Moto wa Katiba Mpya CHADEMA kutinga Ikulu; KAMATI Kuu yateua kamati ndogo ya muafaka

Hapa nina suala kidogo.

Si ni hao hao chadema walimkimbia pale alipokwenda kulifungua Bunge kwa kutoka nje kwa maana kuwa hawamtambui?
Kama kikwete hana hofu ni kwa nini muda wote anapenda kukutana na SHIBUDA kwanini sio CUF,NCCR, au hata CCM???
Wewe unatoka safari baadala ya kumukumbuka mtotowako unamkumbuka mtoto wa jirani !!!!
Hapo kuna nini??

CCM wanahaha kununua Wabunge wa CDM na sio CUF kwa nini??

Kama CCM ni imara kwa nini Kikwete amepiga marufuku Maandamano si ange acha aone kama Watanzania Wanampenda ???
Tuache Ushabiki wa kupewa fedha , tujenge nchi yetu !!!

hata kama Kaitiba ya Kikwete itapita kwa nguvu za dola , bado baada ya upinzani kuchukua nchi 2015 , Wananchi wataunda katiba mpya na Kikwete hatakuwa kwenye rekodi nzuri ya kuandaa katiba!!!

Tuache ushabiki katiba ndiyo inalinda akina JAIRO???

Kama kikwete hana hofu ni kwa nini muda wote anapenda kukutana na SHIBUDA kwanini sio CUF,NCCR, au hata CCM???
Wewe unatoka safari baadala ya kumukumbuka mtotowako unamkumbuka mtoto wa jirani !!!!
Hapo kuna nini??

CCM wanahaha kununua Wabunge wa CDM na sio CUF kwa nini??

Kama CCM ni imara kwa nini Kikwete amepiga marufuku Maandamano si ange acha aone kama Watanzania Wanampenda ???
Tuache Ushabiki wa kupewa fedha , tujenge nchi yetu !!!

hata kama Kaitiba ya Kikwete itapita kwa nguvu za dola , bado baada ya upinzani kuchukua nchi 2015 , Wananchi wataunda katiba mpya na Kikwete hatakuwa kwenye rekodi nzuri ya kuandaa katiba!!!

Tuache ushabiki katiba ndiyo inalinda akina JAIRO???
 
jk hawezi kukubali kukutana na mateja.
mdogo wake rostamu aziz kada wa ccmaitwaye assadi aziz amekatwa na 92.2kg za heron (madawa ya kulevya). sasa hapa tunaweza kujua mateja wapo wapi na wanatokana na nini!!!
 
Nimesoma taarifa za Chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na JK na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa CDM walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa CHADEMA.

Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi. Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....
 
Mpenı salamu huyu Wamagogonı kuwa asıendelee kuwakumbatıa Wazanzıbar, hatuna haja na Muungano ulıofınyangwafınyangwa.
Wazanzıbar kıla leo wanalıalıa ılhal wanajua kabısa Tanganyıka yetu ımemezwa na huu muungano, tıme ımefıka tunataka Katıba hıı ıtuoneshe Nchı yetu ya Tanganyıka regardless of the cost that wıll ıncur!
Na mwambıenı awe makını sana make suala la katıba sıo fundo la ndoa katı ya CCM na Utawala wa Taıfa letu, naamını muda wao wa kuendelea kuwepo madarakanı unahesabıka so wawe makını sana hawa magamba ısıjeıkala kwao kwa kutengeneza katıba yenye mlengo wa kukumbatıa Chama tawala.
Wajıulıze sıku nao wakıwa wapnzanı wakatı huo CDM/UDP/NCCR wapo madarakanı Je wataclaım katıba nyıngıne?
Tengenezenı Katıba yenye mashko kama ya USA ambayo nı nadra sana kufanyıwa revıew.
Mkulu kuwa makını sana na hılı na kama kwelı we nı mchaMungu hıı ndo tym ya wewe kuıshıka vzr tasbıh vıngınevyo ıtakuwa taqbır kwa wapıganıa mabadılıko wa Nchı hıı nıkıwemo na mımı!
Twendenı vıtanı!
 
nimesoma taarifa za chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na jk na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa cdm walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa cdm. Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi. Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....

wanawake wepi? Cjamuona bdo
 
Nimesoma taarifa za Chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na JK na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa CDM walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa CDM. Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi.

Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....
Usifananishe Mambo ya CCM ambao walimpata Anne Makinda kwa hoja mbovu kama hiyo na kumutupa Sitta!!!. Hapa ni CDM!!!!
 
Nimesoma taarifa za Chadema kuunda kamati ya kwenda kuonana na JK na kumpa maoni yao juu ya mchakato wa kupata katiba mpya. Nimeona majina yote ya vidume watupu nikajiuliza kama vimwana wa CDM walikosa sifa ya kujumuishwa au tu ndio mpangilio wa CDM. Kama kuna maudhui na mahitaji maalum kwa kundi la kina mama; basi kamati itakosa msemaji sahihi. Kisha nikakumbuka hobbie za mkuu wa kaya nikahisi ingekaa poa kama angejumuishwa mwanamama japo mmoja....
Mkuu hapo penye red ndo pamenifanya nichangie kwenye hii thread ambayo ni crap tupu.
Nakushauri, kwakuwa kamati bado haijaenda kwa Kikwete, nenda pale Makao makuu ya CDM kamwambie Mbowe kuwa unampendekeza Mama yako awepo kwenye hiyo team.
 
Hapo hawaendi kumwambia katiba mpya wanataka iweje,kiasi kwamba uwakilishi wa wanawake utakosa,ukisema wanawake je walemavu?kuna vipofu nk.hata hivyo hapo kwenye hiyo kamati ndogo kinachokwenda kuzungumzwa ni namna gani mswaada haukuzingatia maslahi ya wananchi wote,tatizo ni hiyo sheria
 
Uwepo wa mwanamke/wanawake kwenye hii team ni jambo zuri, lakini wanatakiwa wawepo kwa sababu ya jinsia yao au kwa sababu ya uwezo wao? Hatuwatendei haki wanawake kwa kwa kuwabeba kama 'hand bag' Tujenge utamaduni wa kuchagua watu kutokana na merits. Achilia mbalii Spika, wanawake wa Tanzania wana nafuu gani kwa kuwa na Waziri mwanamke Wizara ya 'wanawake na watoto'? Ndio, nimesema wizara ya wanawake na watoto.
 
Mkuu hapo penye red ndo pamenifanya nichangie kwenye hii thread ambayo ni crap tupu.
Nakushauri, kwakuwa kamati bado haijaenda kwa Kikwete, nenda pale Makao makuu ya CDM kamwambie Mbowe kuwa unampendekeza Mama yako awepo kwenye hiyo team.

Ni crap kwa mawazo yako duni na huko kwa Mbowe mtangulize kwanza mama yako na dada zako kama unadhani hii ni njia sahihi ya kurespond thread usiyoipenda.......
 
Pipijojo sijui nani anyway cha msingi ni post yako,Labda tu nikujuze ya kwamba kumuona raisi ni mtego kwenu ninyi msiojua,tena ni mtego mkubwa sana na kwa taarifa una pande mbili za matokeo mazuri kwa chadema1.

Hoja za msingi zitawasilishwa kwake ama akubali kutokusaini mswaada urudishwe ili ufanyiwe marekebisho2.

Akikataa yeye ndio shahidi wa kutokukubali muafaka utakaoletwa kwa majadiliano ambayo yatapelekea kuwa na katiba isiyo ya upande mmoja wa CCM na washirika wao CUF.

Hivyo akikataa ujue pia ya kwamba ndio kawaruhusu chadema kuandamana kwa kutumia nguvu ya umma.kwa lie kichwa ngumu utapbisha lakini subiri it is a matter of time
Ndg J umemtengenezea Mh Rais majibu, je akiwauliza wajumbe wetu maswali yafuatayo majibu yake wanayo? 1: Ujumbe wenu unawakilisha pande zote mbili za Muungano?2: Je Mabadiliko haya ni kwa upande mmoja tu wa muungano?3: Mbona muwakilishi kutoka visiwani simuoni hapa?4; Je Katiba hii ni ya CDM na CCm peke yetu? Vyama vingine vya upinzani wana wawakilishi hapa?5: Je, hii mihimili mitatu ya dola inaingiliana? 6;Kwa nini mawazo haya hamkuyawasilisha bungeni ambapo ninyi CDM mna kinga.
ATAWASIKILIZA LAKINI ATAWAPA HADIDU ZA KUFANYIA KAZI ILI AWEZE KUTEKELEZA MAHITAJI YAO.
Waende kwake kama umoja wenye pande mbili( linawezekana)
Waende kwa umoja wao kama wapinzani(sijui kama litakubalika CDM)
Je tutengue maamuzi ya wabunge kuupitisha muswada (usiangalie itikad
CDM wajiandae na majibu mengi zaidi ya wanavyodhani.
 
Sasa mbona mkali kwani mama yako siyo wa kike au hujasomeka juu ukitaka wanawake nao wawepo kwenye kamati hiyo.....
Ni crap kwa mawazo yako duni na huko kwa Mbowe mtangulize kwanza mama yako na dada zako kama unadhani hii ni njia sahihi ya kurespond thread usiyoipenda.......
 

22 NOVEMBER 2011

*KAMATI Kuu yateua kamati ndogo ya muafaka
*Maandamano yawekwa kiporo kusubiri suluhu
*Mbowe: Hotuba ya rais imetusikitisha sana
*Wanaharakati Dar kutoa msimamo mzito leo


Na Benjamin Masese
Mwenyekiti wa Chadema Bw. Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu tamko la Chama hicho kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumweleza msimamo wa kupinga rasimu ya katiba.

SIKU tatu baada ya Bunge la Tanzania kupitisha muswada wa Sheria ya kuundwa Tume ya Kukusanya maoni kuhusu
Katiba Mpya, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kusitisha maandaano ya nchi nzima kuupinga kama ilivyoeleza awali.

Badala yake chama hicho kimetangaza nia ya kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete, ana kwa ana kujadili suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CHADEMA Bw.Freeman Mbowe, alisema baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kujdili suala hilo kwa undani wameazimia kuunda kamati ndogo itakayokutana na Rais Kikwete kushauriana ili kufikia muafaka.

"Kamati Kuu imekaa na kushauriana na kupendekezwa kuundwa kwa kamati ndogo ambayo itakutakuna na Rais Jakaya Kikwete, kushauriana na kuwasilisha mapendekezo yao ili kuafikiana kabla ya kuchukua uamuzi kwenda kwa wananchi na wanaharakati,"alisema Bw. Mbowe.

Majina ya wajumbe


Aliwataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni yeye mwenyewe, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibroad Slaa, Makamu Mwenyekiti Tanzania Visiwani Bw. Issa Ali Mohamed, Mbunge wa Mpanda Bw. Said Arfi, Profesa Abdala Kapala na Profesa Mwesiga Baregu.

Bw. Mbowe alisema tayari kamati hiyo ilianza kufanya mchakato wa kuonana na Rais Kikwete jana na kwamba iwapo hawatasikilizwa au kupokea ushauri na msimamo kwa kujadiliana wanaturudi mezani na kuamua rasmi kwenda kwa wananchi kueneza kile alichokiita kuwa ni sumu ya kupinga muswada huo.

Akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa wiki kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Mbowe alisema hawakubaliani na kauli kwamba CHADEMA iliahidi Katiba Mpya kwa siku 100.

"Chadema tunasikitika kuona rais na wabunge wanaendelea kupotosha umma katika suala hili. Tulisema kwamba tutaanzisha mchakato wa katiba mpya kabla ya siku 100 huu ndio usahihi.

"Suala la katiba mpya limetekwa na baadhi ya wanasiasa ambao hawajui ni fursa ya kila mtanzania, wapo wengine wanaona chadema inapinga kuwepo kwa katiba mpya, sisi tunahitaji sana na tunachokitaka wananchi washirikishwe na waamue wenyewe,"alisema Bw.Mbowe.

