Moved: Kujivua Gamba kwa CCM, (Kujitangaza nchi nzima) na Toba ya Kilokole | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moved: Kujivua Gamba kwa CCM, (Kujitangaza nchi nzima) na Toba ya Kilokole

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kingo, Apr 14, 2011.

 1. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Sijaelewa mantiki ya CCM kuammua kwenda kwa wananchi, nchi nzima kujitangaza kwamba imejivua gamba (CC na Sekretarieti bila shaka ndo vilikuwa gamba) wakati mambo kadha wa kadha yanabaki bila majibu.
  Nianza kutoa mifano michache yenye mwelekeo wa kujitangaza "mtu"(?) anapovua gamba. Kule kanda ya ziwa kwa ndugu zangu Wahaya, kijana akioa kimila (kumbeba/ kutorosha binti usiku) kesho yake asubuhi atapiga makofi mbele ya wazee, akishika miguu ya akina baba na kwa akina mama matiti kama ishara ya utambulisho kuwa ameo na hivyo kaingia daraja lingine la "shumaramu waitu". Ila kijana hasemi kama faini ya kutorosha binti atalipa wala mahari atamaliza vipi na kwa wakati gani.
  Halikadhalika kwa waumini wa kilokole, wanapofanya toba, huenda majukwaani na kujitangaza madhambi yao kabla ya "kuupata" wokovu kuwa (mfano) walikuwa wezi, wabakaji, wazinzi, vibaka, walevi, n.k. na makofi na vigelegele vingi kusindikiza uzandiki na ushuhuda huo. Ila huwa hawasemi kama mali waliyoiba wanarudisha, binti aliyebakwa atasaidiwa vipi, nk. Ila wapendwa hupiga tu vigelegele.
  Tukirudi kwa CCM, wanadai kujivua gamba na hivyo wakajitangaze kwa wananchi kuwa sasa ni wapya. Kama gamba lilikuwa ni CC na Sekretariati yake, ni kw avipi waliojiuzuru CCM waendelee kubaki na vyeo vyao serikalini? kama wameshindwa kumshauri mwenyekiti wao kwenye chama, wanawezaje kumshauri huyo mwenyekiti/ aka Raisi kwenye baraza la mawaziri? Si wakati muafaka wakkachia na nafasi zao za kiserikali tukaamini?
  Kama CCM na serikali yake ndo hiyo iliyogubikwa na kashfa za rushwa, Meremeta, EPA kwa ujumla wake, BOT twin towers,Tangold, Deep Green, (Stimulus Package 2009) e.t.c. inatuelezeaje juu ya kujivua kwake gamba na kashfa hizo? Je hatua gani za kisheria zimechukuliwa kwa watuhumuwa, fedha ya EPA iliyorudishwa na watuhumiwa ni kiasi gani, iko wapi, na ni kina nani wahusika? Je kama ni wanachama wa CCM na pengine wajumbe wa NEC na bado wanaendelea kupeta, ni gamba gani wamevua? Tutawaamini vipi? Sumu ya nyoka si iko palepale hata akibadili gamba?
  Si bora hiyo fedha ya kuzunguka kwa wananchi kujitambulisha na ku-propaganda kuvua gamba wakatekeleza ilani ya chama 2010-2015 na ahadi za kampeni/uchaguzi auliopita nasi tutaona kwa matendo badala ya kutushibisha sifongo?
  No mtazamo tu.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Vipi taarifa za kiintelijensia zinasemaje kuhusu hilo gamba lilivuliwa kutangazwa hadharani. Polisi watakuwa impartial ili watumie taarifa hizo kuwamininia mabomu na risasi za moto?
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Ahaaaa! walipopitisha bajeti mbovu 2007 walipeleka mawaziri mikoa yote kuwahadaa wananchi na badala ya kurekebisha wakazidi kuharibu,

  hadi JK,Kinana nao waachie ngazi maana hata wao ni gamba chafu,na kama haijawahi kuwa tusubiri tu kidogo tuone kama bakora za Mwembe chai hazitaamia CCM... wamfukuze EL tuone kama CCM inabaki
   
Loading...