MoU kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MoU kati ya Serikali na Kanisa Katoliki na Taasisi nyingine za Kidini

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Game Theory, Jun 30, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Sitaki kuamini hili lakini uvumi huu umeeneea sana kiasi cha kwamba umenifanya niwe na shauku kutaka kujua yaliyojiri kwenye kusign hiyo memorandum maana naona kwa taarifa nilizokuwa nazo malalamishi ni kuwa serikali imeipa CCT na TEC nguvu kubwa ajabu na matokeo yake leo watu watu wanaanza kulalama kwa nini serikali haiipi nguvu hizo NGO zingine kama walivopewa na serikali. Na under this memorandum seriali inatoa nafasi za kazi kwa Church candidates kwenye chuo chake cha Teachers Training College

  Mfano kuna kipengele kinasema hivi:

  Hakuna ubaya hata kidogo kwa serikali kusign hii memorandum lakini nataka kujiuliza je ni sawa serikali kufanya agreements kama hizi na taasisi za kidnini? na Je imefanya gareement kama hii na taasisi za Kisslam au wahindu au ni Kanisa tu ndio walifanya nao?

  Je, hamuoni hapo mambo ya bilateral negotiations wakaachiwa wataalam wa mambo hayo?
   
  Last edited: Jul 23, 2009
 2. Amosam

  Amosam Senior Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No comment!
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, tafadhali usituonjeshe, tunataka kuila, tushibe kisha tuzungumze!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Negotiation is just a negotiation. Wewe ulitaka iweje? Juzi si kumekuwa na makubaliano kati ya taasisi za dini na serikali kuhusu misamaha ya kodi na mambo yakaenda vizuri? Kusingekuwa na makubaliano hayo unafikiri nini kingetokea?
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Kazi kweli kweli...tafadhali rejea tena usome nilichokipost ndio utaelewa
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sina Cha kusema hapa kidogo, tusubiri tu na kuona mengi sana, hizi ni harakati za uchaguzi mwakani
   
 7. J

  Jafar JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwenye hotuba ya JK kule Mtwara juzi juzi alisema wazi kuwa wamekubaliana na taasisi za kidini. Kwa hiyo hili sio siri. Kwa upande mwingine naona hakuna la kushangaza sana. Taasisi za kidini zinaziba pengo kubwa sana ambalo serikali haiwezi kuli-cover kwa sasa, huduma nyingi za jamii achilia mbali za kiroho kama maji, hospitali, mashule, habari, elimu zote (ya msingi mpaka ya juu), saccoss (deci) n.k. zinachangiwa na hawa jamaa, vivyo kuwa na uhakikika kwamba wana-backup ya serikali ni muhimi maana investment yake si ndogo kihivyo.
   
 8. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Yaliyojiri, yaani una maana yaliyotokea wakati wa kusign au kilichomo ndani ya MoU?
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  yote mkulu wangu..yote
   
 10. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu
  tupe yote basi hapa ili tuichambue vizuri au vipi
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa ilikuaje wakawa wanabeep kuhusu Kodi kwenye Taasisi za Dini??au ndio alitaka kupata credit hapo au vipi??
   
 12. H

  Haruna Malima Member

  #12
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali iepuke Negotiations za namna hii zinatia wasiwasi. Kwa nini iwe Kanisa peke yake? Memorandum ya namna hii ihusishe Dini na madhehebu mengine. Serikali inaongoza wananchi siyo Kanisa. MoU ya Serikali ni kwa manufaa ya nchi siyo Kanisa. Serikali yetu haina Dini ila watu wake wana Dini, wakipewa madaraka ya serikali wasi assume dogma za Dini zao.Kufanya hivyo ni kukaribisha mkanganyiko wa kisiasa, kiitikadi, kifalsafa na kiutawala.Wenye nchi mpo!
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Then kuna hiyo ya Kanisa na Foreign Governments

