Montserrat
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 10,261
- 13,832
Thanks, nimekuelewa, mimi ni mpenzi mkubwa wa pikipiki and I own one kati ya hizo tatu.Si sahihi sana kusema kuwa hazishiriki kwenye mashindano ya pikipiki, kwani kuna aina mbalimbali za mashindano haya, tofauti inakuja kwenye requirements za mashindano hayo, ambayo huwekwa na chombo kinachosimamia.
Chombo kikubwa kinachosimamia mashindano ya pikipiki ni FIM nacho kina aina nne za mashindano ambayo ni
Road Racing
Motorcross
Enduro and Cross Country
Track Racing
Hii thread imebase zaidi katika Road Racing chini ya daraja la Motorcycle Grand Prix ambayo nayo imegawanyika katika sehemu tatu
Moto3 (125cc)
Moto2 (250cc)
MotoGP (1000cc 4 strokes)
BMW
Haijawahi kushiriki katika MotoGP, hii inaweza kuwa ni kutokana na aina za pikipiki wanazounda.
BMW kama kiwanda wanashiriki katika mashindano ya superbikes(WSBK), ambapo pikipiki zinazoundwa kiwandani kwa matumizi ya kawaida hufanyiwa marekebisho kadhaa na kuweza kushiriki mashindano haya. Ukubwa wa injini katika daraja hili ni kati ya 800cc na 1200cc twins na kati ya 750cc na 1000cc kwa injini ya silinda nne.
Pamoja na kushiriki katika daraja hili kwa miaka kadhaa sasa, BMW haijafanikiwa kushinda mashindano haya.
Tofauti ya pikipiki za MotoGP na Superbikes ipo kwa uundwaji wake, MotoGP ni kwa pikipiki za mashindano tu, huku Superbikes ni pikipiki zilizoundwa kwa lengo la kuingia sokoni kwa mauzo. Hivyo basi MotoGP ina gharama kubwa kiuendeshaji kuliko mashindano mengine ya pikipiki. Zaidi ni maarufu sana ikiwa na wapenzi wengi baada ya F1. Hii inafanya viwanda vingi vikubwa kushiriki mashindano haya. Hapana shaka siku moja tutawaona BMW.
KTM
Ilianza kushiriki mashindano haya katika daraja la Moto3 mwaka 2003 na mwaka 2005 walifanikiwa kushinda Contractor Championship. Katika daraja la Moto2 walishiriki kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kujitoa katika ngazi hizo mbili.
Mwaka huu KTM imeongeza ushiriki wake kwa kuweka pikipiki katika madaraja yote matatu. Kabla ya kuingiza pikipiki katika daraja la MotoGP walirudi mashindanoni mwaka 2012..
Baada ya mizunguko mitatu ya mwaka huu katika daraja la MotoGP, KTM ipo katika nafasi ya mwisho katika timu 6 zinazounda pikikipi ikiwa na point 2 dhidi ya 70 ya timu Yamaha ambayo ipo nafasi ya kwanza.
Kwa upande wa Afrika, KTM imeweza kutupatia bingwa wa Dunia katika daraja la Moto3 kutoka Afrika Kusini mwaka 2016 - 17, kwa jina ni Brad Binder.
Harley Davidson
Pamoja na kuwa ni washiriki wakubwa wa gwaride la MotoGP huko USA. Kiwanda hiki hakina dalili yoyote ya kushiriki mchezo huu. Hii inatokana na aina ya pikipiki wanazounda kuwa tofauti sana na requirements za FIM.