Movie Reviews

Katika maisha yangu huwa nadhani moja ya vitu ninavyopenda ktk ulimwengu wa entertainment upande wa movies n series ni kuangalia zenye maadhi ya kusikitisha na si kusikitisha tu kikawaida ila napenda kuangalia movie/series initoe machozi kweli kweli.

Napenda movie/series za namna hii maana zina mafunzo mengi sana ndani yake ambayo si ya kuigiza ila unaona kbsa hii movie/series akili ilitumika ktk utungaji wa story na ktk story hizo huwa naondokaga na mafunzo makubwa sana ya maisha.

Kwa sasa naangalia drama moja ya korea inaitwa BAD THIEF,GOOD THIEF naenda mwishoni sasa ila kusema ukweli hii movie imeniliza zaidi ya mara 5 yani unaangalia movie inafika mahali unaweka pause kidogo Unalia weeee then ukimaliza unarudi unaendelea iangalia.

sitamani kukosa movie ya kuangalia baada ya hii kuisha naomba yeyote anaejua series/movie yenye mahadhi ya namna hii anisaidie kunipa Jina tu la hiyo movie,namba isiwe movie yenye mabunduki mabunduki.

NOTE: iwe inaliza kweli kweli,sio niishie kusikitika tu na kuwaonea huruma,movie flani ambayo ukiiangalia unaishia tu kushusha machozi na kutafakari maisha yalivyo,binadamu walivyo,nk vitu vya namna hiyo.

Asanteni kwa wote mtakaochukua muda wenu ku comment jina la movie,naweza nisikushukuru kwenye comment ila naomba yeyote ataechuka muda wake kunitajia tu aina hiyo ya movie nimpe Asante na Mungu alie juu akubariki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom