Moto wa Mageuzi Tanzania Umejengwa na Walimu wanasiasa Wametia Kimea togwa likawa Pombe Kali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto wa Mageuzi Tanzania Umejengwa na Walimu wanasiasa Wametia Kimea togwa likawa Pombe Kali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, May 9, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Kwa walio wengi vuguvugu la mageuzi ya mfumo na siasa Tanzania unaonekana kuanzishwa na wanasiasa. Ukweli ni kwamba, walimu wa vyuo vikuu na vile vya elimu ndio haswa wajenzi wa fikra mpya za kutaka mageuzi ya kisiasa nchini.

  Kwa muda mrefu wahadhili wa vyuo vikuu wametumika kupanda fikra mpya kwa wanachuo wao. Hawa wanachuo ambao walisoma ualimu waliendeleza fikra hizo katika vyuo vya elimu na wale wa sekondari na taasisi mbalimbali za elimu wameendeleza fikra hizo kwa wanafunzi wao. Hivyo utaona kwamba, kuanzia miaka ya 2000 vijana ndio wamekuwa mstari wa mbele kujadili mustakabali wa taifa lao kimfumo na kisiasa.

  Jambo hili linajionesha sana katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ambako walimu wamekuwa wakiamsha fikra mpya na mitazomo hasi dhidi ya serikali na chama chake. Ugumu wa maisha na hali mbaya ya walimu imechochea walimu hawa kupandikiza kwa bidii fikra mpya ndani ya vichwa vya wanafunzi wao.

  Vile vile, mwenendo wa Jeshi la Polisi, Makama na Huduma za Afya kutoridhisha kumewafanya vijana waanze kuangalia njia mbadala ya kusafisha ama kuziadhibu taasisi hizi. mathalan, leo hii ukiwauliza vijana mtazamo wao juu ya polisi, wataishia ama kunung'unika ama kuwalaani polisi. Imefika mahali taarifa za jeshi la polisi haziaminiki kabisa kila zinapotolewa kutaarifu mafanikio ya jeshi hilo kupambana na uharifu. Mara kadhaa utawasikia vijana wakibeza taarifa hizo.

  Aidha, ugumu wa maisha na mfumuko wa bei; pengo kubwa kati ya masikini na matajiri umetumiwa na walimu kufafanua na kusisitiza mageuzi nchini. Watanzania wamezidi kuwa masikini wa kutupwa huku nchi yao ikiwa ni ya 16 duniani kwa utajiri wa raslimali; ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vya wanyama na mbuga asilia; ni ya pekee duniani kwa kuwa na madini ya tanzanite na wanyama wasiokuwepo mahala pengine pote duniani.

  Pia, wanasiasa matata kama C. Mtikira chama cha CHADEMA; taasisi na asasi zisizo za kiserikali kama hakielimu; viongozi wa dini; vyombo vya habari nao wamesaidia mno kuchochea wimbi hili la mageuzi.

  Hatimaye, ni uchovu wa hisia kwa watanzania waliowengi juu ya kusikia wimbo 'CCM' toka enzi hizo hadi leo hii wanapokuwa watu wazima. Pia, majina yale yale ya viongozi toka zama zile za Chama chajenga nchi hadi sasa nguvu mpya ari mpya. Uchovu umekuwa mkubwa mno, jamii ya waliowengi wanataka mageuzi.

  Kwa hiyo, itaonekana kwamba walimu wamekuwa mstari wa mbele kuchochea mageuzi nchini huku wanasiasa wakitia kimea na amira kuchachua fikra mpya kutaka mabadiliko. Na upepo huu hauwezi kuzimwa kupitia vyombo vya dola wala usalama wa nchi ni upepo unaovuma kuanzia ndani ya vichwa vya wanazuoni na wasomi wa sasa. KAZI KWELI KWELI!
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, nakubaliana na wewe kabisa, yakuwa vuguvugu la mageuzi makubwa ya kisiasa, walimu na wahadhiri ndiyo chachu.

  Ila bahati mbaya Serikali ya CCM bado inalidharau kundi hili.

  Hongera waalimu. Nathamini sana mchango wenu. Kipindi cha dakika 80, dakika 10 - 20 lazima muiponde CCM na Serikali yake. Mbegu hiyo haipotei bure.
   
Loading...