Moto wa Katiba Mpya CHADEMA kutinga Ikulu; KAMATI Kuu yateua kamati ndogo ya muafaka

Ndg J umemtengenezea Mh Rais majibu, je akiwauliza wajumbe wetu maswali yafuatayo majibu yake wanayo? 1: Ujumbe wenu unawakilisha pande zote mbili za Muungano?2: Je Mabadiliko haya ni kwa upande mmoja tu wa muungano?3: Mbona muwakilishi kutoka visiwani simuoni hapa?4; Je Katiba hii ni ya CDM na CCm peke yetu? Vyama vingine vya upinzani wana wawakilishi hapa?5: Je, hii mihimili mitatu ya dola inaingiliana? 6;Kwa nini mawazo haya hamkuyawasilisha bungeni ambapo ninyi CDM mna kinga.
ATAWASIKILIZA LAKINI ATAWAPA HADIDU ZA KUFANYIA KAZI ILI AWEZE KUTEKELEZA MAHITAJI YAO.
Waende kwake kama umoja wenye pande mbili( linawezekana)
Waende kwa umoja wao kama wapinzani(sijui kama litakubalika CDM)
Je tutengue maamuzi ya wabunge kuupitisha muswada (usiangalie itikad
CDM wajiandae na majibu mengi zaidi ya wanavyodhani.

Hivi kweli ww upo tz? Maana cjaona hata swali 1 hapo, inavooneka ww hata hiyo kamati ya chadema huijiwi kamati ina viongoz kutoka pande zote. Hivi ww hukuona maoni ya chadema yaliyowakilishwa bungeni na TINDU LISU, na spika akasema hayo ni mawazo ya LISU?. Hembu jipange upya
 
Mkuu hapo penye red ndo pamenifanya nichangie kwenye hii thread ambayo ni crap tupu.
Nakushauri, kwakuwa kamati bado haijaenda kwa Kikwete, nenda pale Makao makuu ya CDM kamwambie Mbowe kuwa unampendekeza Mama yako awepo kwenye hiyo team.
So mama yake akakidhi hobbies za mkuu wa kaya?
 
haya ni maongezi ya wanaume kwa wanaume, au pale ikulu rais anajinsia a na b
haya majibu mepesi mnayotoa sio ya viongozi wenu. haijatulia. mnakwenda kujadili muswada ambao mnadai unawajumuisha watanzania, basi mngechanganya jinsia kidogo. Nadhani Bi mdogo halima pale alistahili au chiku abwao , emancipation of women in class struglle is must. mmeshachanganya madawa
 
Muafaka wenye nia ya kuvunja sheria hautakubalika kamwe. Hawa walipoteza nafasi ya kuujadili muswada. Ulipofikia sasa hawana uwezo wa kutia mkono kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
 
Muafaka wenye nia ya kuvunja sheria hautakubalika kamwe. Hawa walipoteza nafasi ya kuujadili muswada. Ulipofikia sasa hawana uwezo wa kutia mkono kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Hii move inavunja sheria kivipi?
 
Sasa mbona mkali kwani mama yako siyo wa kike au hujasomeka juu ukitaka wanawake nao wawepo kwenye kamati hiyo.....
mama yake sio mwana siasa wala member wa cdm. tuwape heshima akina mama wapeni heshima zao. msiwadhalilishe kiasi hicho. mamaoko angekuwa hakutaki wewe uje duniani asingempa babayako unyumba wake, hata kama angempa angekwepesha tarehe zake hata kama ingeingia angeweza kuitoa ukafia mbali nyani dume.
 
Watu wamechaguliwa kwa uwezo wao na nia maalum. Kwanza Kikwete ili kukutana na hao wajumbe itabidi afikirie mara mbili mbili kwanza kwani hao ni watu wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja both kisiasa na kisheria.

Hao maprofessors wawili ni watu waliobebea kitaaluma kwenye mambo ya siasa na sheria
.
Prof Safari ni mwalimu wa masuala ya siasa lakini cio mwanasiasa. Pele alikuwa mchezaji mzuri wa football lakini hajawahi kufundisha mpira hata siku moja.

CUF alipigwa chini na mchumi. nawaombea kila laheri katika msafara wao. tatizo jopo halikuchanganya pande zote za muungano. italeta maswali mengi magumu japo majibu yake yatakuwa rahisi.
 
Ongeza na Saidi Arfi( Makamu Mwenyekiti CHADEMA bara), Freema Mbowe, Saidi Isa Mohamedi, Makamu Mwenyekiti Visiwani
majina niliyoyasikia ni haya hapa sita:
1; Mh Freeman Mbowe
2: Makamu Bara mzee said arfi
3; Katibu mkuu Dr W P Slaa
4: Mh Tundu Lisu
5: Prof M. Baregu
6: Prof safari.
makamu mwenyekiti T/zanzibar sikusikia kutajwa, labda nimekosea kuhesabu.
 
