauaji haya, ‘automatically’ anakuwa amewezesha mtego wa kifo kwa mhanga, zaidi na zaidi.

Na kama ujuavyo binadamu na hulka yake, msemaji wa wanausalama anajaribu kuwatahadharisha watu kutokuingia kutazama yanayorushwa katika tovuti hiyo lakini ndo’ kwanza anakuwa amaeupigia chapuo. watu wanazidi kumiminika kushuhudia.

Sasa Jennifer analazimika kuingia kazini. Mosi, kumtafuta muuaji na makazi yake, lakini kujua ni nini kipo nyuma ya mauaji hayo … hali inakuwa tete zaidi pale ambapo Jennifer anapojikuta anaweka usalama wa familia yake rehani na vilevile anampoteza afisa mwenzake, bwana Griffin. baada ya kutekwa na muuaji na kuonyeshwa mubashara akiuawa.

Endapo Jennifer asipompata bwana huyu, si yeye tu na nchi haitokaa kwa amani, bali pia familia yake: binti na mama yake! …

Hivyo haya yanakuwa ni mapambano binafsi!

View attachment 1510045
View attachment 1510046
GHOSTS OF WAR ya 2020.

Upekee wa filamu hii unakuja kwa kuchanganya ‘themes’ mbili, visa vya kivita na ‘horrors’. Ni aghalabu kukuta kitu kama hiki. Na kama wewe si mwoga wa kutazama vitu vinavyorukisha moyo kichurachura, basi karibu na hapa.

Hii ni filamu inayowahusu wanajeshi wanne wa kimarekani ambao wanapambana kwenye vita ya pili ya dunia. Wanajeshi hawa, ingali wenzao wakiwa upande mwingine wa mapambano, kikosi chao kidogo kinapewa kazi ambayo inaonekana nyepesi na salama zaidi kwa mara ya kwanza ukiisikia lakini inabadilika na kuwa mlima ambao haukudhaniwa!

Mabwana hawa, wakiwa ndani ya kombati na mikono iliyobebelea bunduki na risasi, kazi yao ni moja tu - kushikilia kasri la kifaransa lililokuwa linakaliwa na maadui zao wajerumani huku wakiwa wanangoja vita hii inayoelekea ukingoni iishe.

Wakiwa katika kasri hii, ndipo wanagundua ni kheri hata yale yalokuwa yanatokea kwenye uwanja wa vita kwani ya humu ni hatari zaidi! Wanasikia sauti za ajabu. Wanaona viumbe vya ajabu! Viumbe vinavyoaminika kuwa familia ya watu waliokuwa wanakalia makazi haya hapo awali kabla ya kukumbana na hatma yao.

Familia ambayo iliuawa kinyama na jeshi la NAZI la kijerumani, mtoto wa kiume akizamishwa maji, wa kike akinyongwa na baba akichomwa moto hai!

Ingali haya yakiwa yanapamba, huko nje napo maadui wanawasili.

Chukua muda wako, tazama. Mwisho wa filamu kuna ‘twist’ moja tamu sana. Utajua hujui.

View attachment 1510047
View attachment 1510048
MULAN ya 2020.

Hakuna filamu iliyowahi kuongozwa na ‘director’ mwanamke ikatumia budget kubwa kama hii, pengine huko mbele lakini kwa sasa hii ndo’ inashikilia rekodi. Imetumia takribani dola za kimarekani milioni mia mbili! … si mchezo. Na ukitaka kujua hiyo pesa ilienda wapi, tazama filamu hii uone kila kitu kilivyotulia kikatulizwa … moja ya kazi matata ya Disney.

‘setting’ yake ni uchina ya kale, kipindi hiko ikiwa inatawaliwa na mfalme ambapo nchi inaingia kwenye hali ya dharura kutokana na hatari ya kuvamiwa na watu kutoka kaskazini.

Watu hao wa kaskazini ni hatari sana! Jeshi lao ni zaidi ya majeshi mengine kwani wananguvu kupita uwezo wa binadamu wa kawaida huku wakiwa wanaongozwa na mwanamke mwenye nguvu za kichawi! – the witch … hili jeshi linaweza panda na kukimbia juu ya ukuta kama vile miguu imetiwa sumaku!

Hivyo basi mtawala wa uchina anatoa amri kuwa kila familia ndani ya Uchina itoe mwanaume mmoja kwenda kupambana vita.

Hiyo ni amri!

Kila familia inafanya vivyo, lakini katika familia ya bwana mmoja mzee ambaye hapo kale alikuwa mashuhuri kwenye sanaa ya mapambano, inakuwa tabu kwani hana mtoto wa kiume isipokuwa wasichana wawili na mkewe tu. Kwasababu hiyo basi, inalazimika bwana huyo ndo’ achukuliwe akahudumie jeshi.

Kumuokoa baba yake toka kwenye kadhia hiyo, binti mkubwa wa familia hii, Hua Mulan, anaamua kujitoa ajiunge jeshini. Anavalia na kuigizia kiume akianza safari ndefu yenye majaribu mengi yanayomhitaji kuonyesha ufanisi na ukomavu wake kwenye sanaa ya mapigano … tena kandokando ya wanaume mashababi!

Maisha yake yanakuwa ya kuigiza, lakini zaidi ya hatari akiwa mbele kwenye mapigano yasiyo na macho. Kufa ama kupona.

Ni nini hatma ya mwanamke huyu katika ulimwengu wa wanaume? … nini hatma yake mbele ya jeshi lenye nguvu ya ajabu ambalo lipo mbele yake kama adui? … atarudi nyumbani akiwa hai ama ndani ya jeneza na kilio?
View attachment 1510049
View attachment 1510052
BONUS MOVIE:-

THE WAILING

Mgeni aweza kuwa baraka ama laana. Kila kitu kina pande mbili, mwanga na kiza chake, lakini katika hayo tujichunge tusije kuchanganya upande mmoja kwa gharama za ule mwingine kwani sikio bwana halichagui cha kumeza, vyote hubeba, kazi inabakia kwenye kichwa chako kujua kipi ni hiki na kipi ni kile.

Katika kijiji kimoja cha huko mbali na mji, kunazuka ugonjwa usioweza kuelezeka. Ugonjwa ambao ni mpya kwa kila mmoja hata wale waliokula chumvi wasiweze kuuelezea hata kidogo. Ni ugonjwa ambao hautishi kwa kuambukiza kwake bali kwa matokeo yake.

Punde mtu anapoukwaa, anapatwa na upele wa ajabu, na kama haitoshi anageuka akili kuwa mwehu wa mauaji anayewinda na kuua familia yake!

Ugonjwa huo unapoteza amani na furaha yote ndani ya kijiji hiki. Kila mtu anaishi kwa hofu na hakuna anayeonekana kuwa salama hata familia ya afisa wa polisi kwa jina Jong – Goo, nayo inakumbwa na janga hili baada ya mtoto wao mdogo wa kike kuanza kuonyesha dalili za wazi za maambukizi.

Katika hii taharuki, wanakijiji wanashuku kuwa ugonjwa huu wa ajabu utakuwa umeletwa na mgeni fulani wa aina yake ambaye amejiunga nao si muda mrefu. Mgeni huyo ana asili ya Japan, na kimakazi anaishi kwa kujitenga na wengine huko juu mlimani.

Afisa Jong – Goo anaamua kulivalia njuga hili swala. Baada ya kusikia na kushuhudia mambo kadhaa, anashawishika kufunga safari kwenda kuonana na mgeni huyo aliyeingia kijijini. Akiwa ameongozana na mwenzake na pia mchungaji anayeweza kuzungumza kijapani, wanafika huko na kubaini katika makazi ya mwenyeji wao huyo kuna madhabahu yenye kichwa cha mbuzi, na kutani kuna picha za wale wote waliowahi kuumwa ugonjwa huo wa ajabu na hatimaye kufa!

