Moto wa posho mbili wahamia kwa mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto wa posho mbili wahamia kwa mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bambumbile, Nov 16, 2009.

 1. b

  bambumbile Senior Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moto wa posho mbili wahamia kwa mawaziri
  Waandishi Wetu


  WAKATI vuguvugu la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) la kuwahoji wabunge kwa tuhuma za kupokea posho mbili kwa kazi moja halijatulia, uchunguzi huo sasa unahamia kwa mawaziri na watendaji wakuu wa serikali, imeelezwa.


  Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa kwa sasa Takukuru inafanya utafiti maalum kubaini tatizo hilo kabla uchunguzi kamili kuanza.

  Mpango huo umeanza ikiwa ni majuma kadhaa tangu wabunge warushiane maneno na Takukuru kupinga uchunguzi dhidi ya tuhuma kuwa wamekuwa wakipokea malipo mara mbili kwa kufanya kazi moja.


  Posho za kwanza ni zile ambazo hulipwa na Ofisi ya Bunge wakati wabunge wanapokwenda kufanya kazi kwenye mashirika na taasisi zilizo chini ya kamati zao, wakati posho nyingine hupokea wanapofika kufanya kazi hizo.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya Takukuru zimeeleza kuwa taasisi hiyo sasa inakusudia kufanya uchunguzi huo kwa mawaziri.


  "Mpango huo upo lakini haujaanza rasmi. Kinachofanyika kwanza ni kufanya utafiti wa kina kuwabaini wahusika kabla ya kuwafanyia mahojiano," alidokeza mmoja wa maafisa wa taasisi hiyo nyeti kwa utawala bora ambaye hakutaka kutajwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa Takukuru.


  Kwa mujibu wa afisa huyo, uchunguzi huo unakusudia kuwagusa mawaziri wa Serikali ya Muungano na watendaji wakuu wa wizara zao ambao ni manaibu waziri na makatibu wa wizara.


  Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo alisema jana kuwa suala hilo linahitaji utafiti kwanza ili kuona kama kweli tatizo la watendaji hao kuchukua posho mbili lipo au la.


  Luhanjo alifafanua kwamba asingependa kusema chochote sasa kuhusu suala hilo kwani kufanya hivyo ni kuvuruga mpango huo na kuwachanganya watendaji hao na wananchi kwa ujumla.

  "Suala lenyewe bado halijafanyiwa utafiti naomba tuachane nalo kwanza ili tusiwachanganye wananchi," alisema Luhanjo.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa masuala ya uchunguzi yana mamlaka zake.

  "Unajua uchunguzi wa kitu chochote kile serikalini una taasisi zake. Taasisi hizo siziagizi mimi kufanya uchunguzi ila zenyewe hufanya zinapoona kuna haja," alisema Waiziri Simba.


  Simba, ambaye alikaririwa kutaja baadhi ya wabunge waliohojiwa na Takukuru wakati akitetea uchunguzi dhidi ya malipo ya posho mbili kwenye mkutano wa Kamati ya Mwinyi mjini Dodoma, alisema masuala ya uchunguzi hayapaswi kuingiliwa na mamlaka nyingine, ikiwamo vyombo vya habari.

  "Sio kama sijawahi kusikia taarifa hizo, ila masuala ya uchunguzi hayapaswi kuingiliwa na magazeti, Nyie mna mipaka yenu katika kazi," aliongeza Waziri Simba.


  Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alikataa kuzungumzia taarifa hizo juzi.

  "No comment no, no, no.. (sina cha kusema, hapana, hapana, hapana)," alijibu kwa kifupi.


  Suala hilo la wabunge kuchunguzwa kwa kulipwa posho mbili kwa kazi moja liliamsha mjadala mkubwa kutokana na baadhi ya wabunge kudai kuwa Takukuru inaendesha mpango huo kutokana na wao kushinikiza serikali imuwajibishe mkurugenzi wa taasisi hiyo, ikiwa ni moja ya maazimio ya Bunge dhidi ya kashfa ya Richmond.


