Moto Ulioua 43 Kwenye Harusi Kuwait Ulitokana na Wivu wa Kimapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto Ulioua 43 Kwenye Harusi Kuwait Ulitokana na Wivu wa Kimapenzi

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Aug 19, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mabaki ya vitu vilivyoteketea na moto huo Tuesday, August 18, 2009 7:59 AM
  Moto uliozuka kwenye harusi nchini Kuwait na kuua watu 43, ulianzishwa na mke wa zamani wa bwana harusi ambaye alitaka kulipa kisasi kwa kuachwa. Mke huyo wa zamani wa bwana harusi, alikiri kuanzisha moto huo kwenye hema ambalo sherehe ya harusi kwaajili ya wanawake ilikuwa ikifanyika.

  Gazeti la Al-Qabas la nchini humo lilisema kwamba mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23 aliwaambia polisi kwamba alilimwagia petroli hema hilo la harusi kabla ya kulipiga moto ili kulipa kisasi kwa mumewe kwa kumfanyia madhila mengi kabla kumpa talaka.

  Bi harusi ambaye alikuwemo kwenye hema hilo, alinusurika kufariki lakini mama yake na dada yake walifariki kwa kuteketea kwa moto.

  Likimnukuu mwanamke mmoja mfanyakazi wa ndani toka nchi za Asia, gazeti la Al-Qabas lilisema kwamba mfanyakazi huyo wa ndani alimuona mwanamke huyo akilimwagia petroli hema hilo la harusi kwaajili ya wanawake kabla ya moto mkubwa sana kuzuka kuliteketeza hema hilo ndani ya dakika chache.

  Jumla ya watu 43 wanawake na watoto wamefariki hadi sasa huku watu wengine 90 walijeruhiwa katika moto huo ambao uliteketeza kila kitu ndani ya dakika zisizozidi 10.

  Mwaka jana, wanawake wawili walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tukio linalofanana na hili lililotokea kwenye mji wa Jahra uliopo kilomita 50 magharibi mwa mji mkuu wa Kuwait.

  Sherehe nyingi za harusi katika nchi hiyo ya ukanda wa ghuba hufanyika kwenye mahema huku wanawake na wanaume wakitenganishwa na kufanya sherehe tofauti.

  Mkuu wa zimamoto wa Kuwait alisema kwamba maiti nyingi kutokana na moto huo zilikuwa zimeungua vibaya sana kiasi cha kushindwa kutambulika huku maafisa wa Kuwait wakitumia vipimo vya DNA kuzitambua maiti hizo.

  Maiti 16 zilizikwa jumapili huku maafisa wa Kuwait wakiendelea na vipimo vya kuzitambua maiti zilizobakia. Zaidi ya watoto saba walifariki kwenye moto huo.

  Katika majeruhi 90 wa moto huo, watano wako mahututi kutokana na kuunguzwa vibaya sana na moto huo.

  Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2843802&&Cat=2
   
Loading...