Moto wa Chadema kuhamia Nyanda za Juu Kusini

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Chadema kimepanga kuanza kuanza ziara ya Operesheni Sangara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la April.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, amesema wabunge wote na viongozi wa juu wa chama hicho wataweka kambi mkoani Mbeya hivi karibuni kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha umma kujiunga na chama hicho.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano na mikutano hiyo mara itakapoanza, Operation hiyo itahusisha mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, na Rukwa.

Hii ni awamu ya pili ya mwendelezo wa Operation hiyo iliyobuniwa na chama hicho baada ya kupata mafanikio makubwa kwenye maandamano na mikutano iliyomalizika hivi karibuni katika kanda ya Ziwa ikihusisha mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera.

Naomba tuwaunge mkono kwa sababu madai wanayozungumzia karibu yanamgusa kila mtu, hata baadhi ya makada maarufu wa CCM akiwemo aliyekuwa waziri mkuu Fredrick Sumaye, Chrisant Mzindakaya na kada wa siku nyingi Balozi Paul Ndobho wameanza kukiona umuhimu wa harakati hizi za Chadema.

Naomba kuwasilisha.
 
Mbeya Mbona huko ndo ITAKUA chademe Tupu Tutakapofika mwaka 2015!

Mbeya City Stand up for your rights, Dont let em do what they have doing for the past 45 and above years
 
Dont let em do what they "have doing" for the past 45 and "above years"[/QUOTE]
Mkubwa lugha ya Watu hii.
 
This is a good initiative to that particular areas.
Kwenye msafara wa mamba kenge wamo "Jihadhali na Pro-Mubarak, Pro-Gaddafi na Pro-Kikwete"by Quinine
 
Nawaunga mkono Chadema kwa kuwa na nia ya dhati ya kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa wanyang'anyi. Mungu wabariki viongozi wote wa Chadema. Saa ya ukombozi ni sasa
 
We are ready to sacrifice our souls, our children and our families so as not to give up our beloved country Tanganyika. We say this so no one will think that ccm is capable of breaking the will of the country with its weapons.
 
Chadema, we are with yu kuleta mabadiriko chanya. Let's us fight for our generation to come. We can do it. Keep it up. Mbeya mjitokeze kwa wingi jamani.
 
mpaka kitaeleweka tu....
 

Attachments

  • EDmkwara[1].jpg
    EDmkwara[1].jpg
    31.5 KB · Views: 43
Duh! Nina-imagine hapo Mbeya Mjini itakavyokuwa, na akiwepo Mh Sugu - natumai wazee wa intelenjensia hawataleta upupu.
 
Hii ndo kanda ingine muhimu kwa CDM ili kufanikisha ushindi 2015. Zingine ni Kaskazini, Ziwa. Naomba CDM wasisahau kupita kwa Spika wa Bunge kumwaga sera. Tuone kama ataomba kufuta kauli.
 
Back
Top Bottom