Yote tisa, kumi afisa huyo anakutana na kiatu kimoja cha mtoto wake katika makazi ya bwana huyo! Kitu ambacho kinaonekana baadae huenda kikawa kina mahusiano na ugonjwa wa ajabu kwa binti mhusika.

Katika harakati za kutafuta suluhisho, mama mkwe na afisa Jong – Goo anamwita mtaalamu aje kung’amua nini haswa kinamsumbua mjukuu wake. Mtaalamu akasema mhusika ni jamaa yule mgeni … yule bwana anayeishi kule mlimani! Upesi inabidi ifanyike ibada ya utakaso kumsafisha binti kabla hajakumbwa na makubwa.

Lakini je, mtaalamu huyu ni wa kuaminika? Na kama ndivyo, ni hatua gani alichukua baada ya mtuhumiwa wake kuwasili ndani ya hili eneo? … kufupisha tu habari ni kwamba, ndani ya kijiji hiki kuna watu ambao wanashirikiana na bwana huyu mgeni kwenye kukusanya nafsi za watu kwa ajili ya kumshibisha shetani wanayemwabudu.

Sasa swala linakuwa si kupambana na adui kwani tayari anajulikana bali kujua ni nani rafiki na ni nani adui aliyejiveka ngozi ya kondoo, kwani kosa kidogo litagharimu uhai wako na wa familia nzima!

Ingali hayo bado yakiwa kitendawili, mtoto wa bwana Jong – Goo anaanza kufanya mauaji! … muda unayoyoma, bwana Jong – Goo inabidi afanye maamuzi!
View attachment 1510054
View attachment 1510055
Lufufu legacy
 
- BONUS MOVIE!



ILLANG: THE WOLF BRIGADE (2018)


"We are not humans in wolves clothing, we're wolves in Human clothing!"

(Sisi sio binadamu ndani ya ngozi ya mbwa mwitu, sisi ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya binadamu!)


Korea ilikuwa ni nchi moja kabla ya kutokea mifarakano iliyopelekea kugawana na kutengana kwa mipaka ya moto! Wengine wakawa wa kaskazini (North Korea) na wengineo kusini (South Korea).

Sasa katika mwaka 2029, nchi hizi mbili zinaamua kukaa kitako wayamalize, wawe kitu kimoja tena kama ilivyokuwa hapo awali. Ndugu waonane, mipaka ifutwe na watu waishi chini ya serikali moja!

Lakini ni bayana kuna watu wanafaidika na mfarakano uliopo. Watu hawa hawataki kwa namna yoyote ile kusikia nchi hizi mbili zinaungana hata kama italazimika damu imwagike na watu maelfu kufa.

Watu hawa wapo ndani ya serikali na hata raia wa kawaida. Na kuonyesha adhma yao wanaunda kundi la kigaidi linaloitwa "The Sect". Kundi ambalo ajenda yao ni moja tu, kutokomeza na kukwamisha mpango wa muungano.

Kufuatana na hatari ya kundi hilo, serikali nayo inaunda kundi maalumu la maafisa wa usalama "The Wolf Brigade" kwa ajili ya kupambana na The Sect ...

Hapo ndo' moto unapowaka...

The Wolf Brigade wanapambana na magaidi na maafisa wenzao pia wa serikali ambao wapo nyuma ya wadhalimu hawa!
View attachment 1510057
moto huu acha kabisa
 
Hahahaha mwisho wa siku unajua hujui!

Sema kuhusu VIVARIUM kwa watu ambao hawapendi 'tragic end' itawauma maana haiishi vile wewe utakavyo iishe ... sasa hapa ndo mtu anakuja kusema movie mbaya hii
Imenikumbusha muvi inaitwa mine jamaa kajua kakanyaga bomunkateseka wee kusuburi msaada kwa zaidi ya siku mbili jangwani. Baadae anaamua tu kuuondoa mguu anakuja kujua kumbe alikanya kikopo tu.😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom