Mourinho: Ronaldo hakuwa na msaada fainali ya Euro

DesertStorm

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
2,517
1,714
MOURINHO: RONALDO HAKUWA NA MSAADA FAINALI YA EURO
August 6, 2016

Jose Mourinho amesema kwamba Cristiano Ronaldo hakuwa na msaada wowote kwenye mchezo wa fainali wa Euro ambapo Ureno waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ronaldo alilazimika kutoka nje katika kipindi cha kwanza baada ya kuumizwa na Dimitri Payet lakini haikuzuia timu hiyo kuibuka na ushindi na kutwaa ubingwa.

Mchezaji wa zamani wa Ureno na Benfica Antonio Simoes, alimkosoa Ronaldo kwa mbinu zake, na Mourinho amekubaliana naye kwamba, mchezaji huyo hakuwa na msaada wowote bali tu alizidiwa na hisia.

“Mchango wake ndani ya dakika za mwisho za mchezo wa fainali haukuwa chochote,” Mouriho alikiambia kituo cha runinga cha Sport TV. “Kulikuwa na wachezaji 11 uwanjani ambao walikuwa wakitekeleza majukumu yao, na mtu pekee aliyekuwa akiwaongoza ni kocha tu basi.”

“Kikubwa nilichokiona kwake ni kuzidiwa na hisia tu, kwa mtu yeyote ambaye aliiangalia timu vizuri, isingechukua muda mrefu kwako kufanya kile walichodhamiria.

“Alishindwa kudhibiti hisia zake, japokuwa sio kitu kibaya. Nadhani wachezaji 11 ambao walikuwa uwanjani kwa wakati huo, walikuwa na dhamira moja tu ya kutaka ushindi, na walikuwa wameonesha dhamira hiyo.
 
Yule hana lolote basi vijana wa jf wanampamba tu ili kuondokana na aibu zao. Lkn ukweli utabakia pale pale ze king iz ze fadha of futbol,nikisema ze king anajulikana hata watoto wa miaka miwili wanamjua mnyama huyu

Kwaherini
 
Yule hana lolote basi vijana wa jf wanampamba tu ili kuondokana na aibu. Lkn ukweli utabakia pale pale Mfalme ndie baba wa soka,nikisema mfalme anajulikana

Kwaherini

Naunga hoja ya wawili hao, unless kuna walioanza kuangalia mpira 2010 watakuja kupinga hoja zao
Sasa mtu aliumia mlitaka afanyaje!!?

Au mlitaka akose penalt kama Messi ndio mseme alikuwa na msaada
 
1470612859937.jpg
bingwa wa Euro 2016
 
Tatizo ni 'egoism' ya CR7 - kujifanya kocha baada ya goli kufungwa na kujishangilia mwenyewe mpira ulivyoisha (... badala ya kuwakimbilia na kuwapongeza mfungaji wa goli na kipa kama kikosi kizima kilivyofanya).
Cristiano Ronaldo’s Portugal teammates have hailed his pep talks as the catalyst behind their 1-0 victory over France in Sunday’s
European Championship final.
The Real Madrid forward and national team captain was stretchered off the Stade de France field in the 25th minute after suffering an early knee injury.
Despite leaving the pitch in tears, Ronaldo returned to the touchline after half-time and barked directions at his teammates for the remainder of the match.
After Eder’s strike sealed victory for Portugal in extra-time, Cedric Soares, the Southampton full-back, revealed how Ronaldo had inspired the win.
"He gave us a lot of confidence and he said, 'Listen people, I'm sure we will win this Euro so stay together and fight for it'.
"It was unbelievable,” Soares added. “All the team had a fantastic attitude and showed that when you fight as one you are much, much stronger.
www.independent.co.uk/.../cristiano-

Mkuu
Sasa wachezaji walo cheza wenyewe wana sema jamaa alikuwa bonge ya msaada hasa nyie mlo kuwa nyumbani kwenu mnabisha nn!!?

Ronaldo hakuwa na haki ya kushangilia!!?
Maana sja kuelewa hapo
 
Mkuu
Sasa wachezaji walo cheza wenyewe wana sema jamaa alikuwa bonge ya msaada hasa nyie mlo kuwa nyumbani kwenu mnabisha nn!!?

Ronaldo hakuwa na haki ya kushangilia!!?
Maana sja kuelewa hapo

Hakuna aliyesema hakuwa na haki ya kushangilia. Nilichoandika ni opinions tu ya baadhi ya wareno ... Hizi ni baadhi ya quotes kutoka kwenye baadhi ya outlets ..

Some observers, including 46-times capped Portugal legend Antonio Simoes, have been critical and suggested the actions were more about his own ego than actually helping the team." ...

Former Benfica winger Simoes, who scored for his country against Brazil in the 1966 World Cup, an injured player "going crazy" on the sideline did nothing to help his team win, and was not the behaviour of a real great."
 
Hakuna aliyesema hakuwa na haki ya kushangilia. Nilichoandika ni opinions tu ya baadhi ya wareno ... Hizi ni baadhi ya quotes kutoka kwenye baadhi ya outlets ..

Some observers, including 46-times capped Portugal legend Antonio Simoes, have been critical and suggested the actions were more about his own ego than actually helping the team." ...

Former Benfica winger Simoes, who scored for his country against Brazil in the 1966 World Cup, an injured player "going crazy" on the sideline did nothing to help his team win, and was not the behaviour of a real great."
Sasa hao wanaosema hayo na Mou ni sawa tuu
Walio cheza wenyewe wana sema alisaidia
Yaan haiwezekani ukawabishia wanao guswa na tukio moja kwa moja halafu u claim kwamba wewe ndo uko sahihi kuliko wao
 
Ronaldo na Mourinho sijui huwa wanagombea nini, hawaelewani kabisa hawa watu. Sijui ni wanaonea wivu hata sielewi.
 
Mourinho alipokuwa Madrid alikuwa anampa Ronaldo kila aina ya sifa, alipotoka Madrid hachoki kumdiss kwa kila afanyalo, uzuri wa Ronaldo huwa hajibizani naye, anamjibu uwanjani. Alisema Hazard ni zaidi ya Ronaldo alipokuwa Chelsea, walipokutana kwenye mechi Madrid vs Chelsea Ronaldo akatia goli 2, huku Hazard akiflop vibaya
 
mourinho namkubali lakini hapa kaniboa, ronaldo kaumia tena analia kwa uchungu kabisa kwa hisia kwa yeyote aliyeangalia game anajua hilo, mtu hadi kashindwa kuukimbili mpira, sio rahisi kwa mchezaji kama ronaldo kuomba mwenyewe atolewe, mimi mwenyewe gheto machozi yalinirenga, pamoja na jeraha ilibidi dk90 aje kuwapa morali wenzake, mwacheni ronaldo aishi maisha yake, ndo maana aliwaambia mnamfuatilia kwa sababu ana hela, ni mzuri na pia mpira anajua
 
Back
Top Bottom