Nimesoma taarifa za Chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na JK na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa CDM walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa CHADEMA.

Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi. Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....

Kumbe Crucifix ni SHE!
 
Cracwise, kuna point ya kuzungumzika kwenye hoja yako, ila ondoa hiyo dhana ya uwepo wa mwanamke
kwenye kamati kwa ajili ya kukidhi hobbie ya Mkuu wa Kaya sababu japo unamaanisha kuwapigia chapuo
wanawake ila umewadhalilisha kwa kiwango cha juu sana. naomba uwe muungwana tafadhali
Mkuu mbona unanionea mimi sijaleta mada hii...soma vizuri.......
 
mama yake sio mwana siasa wala member wa cdm. tuwape heshima akina mama wapeni heshima zao. msiwadhalilishe kiasi hicho. mamaoko angekuwa hakutaki wewe uje duniani asingempa babayako unyumba wake, hata kama angempa angekwepesha tarehe zake hata kama ingeingia angeweza kuitoa ukafia mbali nyani dume.
Mkuu heshima kwako....Soma mwanzo mwisho kabla hujakurupuka kujibu.................
 
tatizo jopo halikuchanganya pande zote za muungano. italeta maswali mengi magumu japo majibu yake yatakuwa rahisi.

majina niliyoyasikia ni haya hapa sita:
1; Mh Freeman Mbowe
2:Makamu Bara mzee said arfi
3; Katibu mkuu Dr W P Slaa
4: Mh Tundu Lisu
5: Prof M. Baregu
6: Prof safari.
makamu mwenyekiti T/zanzibar sikusikia kutajwa, labda nimekosea kuhesabu.
Naomba ufafanuzi kwenye nyekudu hao watu sikutoka zanzibar....hata hivyo kamati ilikuwa haitafuti watu wa kwenda kunywa chai na Kikwete ilizingatia watu wanao weza kujenga hoja.....
 
Nimesoma taarifa za Chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na JK na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa CDM walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa CHADEMA.

Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi. Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....

Unaposema mwanamana japo mmoja tukuelewe nia yako ni ipi...sijawahi ona utumbo kama huu ulioandika hapa. CDM sio CCM inayofanya mambo kwa fasheni. Ndio nyinyi mliotuchagulia rais kwa sura, haya sasa anazeeka tumieni hiyo sura yake mfaidike. Total Rubbish, crap, utumbo, taka-ngumu, maneno ya saluni za hao hao kina mama!

Wakati wanaume wanajadili mambo ya maana kwa mustakabali wa Taifa wengine wanawaza dada zao watatongozwa na nani, kichefuchefu usiye na mfano

22 NOVEMBER 2011

*KAMATI Kuu yateua kamati ndogo ya muafaka
*Maandamano yawekwa kiporo kusubiri suluhu
*Mbowe: Hotuba ya rais imetusikitisha sana
*Wanaharakati Dar kutoa msimamo mzito leo

Na Benjamin Masese

Mwenyekiti wa Chadema Bw. Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu tamko la Chama hicho kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumweleza msimamo wa kupinga rasimu ya katiba.

SIKU tatu baada ya Bunge la Tanzania kupitisha muswada wa Sheria ya kuundwa Tume ya Kukusanya maoni kuhusu
Katiba Mpya, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kusitisha maandaano ya nchi nzima kuupinga kama ilivyoeleza awali.

Badala yake chama hicho kimetangaza nia ya kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete, ana kwa ana kujadili suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CHADEMA Bw.Freeman Mbowe, alisema baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kujdili suala hilo kwa undani wameazimia kuunda kamati ndogo itakayokutana na Rais Kikwete kushauriana ili kufikia muafaka.

"Kamati Kuu imekaa na kushauriana na kupendekezwa kuundwa kwa kamati ndogo ambayo itakutakuna na Rais Jakaya Kikwete, kushauriana na kuwasilisha mapendekezo yao ili kuafikiana kabla ya kuchukua uamuzi kwenda kwa wananchi na wanaharakati,"alisema Bw. Mbowe.

Majina ya wajumbe

Aliwataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni yeye mwenyewe, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibroad Slaa, Makamu Mwenyekiti Tanzania Visiwani Bw. Issa Ali Mohamed, Mbunge wa Mpanda Bw. Said Arfi, Profesa Abdala Kapala na Profesa Mwesiga Baregu.