Alisema chama chake kimekipongeza chama cha NCCR Mageuzi kuungana nao kwa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa lengo la kupinga muswada wa Katiba Mpya huku akikiponda Chama cha Wananchi (CUF) na vingine ambavyo vilishiriki mjadala huo bungeni.

CHADEMA na Polisi

Katika hatua nyingine CHADEMA imetoa mwito kwa Jeshi la Polisi kuondoa pingamizi la kufanya maandanao na mikutano ya kisiasa mara moja kwa madai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuvinyika haki ya msingi vyama pamoja na wananchi kwa ujumla.

Bw. Mbowe alisema baada ya taarifa kutolewa na Jeshi la polisi walitii agizo hilo lakini wamestushwa na kauli ya Rais Kikwete kuwaagiza wabunge wa CCM kufika kwenye majimbo yao na kuzungumza na wananchi juu ya muswada wa Katiba Mpya.

Alidai iwapo wabunge watafanya mikutano na wananchi watakuwa wameanzisha ligi ya mikutano na maandamano na kuliomba jeshi la polisi kuondoa pingamizi hilo.

Sakata la Jairo

Akizungumzia suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, ambaye bunge liliazimia kuchukuliwa hatua Bw. Mbowe alisema msimamo wa chadema uko pale pale kama wabunge walivyopendekeza bungeni.

Alisema hakuna sababu yoyote ya Bw. Jairo, Waziri wa wizara hiyo Bw. William Ngeleja, Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, pamoja na watumishi wengine kuendelea kuwa watumishi wa umma na kwamba msimao wa CHADEMA ni kuona wakifukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Alisema hatua zisipochukuliwa mapema kabla ya bunge kuirejea Januari 31, mwakani hapatatosha kutokana na kile alichodai kuwa ni uzembe huku kukiwa na ushahidi wa ubadhirifu huo kufanywa kwa makusudi.

Kwa upande wake Dkt. Slaa pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tindu Lissu, walikituhumu CCM kwa maelezo kuwa kimetumia 'ujangili' kupitisha muswada wa katiba mpya usio na maslahi kwa wananchi.

Wakati huohuo wanaharakati mbalimbali wanatarajia kutoa tamko zito kuhusu Muswada huo leo Jijini Dar es Salaam huku kukiwa na taarifa kuwa kulikuwa na vikao vya hapa na pale vya jumuiya hizo chini ya Jukwa la Katiba tangu Ijumaa wiki iliyopita.

"Tutatoa tamko letu kesho (leo) ili wananchi watuelewe na wajue wazi msimamo wetu baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Kuundwa ya Katiba Mpya,"alisema mmoja wa mwanarakati ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji rasmi wa kundi hilo.

Awali katika mdahalo wao Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Jukwa la Katiba walitishia kuhamasisha wananchi kufanya maandamano ya nchi nzima yasiyokuwa na kikomo kupinga muswada huo kwa madai kuwa ulipaswa kusomwa mara ya kwanza bungeni na sio mara ya pili.










 
Sasa mbona mkali kwani mama yako siyo wa kike au hujasomeka juu ukitaka wanawake nao wawepo kwenye kamati hiyo.....

Wewe unayedhani ni sahihi kumpelekea Mbowe mama yako endelea tu siwezi kukukataza, thread yangu inahusu kamati kutokuwa na mwanamama, kama una akili changia maudhui ya thread yangu na usianzishe mapya.
 
Chadema kuna wanawake wana uwezo mkubwa sana pengine kuliko hata wanaume wengi walioko pale chadema lakini cha kuangalia hapa je kulikuwa na ulazima wa wanawake kuwepo kwenye kamati hiyo....
Uwepo wa mwanamke/wanawake kwenye hii team ni jambo zuri, lakini wanatakiwa wawepo kwa sababu ya jinsia yao au kwa sababu ya uwezo wao? Hatuwatendei haki wanawake kwa kwa kuwabeba kama 'hand bag' Tujenge utamaduni wa kuchagua watu kutokana na merits. Achilia mbalii Spika, wanawake wa Tanzania wana nafuu gani kwa kuwa na Waziri mwanamke Wizara ya 'wanawake na watoto'? Ndio, nimesema wizara ya wanawake na watoto.
 
Back
Top Bottom