Moto wa Katiba mpya Unapagawisha

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,827
Moto wa katiba mpya unawahusu moja kwa moja watawala na watawaliwa. Unahusu haki na usawa wa watu.

Moto huu unahusu utawala bora na mamlaka kwa wananchi.

Moto huu ndiyo ulio pelekea Mh. Mbowe kukaa korokoroni kwa miezi 8. Mbowe ametoka na kazi inapoendelea kupagawa kupo pale pale.

IMG_20220329_083042_871.jpg

Kwamba inajulikana kuwa Mukandala na watawala wameleta maamuzi kinyemela kuwa katiba mpya iwe baada ya 2025?

Huu si mwendelezo ule ule wa kupagawa?

Chadema, CUF, NCCR na wote tuitakiao mema nchi hii, huu na uwe muda mahsusi wa kuunganisha nguvu.

Tuweke pembeni tofauti zetu tupate katiba mpya kwanza.

Katiba mpya ni sasa.
 
Chadema ni chama cha Michango

Wale wenzao ni chama cha Michongo!
Heri kuwa chama cha michango kinachosimamia na kutetea haki za wananchi na upatikanaji wa katiba ya wananchi kuliko kuwa chama kinacho ua wananchi kila chaguzi, chama kisichothamini haki za msingi za wananchi wake
 
Ukawa wa ki aina ingetufaa sana kuipata katiba mpya asubuhi asubuhi na jamii hii ya akina Kingai ikapumzishwa wanakostahili to stay.
 
Back
Top Bottom