Bw. Mbowe alisema tayari kamati hiyo ilianza kufanya mchakato wa kuonana na Rais Kikwete jana na kwamba iwapo hawatasikilizwa au kupokea ushauri na msimamo kwa kujadiliana wanaturudi mezani na kuamua rasmi kwenda kwa wananchi kueneza kile alichokiita kuwa ni sumu ya kupinga muswada huo.

Akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa wiki kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Mbowe alisema hawakubaliani na kauli kwamba CHADEMA iliahidi Katiba Mpya kwa siku 100.

"Chadema tunasikitika kuona rais na wabunge wanaendelea kupotosha umma katika suala hili. Tulisema kwamba tutaanzisha mchakato wa katiba mpya kabla ya siku 100 huu ndio usahihi.

"Suala la katiba mpya limetekwa na baadhi ya wanasiasa ambao hawajui ni fursa ya kila mtanzania, wapo wengine wanaona chadema inapinga kuwepo kwa katiba mpya, sisi tunahitaji sana na tunachokitaka wananchi washirikishwe na waamue wenyewe,"alisema Bw.Mbowe.

Alisema chama chake kimekipongeza chama cha NCCR Mageuzi kuungana nao kwa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa lengo la kupinga muswada wa Katiba Mpya huku akikiponda Chama cha Wananchi (CUF) na vingine ambavyo vilishiriki mjadala huo bungeni.

CHADEMA na Polisi

Katika hatua nyingine CHADEMA imetoa mwito kwa Jeshi la Polisi kuondoa pingamizi la kufanya maandanao na mikutano ya kisiasa mara moja kwa madai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuvinyika haki ya msingi vyama pamoja na wananchi kwa ujumla.

Bw. Mbowe alisema baada ya taarifa kutolewa na Jeshi la polisi walitii agizo hilo lakini wamestushwa na kauli ya Rais Kikwete kuwaagiza wabunge wa CCM kufika kwenye majimbo yao na kuzungumza na wananchi juu ya muswada wa Katiba Mpya.

Alidai iwapo wabunge watafanya mikutano na wananchi watakuwa wameanzisha ligi ya mikutano na maandamano na kuliomba jeshi la polisi kuondoa pingamizi hilo.

Sakata la Jairo

Akizungumzia suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, ambaye bunge liliazimia kuchukuliwa hatua Bw. Mbowe alisema msimamo wa chadema uko pale pale kama wabunge walivyopendekeza bungeni.

Alisema hakuna sababu yoyote ya Bw. Jairo, Waziri wa wizara hiyo Bw. William Ngeleja, Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, pamoja na watumishi wengine kuendelea kuwa watumishi wa umma na kwamba msimao wa CHADEMA ni kuona wakifukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Alisema hatua zisipochukuliwa mapema kabla ya bunge kuirejea Januari 31, mwakani hapatatosha kutokana na kile alichodai kuwa ni uzembe huku kukiwa na ushahidi wa ubadhirifu huo kufanywa kwa makusudi.

Kwa upande wake Dkt. Slaa pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tindu Lissu, walikituhumu CCM kwa maelezo kuwa kimetumia 'ujangili' kupitisha muswada wa katiba mpya usio na maslahi kwa wananchi.

Wakati huohuo wanaharakati mbalimbali wanatarajia kutoa tamko zito kuhusu Muswada huo leo Jijini Dar es Salaam huku kukiwa na taarifa kuwa kulikuwa na vikao vya hapa na pale vya jumuiya hizo chini ya Jukwa la Katiba tangu Ijumaa wiki iliyopita.

"Tutatoa tamko letu kesho (leo) ili wananchi watuelewe na wajue wazi msimamo wetu baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Kuundwa ya Katiba Mpya,"alisema mmoja wa mwanarakati ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji rasmi wa kundi hilo.

Awali katika mdahalo wao Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Jukwa la Katiba walitishia kuhamasisha wananchi kufanya maandamano ya nchi nzima yasiyokuwa na kikomo kupinga muswada huo kwa madai kuwa ulipaswa kusomwa mara ya kwanza bungeni na sio mara ya pili.

CHADEMA INAFANYA MAKOSA KWAKO M-KITI MBOWE.
Mpaka sasa mlikuwa mnafanya vizuri kwa maana mlikuwa mnacheza offensive na CCM walikuwa wanancheza defensive kwani ni
chama kimojatu kati hivi viwili ndio kilihaidi kuleta katiba mpya kabla ya uchaguzi kwahiyo ccm inacheza ngoma yenu kwa hivi sasa kwa kuweza kuwasukuma kwa kutumia political pressure ya nguvu na kuweza kukubalina nanyi.

kosa kubwa linalotokea hivi sasa ni kushindwa kutangaza phase ya pili ya mapambano kwa maana ya kuwaweka ccm katika angle mnayoitaka lazima kuweka option zote mezani na kuwaambia wazi CCM nini kitatokea kama wasipofanya yale mtakayojadiliana na JK bila hivyo hawawezi kusikia sasa ilibidi mpaka hivi sasa iwepo tarehe maalum ya execute second phase endapo mazungumzo yatashindika ili wananchi wajue ahead of time nini kinachoendelea ili wawe tayari na sio kila siku kuibuka na matangazo.

Pili chama hiki lazima kiendeshwe kwa uwazi muwaambie wananchi nini mnachoenda kujadiliana na JK ili wananchi wajue Rais amekataa kitu gani kilicholetwa mbele ili kuondoa upotoshaji utaotokea hapo baadaye.

Tatu inabidi muunganishe nguvu na wenzenu wengine weny mawazo yanayofanana ili muwe kitu kimoja na siku zote umoja ni ngivu na utengano ni udhaifu, jukwaa la katiba lometangaza maandamano jumamosi hii tarehe 26. wakati nyie mnampango wa kuonaana na rais mnawachanganya wananchi wale ambao wangelipenda kushiriki ktk maadamano hayo kwa kukosa mawasiliano kati yenu. kwahiyo lazima muwasiliane na DEUS KIBAMBA na vikundi vyote ili wote muwe na kauli moja yenye kueleweka na nguvu moja.
 
OOhoo, angalieni Nyie Cream ya CDM msiwekewe ile Polo ili m do Mwakyembe??

Wanaweza kuweka kwenye Viti au makochi mtakayokalia huko Ikulu!!

teh teh haha haaaaa

Nilikuwa natania tu
 
Maamuzi mazito kama haya ya 'MUSWADA WA MAKINDA' pindi yanapopitishwa kwa kuegemea tu hisia badala ya hoja huku msukumo wote unapogeuka kuwa ni kukomoa chama fulani hivi nchi basi hapo ndipo kuliko na mwanzo wa kupasuka kwa pachaka na hesabu kubwa za madhara kuliko faida.
 
BAADHI YA WAZEE WALIOWAHI KUVUMAA HUKO CCM WADAIWA KUKACHA VIKAO VYA NEC DODOMA BAADA YA KUNUSA HARUFU ZA FEDHA HEWANI NA POTEZESHA DIRA MKUTANO MZIMA NA VILE VILE 'MUSWADA WA MAKINDA' KUONEKANA SUBILI

Eti mkutano wa CCM Dodoma; hakuna kitu pale na ni bure kabisa!!! Swala lote la gamba kuvuka limegoma mara baada ya kuloweshwa na utitiri wa vijisenti na kuwa ngumu na kunata zaidi mwilini. Hiyo ndio maana baadhi ya wazee wa chama hicho wakaamua kujitunzia heshma zao mbali yale yanayoendelea huko.

Kuna ugomvi mkali mno wa makundiunaoendelea ndani CCM hadi dakika hii lakini yote yanaendelea hivi sasa nyuma ya pazia.

Nasema ugomvi hatari ya kuwahi kutokea CCM unaendelea kupamba moto hadi kakika hii tunavyoendelea kuandika humu.

HAKUNA tena mwenye ubavu wa kufungia paka fisadi kengele baada wale wazee wenyewe kusikia ukigeugeu na unafiki kutoka Magogoni hdi wakaamu kujiweka kando na mkutano wa NEC CCM kule Daodoma ambao kwa maelezo yao ni kwamba hauna dira.

Vile vile kuna taarifa kwamba nako nyumbani kwa wana CUF nako si shwari kote Bara na Visiwani kutokana na uamuzi wao kuunga mkono muswada uliowaondolea kabisa matumaini wananchi wa pande zote mbili.

Kama mtu bado anasubiri zaidi moshi wa kijani na zambarau kuhusu BOMU linalowasubiri hadi hivi sasa basi kajikalie hapo. Mama Anna Makinda wabunge wa CUF huku Dodoma wamevimaliza kabisa hivi vyama viwili vya CCM na KAFU; hakuna tena kitu pale!

Mtoto tuliza boli; CHADEMA wanao mahesabu makali sana humu ili kusije kukatoka lawama baadaye kwamba hawakufanya mashauriano vya kutosha na CCM juu ya jambo hili ambalo tayari kwa KAFU na SISIEM zaidi ya sumu ya mamba hadi hivi sasa - jitulize kidogo mkuu, tuko pamoja??

Amini usiamini mwezi huo wa Decemba kuna mabadiliko mazito ajabu kutokea hadi kunakonusa pasaka mwakani, habari ndio hiyo!!

Back
Top Bottom