Moto wa CHADEMA wawastua Wabunge wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto wa CHADEMA wawastua Wabunge wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Aug 21, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,275
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Baada ya wabunge wa CCM kuona serikali imelala usingizi, na chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambaye ndiye rais, kinashabikia udhaifu wa serikali na chama kupoteza mvuto mbele ya wananchi, wameshtuka na kuanza kuishambulia serikali yao waziwazi, hasa baada ya kuona wabunge wa upinzani wanatoa hoja zinazogusa maisha ya wananchi wa kawaida.

  Kwanini mabadiliko haya yanatokea sasa.........baadhi ya wahadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wanatoa maoni yao.

  Dk Mohamedi Bakari-Mhadhiri Sayansi ya Siasa, UDSM

  Dk Benson Bana-Mhadhiri Sayansi ya Siasa, UDSM


  Profesa Gaudence Mpangala-
  Mhadhiri Sayansi ya Siasa, UDSM

  Richard Mbunda-Mhadhiri Sayansi ya Siasa, UDSM

  Augustine Mrema -Mbunge wa Vunjo Agustino Mrema -TLP)

  My Take:
  Miongoni mwa wabunge ambao wameonekana kuungana na wapinzani katika kutetea masilahi ya wananchi ni Deo Filikunjombe (Ludewa), Beatrice Shelukindo (Kilindi), Christopher ole Sendeka (Simanjiro), Dk. Khamis Kigwangalah (Nzega) na Kaika Telele (Ngorongoro).

  Hata hivyo, duru za siasa zinadai kwamba inawezekana mashambulizi ya wabunge hawa wa CCM ni kiinimacho cha kudhoofisha nguvu ya wapinzani, kama ilivyokuwa kwa waliojiita wapambanaji wa ufisadi, ambao miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu uliopita walitumika kupoka ajenda ya ufisadi kutoka kwa wapinzani, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili CCM iweze kuaminiwa tena na umma.

  Source: Gazeti la Mwananchi na Tanzania Daima.
   
 2. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Hata kama Magamba watajidai wameshtuka na kutaka kuonekana upande wa CDM a.k.a nguvu ya wananchi msijichanganye nao kwani watawapotezea ramani kwani lengo kuu lao ni kujidai wamezaliwa upya. Wengi wa wabunge wa CCM wanaojidai kuishupalia Serikali hawamaanishi bali wanaangalia upepo wa mabadiliko wa mwamko wa wananchi kujihakikishia mustakabali wa maisha yake ya kisiasa ifikapo 2015.

  CDM move on na msitoe silaha zote kwani hawa jamaa wamekuwa mafundi wa ku copy and paste strategies zenu na kuna uwezekana waka hadaa watu wakafikiri ni kitu halisi wanaona kumbe ndani ni kanyaboya. Andaeni makombora mapya kwani kazi iliyoko mbele yenu bado pevu na focus iwe kuyeyusha kabisa matumaini ya Magamba siyo tu ya kusimamisha mgombea 2015 bali pia kufisha matumaini ya kushinda.

  Tumieni strategies zitakazo waondolea credibility kwa wananchi na hivyo kuwafanya kila wanapokwenda wazomewe na kukata tamaa na mwishowe watabaki kulaumiana wao kwa wao, kusambaratika na kuangushwa kwa kishindwa hata kabla ya uchaguzi mkuu. Tumieni strategies zitakazowafanya wakate tamaa na kujiunga na CDM na hivyo kudhoofisha kabisa ngome dhaifu ya magamba.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wengine hao ni kweli wametambua tangu siku nyingi tu umuhimu na faida ya KUTETEA MASLAHI YETU badala ya kupoteza muda kutetea MASLAHI YA CHAMA cha siasa; ila huyo kwenye wino mwekundu hapo chini katutetea katika lipi tena Luteni mbona hivo??????????????

   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,353
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Cha msingi ni kwa kambi ya upinzani kuhahakikisha inendelea kuwa pro-active katika kila move!! Magamba wanafahamika kwa mbinu chafu, wanaweza waka-strategize vizuri wakaja kuwa-outsmart!!!

  Kza uzi, kazi bado ni ngumu!!!
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,940
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 180
  Unajua sisi wananchi wa kawaida hatujali nani anatuletea maendeleo awe CCM au CCJ hata wakiwa outsmart wabunge wa CDM ni sawa kama dhamira yao itakuwa ya kweli na sisi wananchi tutaona, binafsi nawapongeza wabunge wote wanaosimamia maslahi ya taifa bila kujali wanatoka chama gani sote tumeona kwenye bajeti ya Madini na Nishati ndio maana unaweza kunikuta leo nampongeza mzee Sitta kesho akibadilika na mimi nabadilika na kumponda vilevile.
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,564
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hao bado hawajajipambanua kama wana simamia maslahi ya chama ila wanasema wanasimamia maslahi ya wananchi so ku sum up kuwa ni wa ccm si sahihi kwani hata huko ccm wanaonekana wasaliti ila muondoe huyo KIGWANGALA haimuhusu na kwanza ni Kihiyo aliiba jina la mtu kusoma sec school
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 780
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM si wakuwaamini hata chembe.Ni vigeugeu wakubwa.
  Wachache wanaojifanya kutetea wananchi wanasoma tu uelekeo wa upepo.
  Binafsi siamini kama CCM wanaweza kufanya lolote kwa nia njema.
  Nataka kuona CCM ikizikwa na si vinginevyo.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wana-JF,

  hapo penye wino mwekundu panahitazi UPEMBUZI wa ndani zaidi na kutoa vyote vya uvunguni na kuviweka hadharani meza kuhusu huyu baba Daktari karubandika wa falsafa katika mchepuo usijulika kwa mtu yeyote.

  Hakika kuna haja kujadili kama kweli Kigwangala ni msomi kweli au ni Kihiyo mwingine tu ndani ya CCM; na endapo jibu ni hilo la mwisho basi tuone ya kwamba kwa hilo jamii ifanye nini hasa kuondokana na hawa watibu kichwa kwa ugonjwa wa goti.


   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  wabunge wa ccm ni km vinyonga sio wa kuwaamini kabisa! Naangalia aljazeera wakombozi wa libya wameikamata tripoli kilaini na watoto wawili wa gadafi mikononi mwa wakombozi bd hii serikali legelege pamoja na ridhiwani ukombozi waja
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,003
  Likes Received: 1,885
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi siwezi kuwaamini wazee wa MAGAMBA,hata wangetumia jiki kujisafisha hawawezi takata.
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  CDM Moto chini mpaka kieleweke, mna sapoti kubwa sana.
   
 12. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #12
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 3,810
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  Mkuu, nakubaliana nawe lakini hapo kwenye RED kuna tatizo, huyu kijana
  wa Mama Salma anauota uwaziri ndiyo maana misimamo yake ina utata sana...
   
 13. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  huyu KIGWANGALAH si ndo wa nzega 'MAKAMBA YUSUF' kamtoa wapi huyu sababu yeye ndo alimpiga chini "BASHA" akadai eti ni msomali alafu yule mzee kashawahi kutubu kuwa uzee unampelekesha. Sasa baada ya bashe akaja kigwangala tukaambiwa mara mrundi mara eeh kumbe kama mm std 7. Halafu ule usomali wa bashe umetoka wapi? Mbona wahindi na waarab hata kwa rangi wanaonekana lakini mnawachunia? HIVI MNAFIKILI WAHINDI WAMEWASAHAU MLIVYOWAFANYA KWENYE AZIMIO LENU LA A-TOWN HEE? Watakuja kuwafanyia kitu mbaya sana ndo mana hata dada zetu wa kazi wanakoma wana visasi hawa shauriyenu.
   
Loading...