'Moto wawababua' wezi wa fedha za wakulima wa ufuta wawafikia na kuwatesa wezi wa fedha za wakulima wa Korosho

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( TAKUKURU) mkoani Lindi imeanza kuwabana viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika ( AMCOS) ambao vyama vyao havijawalipa wakulima wa Korosho.
Budi alisema wakulima wa korosho ambao hawajalipwa fedha zao wameanza kujitokeza na kulalamika baada ya kusikia wakulima wenzao wa ufuta wanalipwa.

Kwani wanajitoza na kuomba walipwe malipo yao ya msimu wa 2017/ 2018.

Alisema kufuatia malalamiko hayo ya wakulima, taasisi hiyo ilianza zoezi la kuwakamata viongozi wa AMCOS ambazo hazijawalipa wakulima wa korosho waliopeleka kwenye vyama hivyo kuanzia msimu wa 2017/2018 kushuka chini ili wakulima hao walipwe kama wanavyolipwa wakulima wa ufuta.

'' Zoezi hilo lililoanza wiki moja iliyopita, tayari limeanza kuwa na mafanikio. Kwani viongozi sita wa vyama viwili wameanza kurejesha fedha. Moto tuliowasha hautazimika wala kupoa, walioiba wajiandae kurejesha. Sisi hatuhitaji maneno bali fedha za wakulima tu,'' alisema Budi.

Mkuu huyo wa TAKUKURU wa wilaya ya Nachingwea alivitaja vyama ambavyo wakulima tayari wamelalamika na viongozi wameanza kurejesha fedha kuwa ni Mchangani na NAMTAKANA.

Alisema chama cha msingi cha ushirika cha Mchangani kinadaiwa shilingi 9,499,524.00 na NAMTAKANA kinadaiwa shilingi 2,779,000.00.

''Baada ya kuwabana wameanza kurejesha. Viongozi wa Mchangani tayari wamerejesha shilingi 5,965,696.68 kati ya shilingi 9,499,524.00. Na viongozi wa chama cha NAMTAKANA wamezitema shilingi 794,000.00 kati 2,779,000.00. Wanaendelea kubanana wamalizie,'' Budi alisema Aliwahakikishia wakulima waliouza korosho zao kwenye vyama hivyo kwamba zoezi la kuwalipa litaanza jumatatu ya wiki ijayo.

Huku akitoa wito wakulima wa vyama vingine ambao hawajalipwa wapeleke nyaraka zinazothibitisha madai yao ili taasisi hiyo ikawakamate viongozi wake ili warejeshe.

Alionya kwamba viongozi wa AMCOS wasijaribu kuwaibia wakulima kuanzia wakati wa kupima mazao yao hadi malipo. Akiweka wazi kwamba mtendaji atakayekamatwa na mkulima anaiba wakati anapima mzigo wake kwenye mizani atambue kwamba anastahili kughulikiwa kama wezi wengine.

Alibainisha kwamba wanashughulika na viongozi wa vyama vinavyodaiwa na wakulima malipo ya msimu wa 2017\2018 na misimu mingine ya chini ya msimu huo. Kwani mchakato wa malipo ya msimu wa 2018\29 unaendelea ili wasiolipwa waweze kulipwa
 
Back
Top Bottom