Moto wawaka jengo la Ushirika, Lumumba

Dotori

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
544
24
Nimepokea taarifa kuwa Ofisi za Brela zilizopo Dar zimeungua moto. Wenye taarifa zaidi kuhusiana na suala hili tunaomba watujulishe pamoja na extent of damage.
 
Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaatttttttttttttttttttttttttttttt!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kama ni kweli, basi Watanzania wanalindwa na Mungu hawana serikali.
 
Katika hali tete ya ufisadi, inakuwa ngumu kuamini kuwa tukio hili ni bahati mbaya.
 
Jana usiku nilikuwa natizama channel 10 na walikuwa wanaleta live moto uliokuwa ukiwaka kwenye jengo la Ushirika pale Lumumba Street Dar. Kwa kuwa naishi maeneo ya karibu na hapo nikaamuwa kwenda kujionea live. Nilipofika hapo nilikuta kweli kuna moto mkubwa kwenye hilo Jengo kwa upande wa kushoto (ukiwa lumumba unalitazama hilo jengo) na moto ulikuwa unawaka chini na magari mengi ya zimamoto yalikuwepo hapo na ulinzi mkali wa askari na silaha ulikuwepo hapo. Nilichoshuhudia mimi kwa macho yangu ni kuwa moto ulikuwa ukiwaka upande wa kushoto, chini, na si upande wa kulia juu ambapo ndio ninavyohamu kuwa zipo ofisi za brela. Sikukaa sana, kwa hiyo sijuwi kama waliweza kuudhibiti huo moto usiendelee kufika upande wa kulia wa jengo na kuwa umefika kuunguza ofisi za brela. Mimi nilopokuwepo hapo, hata ile bank ya CRDB iliyopo chini ilionekana kuwa haijashika moto kwa wakati huo. Ilikuwa majira ya saa saba na nusu za usiku na nilikuwa hapo mpaka saa nane za usiku.
 
Ninaomba serikali itueleze inakuwaje kuhusu haya mambo, lakini pamoja na hayo nataegemea kutakuwa na backup (Photocopy) amabzo zinahifadhiwa sehemu nyingie, hivyo sidhani kama limeharibika neno hapa.
Ili Naitaji kikwete ajieleze please kama hilo Jengo limeungua jamani

Hizo photocopy ndiyo rahisi kucheza nazo maana kama original document haipo, chochote utakachopewa itabidi ukubali. Kwa hiyo bado kuna kazi kama watu tunategemea photocopy.
 
Jana usiku nilikuwa natizama channel 10 na walikuwa wanaleta live moto uliokuwa ukiwaka kwenye jengo la Ushirika pale Lumumba Street Dar. Kwa kuwa naishi maeneo ya karibu na hapo nikaamuwa kwenda kujionea live. Nilipofika hapo nilikuta kweli kuna moto mkubwa kwenye hilo Jengo kwa upande wa kushoto (ukiwa lumumba unalitazama hilo jengo) na moto ulikuwa unawaka chini na magari mengi ya zimamoto yalikuwepo hapo na ulinzi mkali wa askari na silaha ulikuwepo hapo. Nilichoshuhudia mimi kwa macho yangu ni kuwa moto ulikuwa ukiwaka upande wa kushoto, chini, na si upande wa kulia juu ambapo ndio ninavyohamu kuwa zipo ofisi za brela. Sikukaa sana, kwa hiyo sijuwi kama waliweza kuudhibiti huo moto usiendelee kufika upande wa kulia wa jengo na kuwa umefika kuunguza ofisi za brela. Mimi nilopokuwepo hapo, hata ile bank ya CRDB iliyopo chini ilionekana kuwa haijashika moto kwa wakati huo. Ilikuwa majira ya saa saba na nusu za usiku na nilikuwa hapo mpaka saa nane za usiku.

..sahihi kabisa!

..na haukuenea sehemu nyingine. kwahiyo BRELA haijaungua na itakuwa vizuri watu wakiacha ku-speculate kuhusu brela na hujuma dhidi yake!
 
Ninashukuru kwa ufafanuzi. Inasaidia kutoa mwanga kuhusu suala hili hasa kwa sisi tuliopo porini.
 
..mods,

..dotori,

..hiki kichwa cha habari ni vyema kikasomeka "moto wawaka jengo la ushirika,lumumba" au vingine vizuri zaidi.
 
Ni hivi sehemu iliyoungua ni wing ya kushoto ukiwa unaliface jengo la ushirika,huko kuna ofisi mbalimbali za watu binafsi na chuo cha ushirika moshi,upande zilipo ofisi za BRELA na CRDB hakuna moto wowote uliofika bali masizi ya moshi wa moto huo.Na leo hakuna huduma zozote zile kutoka BRELA kwani HAWANA umeme!!Yaani na umuhimu wake wote eti BRELA wanasimama kufanya kazi kwa vile tu standby generator (hata ya kichina) haipo.Nimekuta pale watu wengi sana wako stranded hawajui biashara zo zitaenda vipi kwani BRELA pamefungwa.Just think ni mapato kiasi gani yanapotea leo hii kwa kufungwa kwa BRELA kwa "sababu zilizo(?) nje ya uwezo wao (ukosefu wa UMEME)!!!".
 