  Tayari mmbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ameshaeleza bayana kuwa hatakubali kuhojiwa kwa kuwa hajaona kosa lake na kwamba suala hilo linaendeshwa sasa kutokana na moto wa Richmond.


  Hata hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema uchunguzi huo hautasitishwa kwa sababu ni maagizo ya Ofisi ya Rais, huku Waziri Simba akisema kuwa Ofisi ya Bunge ndiyo iliyoomba kufanyika kwa uchunguzi huo.


  Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mawaziri kuchunguzwa tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, mara ya kwanza ikiwa ni uchunguzi kuhusu mali wanazomiliki.


  Novemba 15 2007 mkurugenzi wa uchunguzi wa Takukuru, Dk Vincent Kihiyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa mawaziri na manaibu ni miongoni mwa zaidi ya vigogo 100 waliokuwa wanachunguzwa kuhusu umiliki wa mali.


  Alisema hatua ya kuchunguza vigogo hao ni dalili kwamba taasisi hiyo haichunguzi rushwa ndogo tu kama baadhi ya watu wanavyodhani.


  "Tunachunguza rushwa za aina zote, sio ndogo tu kama wanavyofikiri baadhi ya watu," alisema Dk Kihiyo kwenye mkutano wa mwaka wa Shirika la Kusaidia Maendeleo la Ujerumani (DED), jijini Dar es Salaam jana.


  Alisema kuchunguzwa kwa vigogo hao ni matokeo ya ushirikiano mzuri ambao Takukuru imekuwa ikipewa kutoka kwa baadhi ya wasamaria wema ambao huwasilisha taarifa za siri kuhusu watu hao.


  "Kuna watu wengi hutupatia taarifa kwa hutupigia simu, wengine huenda kwenye ofisi zetu zilizo katika wilaya na mikoa yote nchini, ikiwa ni pamoja na kuacha nyaraka," alisema.


  "Tunawashukuru sana wote wanaowasaidia. Kwa ujumla mwamko wa jamii katika kupambana na rushwa umeongezeka kwa kasi na hii ni kwa sababu ya elimu wanayopewa kwa njia mbalimbali na serikali kwa ujumla,"alisema. Habari hii imeandaliwa na Salim Said na Patrica Kimelemeta
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kumbe uchunguzi ambao Bunge lenyewe liliwaandikia TAKUKURU barua ili walichunguze haukuwalenga "wapiganaji" pekee, na sasa unaelekea kwenye mhimili mwingine wa nchi? Wasiwasi wangu ni kwamba hakuna atakayepona kama alivyodai Waziri Sophia Simba kwamba CCM haina aliye safi!
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Suala la integrity lazima lipewe kipaumbele na Taasisi zote ikiwemo Takukuru yenyewe. Na imefika wakati sasa we have to put in place proper mechanism za kuzuia matatizo ya aina hii yasitokee in future.Tukiyaacha kama yalivyo ndio mwanzo wa kuchochea watu kupewa posho za seminar wazizohudhuria
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Unamaanisha kuwe na TAKUKURU-A kuichunguza TAKUKURU-B and vice versa? Kaazi kweli kweli!
   
 5. E

  Engineer JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wale wanaodanganya wameenda kutibiwa Ujerumani huku wamejifungia kwenye mahekalu yao Kunduchi waki chat JF nao wachunguzwe na mamilioni waliyolipwa kwa safari na matibabu hewa warudishe.

  Kuna wizi wa ajabu ajabu sana Tanzania. Eti spika wa bunge tukufu anaruhusu wizi wa namna hiyo kwa wapambe wake? Kweli hilo lichama halina mtu safi hata mmoja.

  Kuna wabunge kibao hawahudhurii vikao kwasababu ambazo sio za msingi na bado wanalipwa posho.

  Lazima nchi itengeneze kanuni zingine za maadili na tuhakikishe zinafuatwa.

  Hata huyo rais na msafara wake wachunguzwe mbona wanachukua pesa nyingi zaidi ya zile wanazotumia? Mbona wanalipiwa malazi hata wakati malazi yameshalipiwa na taasisi nyingine?

  TAKUKURU kuweni ngangari tu na hawa viongozi mafisadi wetu.
   
Loading...