  makubwa kweli kweli
   
 14. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mzee utuletee document nzima ya momerandum ili tuweze kuisoma na kuichambua. Haka kakipande ulikoKanyofyoa hakatoshi kutuingiza kwenye mjadala wa haki na kweli. Kwa mfano unasema serikali inatoa nafasi za kazi kwa church candidates kwenye chuo cha TTC. Tungependa kuona wapi imeandikwa kwenye hiyo memorandum. Tunapowajadili watu au taasisi ni vizuri tuwatendee haki tukiwa na vielelezo kamili.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani kuna uhakika gani kuwa serikali haijafanya negotiations na taasisi nyingine za kidini?
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Jun 30, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Inawezekana dini au madhehebu mengine hawana cha kunegotiate sasa walazimishwe tu kunegotiate? Chukulia mfano serikali imeingia mkataba na kampuni fulani kuhusu madini ina maana makampuni yote yaingie mkataba na serikali ili kubalance?
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jun 30, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nilitaka nichangie lakini naona kwa makusudi au bahati mbaya umetupa kipande tu cha hiyo MoU. Kuna uwezekano wa kutupotosha kwa hiyo habari yako. Nikisema kuwa habari yako ni uzushi utakataa? Tupe hiyo MoU na source yake, pls!
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Baada ya kuweka suala la mahakama ya kadhi kwenye Ilani ya CCm sasa wanakuja na kuwapoza, sisi yetu macho tutaona mengi sana
   
 19. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kwangu mimi naona kuwa huenda kwa CCT na TEC ku'sign' MoU ni wao kuomba wasaidiwe katika huduma wanazotoa (ikiwa ni pamoja na kutolipa kodi). Kama CCT na TEC wameomba sidhani kama serikali ita'sign' MoU na madhehebu ya Kiislamu ambayo pengine hayakuomba au hayakuwa yameomba kwa wakati huo.

  Mimi ningeona cha ajabu kama serikali itasema ina'sign' MoU na madhehebu ya dini ya Kikristo tu na siyo waislamu. Otherwise, sioni ubaya wowote na hasa kwa mashirika ambayo yanasaidia katika maendeleo ya watu na nchi. Au wewe ulifikiri hiyo MoU ni ya kwa ajili ya kueneza Ukristo?
   
  Last edited: Jul 1, 2009
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Jun 30, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 4,999
  Trophy Points: 280
  GT,

  ..at first nilibabaika na nikaona serikali inajitumbukiza ktk masuala ya kidini.

  ..lakini baada ya kutulia na kutafakari nadhani hii MOU haina matatizo.

  ..hata mataifa makubwa kama MAREKANI yana ushirikiano kati ya SERIKALI na FAITH BASED organisations.

  ..sidhani kama hiyo MOU inaelekeza serikali ktk kusaidia Kanisa ktk shughuli zake za kiroho.

  ..kwa mazingira yetu Tanzania serikali inapaswa kushirikiana na mashirika ya kidini ktk urahisishaji wa utoaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya, maji,mazingira etc.

  ..kama taasisi ya kidini imejenga hospitali na inatoa madawa na chakula sioni ubaya wa serikali kuwasaidia ktk kutoa waganga na wauguzi na kuwalipa mishahara. ushirikiano wa minajili hiyo nadhani ndiyo unaoelekezwa na MOU hiyo.

  ..pia tangu kusainiwa kwa MOU hiyo sijaona dalili zozote zile za serikali kuipendelea dini moja dhidi ya nyingine.

  ..tumeshuhudia serikali ikifadhili mkutano wa Bakwata, ikitoa majengo kwa chuo cha Kiislamu, na kusaidia kutatua ile sakata ya mahujaji kukwama kwenda hijja. pia tumeona serikali ikirudisha shule za kanisa zilizokuwa zimetaifishwa, tumeona viongozi wakuu wakishiriki fundraising za ujenzi wa shule za kanisa etc etc. vilevile kiongozi wa mabohora ametembelea nchini na kupokewa kwa heshima zinazostahili.

  ..badala ya kukaa pembeni na kulalamika labda madhehebu mengine nayo yachukue initiative na kusaini MOU na serikali kama ambavyo makanisa yamefanya. lakini with or without MOU sidhani kama serikali ina nia ya kubagua madhehebu yoyote ya dini.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...