..moja ya sababu za moto kuwaka kwenye hilo jengo siku za nyuma ilikuwa ni hitilafu za umeme. nadhani hata safari hii inaweza kuwa hivyo.

..hilo jengo ni la zamani na install zake za umeme inabidi zifanyiwe uangalizi kama zinafaa. ama sivyo kuna siku litashika moto lote!
 
Nimepokea taarifa kuwa Ofisi za Brela zilizopo Dar zimeungua moto. Wenye taarifa zaidi kuhusiana na suala hili tunaomba watujulishe pamoja na extent of damage.

BASI ITABIDI WACHOME OFISINYINGI SANA TUU.....
 
..sahihi kabisa!

..na haukuenea sehemu nyingine. kwahiyo BRELA haijaungua na itakuwa vizuri watu wakiacha ku-speculate kuhusu brela na hujuma dhidi yake!

Nashukuru kwa kututoa wasiwasi, lakini usiwalaumu sana wale unaosema wana - speculate kwani nchi hii ambayo viongozi wake ni mafisi mafisadi lolote lawezekana ili kupoteza ushahidi, kwani wameshashtuka japo kwa mbali kuwa WTZ hawaukubali ukondoo.
 
Jana usiku nilikuwa natizama channel 10 na walikuwa wanaleta live moto uliokuwa ukiwaka kwenye jengo la Ushirika pale Lumumba Street Dar. Kwa kuwa naishi maeneo ya karibu na hapo nikaamuwa kwenda kujionea live. Nilipofika hapo nilikuta kweli kuna moto mkubwa kwenye hilo Jengo kwa upande wa kushoto (ukiwa lumumba unalitazama hilo jengo) na moto ulikuwa unawaka chini na magari mengi ya zimamoto yalikuwepo hapo na ulinzi mkali wa askari na silaha ulikuwepo hapo. Nilichoshuhudia mimi kwa macho yangu ni kuwa moto ulikuwa ukiwaka upande wa kushoto, chini, na si upande wa kulia juu ambapo ndio ninavyohamu kuwa zipo ofisi za brela. Sikukaa sana, kwa hiyo sijuwi kama waliweza kuudhibiti huo moto usiendelee kufika upande wa kulia wa jengo na kuwa umefika kuunguza ofisi za brela. Mimi nilopokuwepo hapo, hata ile bank ya CRDB iliyopo chini ilionekana kuwa haijashika moto kwa wakati huo. Ilikuwa majira ya saa saba na nusu za usiku na nilikuwa hapo mpaka saa nane za usiku.

Wamechoma moto ofisi hizo ili kupoteza ushahidi kuhusiana na makampuni fake ya kifisadi akina ANBEN, KAGODA n.k. Maskini Tanzania inasikitisha sana inafisadiwa kila kona tena na wale wale tuliowamini na kuwapa nafasi za uongozi kumbe ni mafisadi tu!
 
Mbona hamsomi vizuri post yangu "sijaona" ofisi za brela kuungua, upande wa jumba ulipounguwa hauhusiani na brella kabisa. Eeeh jamani someni post yangu vizuri. Na mchana huu nilipita tena hapo na kuhakikisha kuwa moto haujafika ofisi za brella, kulikoni jama?
 
Wamechoma moto ofisi hizo ili kupoteza ushahidi kuhusiana na makampuni fake ya kifisadi akina ANBEN, KAGODA n.k. Maskini Tanzania inasikitisha sana inafisadiwa kila kona tena na wale wale tuliowamini na kuwapa nafasi za uongozi kumbe ni mafisadi tu!

Mkuu heshima kwako,

hapo naomba kupishana na wewe kidogo.Sijui swala la kuchoma ofisi "kupoteza ushahidi" inaingia vipi hapa.Kwanza ieleweke kuwa limeungua JENGO LA USHIRIKA na sio OFISI ZA BRELA.Ila tu ni kuwa BRELA iko katika jengo hilo lakini katika wing tofauti ambako pia liko tawi la CRDB.Sasa inawezekani ni speculation ya wengi kuwa BRELA "imechomwa", kumbe sio.Hii imesababishwa na mleta taarifa hapa aliyepost mara ya kwanza kuwa ofisi za BRELA zimeungua,pili nafikiri ni ile habit ya muda mrefu ambapo baadhi ya majengo ambayo yamehusishwa na kashfa mbalimbali kuungua moto katika mazingira tata, mf. moto wa BoT 1980's, NASACO late 1990's,etc, na hivyo kuzua hisia kuwa kila moto uwakapo mahali fulani basi "ushahidi huwa unapotezwa".Na hii coincidentally hutokea katika ofisi za umma ambazo zimekumbwa na skandali kama hivi sasa BRELA.Ila kwa vile nilikuwapo na nimeshuhudia mwenyewe sehemu iluiyoingia nadhani ni mapema sana kusema kuwa BRELA "imeunguzwa kuficha ushahidi".Lets just wait and see and only time will tell...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom