Moto wa teketeza maduka nane na baa katikati ya jiji ,vibaka kama kawa wagandamiza

Arusha Leo

Senior Member
Mar 12, 2012
122
72
MOTO mkubwa umezuka katikati ya jiji la Arusha na kuteketeza maduka nane ya wafanyabaishara pamoja na baa moja ya Pentagoni ambapo vitu vichache viliweza kuokolewa hukui idadi kubwa ya bidhaa zikiteketea kabisa .


Tukio hilo limetokea eneo la majengo katikati ya jiji,majira ya saa 7 mchana na kudumu kwa zaidi ya saa moja na nusu ukiwaka hadi majira ya saa 8.30 mchana,ambapo jitihada binafsi za wananchi wakishirikiana na magari ya zima moto walifanikiwa kuuzima .

Taarifa zauhakika ni kwamba mmiliki wa nyumba hiyo ambaye amejulikana kwa jina la ukoo wa Chonjo amelazwa katika hospitali ya Selian baada ya kuzimia alipopata taarifa kuwa nyumba yake imeteketea kwa moto



Moto huo unadaiwa kuzuka sehemu ya jikoni katika baa hiyo ya Pentagoni na kusambaa hadi kwenye duka moja la spare za magari na kusambaa kwenye maduka mengine yanayoizunguka baa hiyo ,Kutokana na ukubwa wamoto huo gari la zima moto la manispaa ya jiji la Arusha lilifika mapema,lakini lilishindwa kuudhibiti baada ya kuwa unawake kwa kasi kubwa na wingu la moshi mweusi kutanda angani.


Baadhi ya maduka aliyoungua na bidhaa zake kuteketea kabisa ni pamoja maduka ya nguo,duka la spare na bidhaa zote zilizokuwa kwenye baa ya pentagoni,hata hivyo polisi waliweza kuwahi eneo la tukio na kufanikiwa kudhibiti vitendo vya wizi japo vibaka waliojifanya kuokoa waliweza kupora baadhi ya bidhaaa


Aidha umati mkubwa wa wananchi waliofika katika la eneo la tukio walilalamikia magari ya zima moto yaliyofika bila maji na kuondoka hatua ambayo iliwalazimu wananchi kuyapopoa kwa mawe na jitihada za wanachi ndizo zilifanikiwa kuzima moto huo.


Wananchgi hao waliokuwa wakiimba peoples powers walionekana kukerwa na hatua ya gari la zima moto la manispaa kuingia kwa mbwembwe huku likiwa halina maji ndipo wananchi hao walipoanza kulifukuza na kurushia vitu vigumu ,ambapo dereva aliondoka kwa kasi kuepusha kipigo.


Hata hivyo msikiti wa Ahamadia ambao upo mkabakana na eneo la baa iliyokuwa ikiungua,ulinusurika baada ya wananchi kupanda juu ya paa na kuanza kungóa mabati yanayounganisha kuta za msikiti huo pamoja na baa hiyo.


Kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha Akili Mpwapwa alithibitisha kutokea kwa kukio hilo na kudai kuwa polisi bado inafanya uchunguzi wa chanzo cha tukio hilo pamoja na thamani ya vitu vilivyoteketea ,na kwamba hakuna madhara ya mtu kujeruhiwa na moto huo.

Mwisho.
 
source plse yz taarifa uliyoitoa.

Moto ulianzia duka la spare na siyo jikoni kama unavyosema. Mwenye nyumba huyo sijui Chonjo unayemsema mbona hajalazwa hospitali yeyote kama unavyodai yupo na jana alikuwa anakagua jengo lake lililoungua. Msilete taarifa za uongo hapa. We are great thinkers jamani mnatuaharibia JF yetu. Source mimi mwenyewe nilikuwepo tena nilikuwa nimeenda kununua uniform katika moja ya maduka hayo yaliyoungua.
 
hapakuwa na vibaka, km kuna vilivyoibwa bi vichache sana majirani walishiriki saidia kwa kujipanga na kutengeneza km njia ktk ya watu ambapo vitu vilipitishwa hadi maduka ya upande wa pili
 
source plse yz taarifa uliyoitoa.

Moto ulianzia duka la spare na siyo jikoni kama unavyosema. Mwenye nyumba huyo sijui Chonjo unayemsema mbona hajalazwa hospitali yeyote kama unavyodai yupo na jana alikuwa anakagua jengo lake lililoungua. Msilete taarifa za uongo hapa. We are great thinkers jamani mnatuaharibia JF yetu. Source mimi mwenyewe nilikuwepo tena nilikuwa nimeenda kununua uniform katika moja ya maduka hayo yaliyoungua.

Hiki ndo kinanishangaza sana huku kwa great thinkers. Mtu anakurupuka tu na kusema uongo. Huyo Chonjo mbona ni Uncle wetu? na siku hiyo tulikuwa na naye kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Hata hospital kupima presure tu hajaenda. Sasa hizi habari amezipata wapi? Aisee kama kitu hujui usiandike coz unailet down jamii forum
 
Acha uongo. Source yako plz? Alilazwa wodi namba ngapi? Aisee huku ni kwa ma great thinkesr na si kwa great gossipers. Habari hizi ni za uongo kabisa. Nyumba yes imeungua, vibaka yes walikuwepo but walikuwa wakichukua vitu vidogo vidogo baada ya wenye maduka kuhamisha mali zao. But mwenye nayo hakulazwa na pia hakuanguka.
 
Back
Top Bottom