Moto wateketeza bweni Shule ya Sekondari Oljoro

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Bweni la wasichana la shule ya sekondari Oljoro namba tano iliyoko wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara limeteketea kwa moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana na kusababisha uharibifu wa miundombinu pamoja na vifaa vya wanafunzi.

F7597070-0EA0-41AF-A43C-41275860EA46.jpeg
 
Haya masuala ya Moto mashuleni yameanza kurudi kwa Kasi Sana miaka ya karibuni.

Hivi tatizo laweza kuwa Nini jamani?

Maana kipindi Fulani hapo Kati palitulia kabisaa.
 
Ni hujuma au ni nini kwenye hizi shule? Ni matumaini yangu hakuna vifo wala majeruhi!

Na sasa wazazu na mamlaka; shule za mabweni zianzie angalau kidato cha 1 au hata cha tano na vyuo huko. Wale wadogo tuwalee tu huku huku majumbani.
 
Nikikumbuka tuliwai organize mgomo tukapanga ety tuchome shule sijui tungefaidika nini ahahahah ..pole kwa uongozi wa shule nzima
 
This is to much aisee!!.
Hivi hakuna hata taskforce iliyoundwa kuchunguza majanga haya ya moto kwa shule za sekondari( bweni)!!?
 
Hata mimi nakumbuka aisee shuleni kwetu tuliorganize tuchome moto na petroli ilishapatikana lkn ikawa haina nguvu kila tukichoma inazimika

Wenye ilikuwa ifike saa mbili usiku ,,shule ianze kufuka moshi sema tuu mchana wake mkuu wa shule akatuliza amani ya shule
 
Duuh!! Huu moto sasa unatshia kwenye shule za bweni. Mbona siku zinavyozidi kwenda na kasi ya moto inazidi kuongezeka. Hatuna budi kumuomba Allah atuepueshe na haya majanga ya moto.
 
Back
Top Bottom