Moto wateketeza jengo la makazi ya askari wa FFU mjini Moshi

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Moshi. Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika, unaendelea kuteketeza jengo la ghorofa mbili la makazi ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) la mjini Moshi usiku huu.

Vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Kiwanda cha Sukari cha TPC vilikuwa vikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.

Mashuhuda wameliambia gazeti hili kuwa moto huo umeanza saa 2: na hadi kufikia saa 4:00 ulikuwa umeteketeza ghorofa ya pili unakosadikiwa kuanzia.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa familia zote za askari wa kikosi hicho cha FFU wanaoishi katika nyumba hiyo wamefanikiwa kutoka salama isipokuwa baadhi ya mali zimeteketea.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia jitihada kubwa zikifanyika za kuuzima moto huo lakini unaonekana kuzidi kushika kasi baada ya gari la Halmashauri kuishiwa maji.

Hii ni mara ya pili kwa jengo hilo kuungua moto, miaka ya hivi karibuni lililipuka moto na vikosi vya zimamoto vilifanikiwa kuudhibiti.


Chanzo: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom