Moto Ndani ya CC: Mbowe azuiwa ku-chair kikao!

Kwanza kikao kilichelewa kuanza kwasababu Mwenyekiti alichelewa kuwasili. Kimeanza. Watu wa upande wa Zitto wameomba Mwenyekiti Mbowe asiwe mwenyekiti wa kikao kwasababu ameonyesha dhahiri kwamba hayupo neutral. Makamu wa Mwenyekiti ndiye Mwenyekiti wa kikao hadi sasa. Nitawaletea habari kadri ninavyotumiwa text kutoka ndani ya kikao.

Shetani wenu.

Ujue njia ya mwongo ni fupi!

Mbowe alichelewa kufika, alifika kikao kimeisha pita hoja ya Zitto, iweje tena Wamkatalie kuwa mwenyekeiti wa kikao ambacho hakuwepo kwanza? na pili alikuwa hajafika hata kutoa maoni yake wakajua yuko upande gani?

Shetani wewe shindwa kabisa!
 
SHEttani....

taratibu ndugu,ina maana MBOWE anataka kupokonywa CHAMma na DOGO ZITTO ZUBEIR KABWE? duh hiyo itakuwa ya FUNGA MWAKA 2007.

Mmh nyie wakali kwa kuchombeza tu vitu vya kuchonganisha sio mchezo, lakini hiyo style ya kiwazi hivyo cheap sana yaani kila mtu anawashtukia mnataka kuchonganisha.
 
mwenyekiti babaako ..hii ni post yako ya nane ..haya yote yanatoka wapi????..au kwa ajili unaingia na MULTIPLE NAMES..

SON OF A.. YAANI MTU AKITOA MAONI LAZIMA AWE FULANI ... hata akiwa mlalajoi wa kawaida....

anyway tunajua wengi hapa mnafalipwa pesa ili kupost humu...lakini wengi tuliobaki tunapost kwa mapenzi ya nchi yetu...hatulipwi!!!!

mzee mwanakijiji, hamna msaada wa ushauri!! hawa vijana wamemshika pabaya mkuu. Pole mzee, ndio siasa za kwenye blogu hizo!!!!
 
Afadhali Mbowe amekuwa mkweli kwa kusema kile ambacho kila mwenye akili atimamu anajua kwamba kulikuwa na mgongano wa mawazo juu ya hili kwenye uongozi wa CHADEMA. Wengine tunaamini migongano hiyo ya mawazo ni jambo jema na kichocheo cha maendeleo kama inakuwa haiishii kuleta chaos. Hongera CHADEMA kwa kumaliza mkutano wenu salama.

Wingu la Zitto bado

na Irene Mark

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa baadhi ya wajumbe aliowateua katika kamati aliyoiunda kupitia sheria za madini aliyoitangaza Novemba 13, mwaka huu.
Matakwa hayo ya chama hicho cha upinzani ambacho kina mjumbe katika kamati hiyo, yalitangazwa jijini Dar es Salaam jana.

Akisoma tamko la chama hicho, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kuwaondoa watu hao katika kamati hiyo kwa sababu hawana sifa.

Alisema baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, mbali na kuwa watumishi wa serikali, pia wanahusika kwa namna moja ama nyingine katika kuishauri serikali na kuingia kwenye mikataba ya madini ambayo sasa inaligharimu taifa.

Mbowe aliwataja wajumbe hao kuwa ni Maria Kejo, ambaye ni Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Mkaguzi wa Hesabu kutoka Kampuni ya kimataifa ya Ukaguzi wa Hesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo.

Wajumbe wengine ni Peter Machunde kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), ambaye hata hivyo imeelezwa kuwa tayari ameshatangaza kujitoa katika kamati hiyo. Mwingine ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange.

Mbowe alisema kuwa iwapo Rais Kikwete atashindwa kufanya mabadiliko hayo, upo uwezekano mkubwa wa matokeo ya kamati hiyo kukataliwa, si na vyama vya siasa tu, bali pia na wananchi.

Mbowe alikuwa akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho kuhusu mwenendo wa wajumbe wa kamati hiyo, baada ya mzozo wa siku kadhaa uliokiandama chama hicho kwa madai ya kupinga uwepo wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Katika tamko hilo, Mbowe alikiri kuwapo kwa mgongano wa mawazo miongoni mwa viongozi wa CHADEMA kuhusu uwepo wa Zitto kwenye kamati na kusisitiza kuwa hayo ni maoni ya watu binafsi.

Pamoja na tamko hilo, CHADEMA ilimruhusu Zitto kuendelea kuwemo kwenye kamati kwa sharti la kujiondoa wakati wowote endapo mambo hayatakuwa shwari kwenye kamati hiyo.

Aidha, CHADEMA imeahidi kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo yenye wajumbe 12 chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani, huku ikisisitiza uwepo wa watu kutoka maeneo mengine ili kuongeza wigo wa uwakilishi.

Aidha, chama hicho kilichopo ndani ya ushirika wa vyama vingine vitatu vya upinzani, kimemtaka Rais Kikwete kurekebisha hadidu za rejea kwa kuongeza baadhi ya vipengele kwa masilahi ya wananchi wanaoishi jirani na migodi.

Chama hicho kinataka kamati ya madini kujadili tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na uchafuzi wa mazingira kwenye makazi ya watu jirani na migodi mikubwa ya madini.

Aidha, wameitaka kamati kujadili tuhuma za ufisadi na rushwa zinazohusu uandaaji na upitishwaji wa mikataba ya madini kati ya serikali na kampuni binafsi, pia mchango wa sekta ya madini kwa uchumi na maendeleo ya wananchi jirani na machimbo.

Kwa upande mwingine, CHADEMA imemtaka rais kuweka hadharani taarifa za kamati nne za madini zilizotangulia kabla ya kuanza kazi kwa kamati hii, ambayo kwa kiasi kikubwa imehusisha watumishi wa serikali na wanasiasa.

Akizitaja kamati za madini ambazo baada ya kazi waliyopewa taarifa zake zinaendelea kuwa siri ni kamati ya Jenerali Mboma ya mwaka 2001 na ile ya Brigedia Mang’enya ya mwaka 2003.

Kamati nyingine iliundwa mwaka 2004 chini ya uenyekiti wa Dk. Kipokola na ile ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Lawrenve Masha, ya mwaka jana. Kamati zote ziliundwa kwa kipindi cha miaka mitano bila matokeo yake kuwekwa wazi hadi sasa.

CHADEMA imemtaka Rais Kikwete kuahidi kuwa baada ya kamati hii kumaliza kazi yake, matokeo yatatangazwa hadharani ili kuondoa dhana ya matumizi mabaya ya fedha za umma kwa wajumbe wa kamati hizo.

“Zimeundwa kamati nne ndani ya miaka mitano, huu ni ufujaji wa fedha za wananchi…mbaya zaidi matokeo ya kamati hizo yanafungiwa kwenye makabati na kubaki kuwa siri.

“Tunataka kuona tofauti ya kamati hii na zilizopita, rais asifunike kombe ili mwanaharamu apite, kwa sababu tulilipigia kelele jambo hili…tunakubali kuwa watch dogs (mbwa walinzi), kazi yetu ni kubweka tu, lakini tunaamini hali itabadilika,” alisisitiza Mbowe.

Aidha, alitumia muda huo kuvionya baadhi ya vyombo vya habari vinavyopotosha umma kuhusu suala la kamati hiyo na uwepo wa Zitto kwa lengo la kuharibu kambi ya upinzani.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Ushirika wa vyama vya upinzani, Augustine Mrema (TLP), alisema umoja huo unamshauri Rais Kikwete kuunda tume huru kama alivyoahidi kutokana na ukweli kuwa kazi ya tume na kamati ni tofauti.

Aidha, ushirika huo uliunga mkono maazimio ya kamati kuu ya CHADEMA iliyokaa juzi na kumtaka Zitto kufanya kazi ndani ya kamati hiyo kwa uadilifu na kupokea ushauri wa kambi ya upinzani.

Katika kamati hiyo, yumo pia Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige, Dk. Harrison Mwakyembe, kutoka Kyela (CCM), John Cheyo (UDP) na mwanasiasa mkongwe, Iddi Simba.

Wengine ni Kamishna wa Sera katika Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa.

Hadidu za rejea za kamati hiyo inayotarajia kutoa ratiba ya shughuli zake leo, zinaonyesha kuwa itapitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo.

Aidha, kamati itapitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, itachambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na serikali na pia itakutana na ‘Chamber of Minerals’ na wadau wengine na kutoa mapendekezo kwa serikali.
 
Ujue njia ya mwongo ni fupi!

Mbowe alichelewa kufika, alifika kikao kimeisha pita hoja ya Zitto, iweje tena Wamkatalie kuwa mwenyekeiti wa kikao ambacho hakuwepo kwanza? na pili alikuwa hajafika hata kutoa maoni yake wakajua yuko upande gani?

Shetani wewe shindwa kabisa!

mbona unatoboa povu la waaminio kwa urahisi?
 
Afadhali Mbowe amekuwa mkweli kwa kusema kile ambacho kila mwenye akili atimamu anajua kwamba kulikuwa na mgongano wa mawazo juu ya hili kwenye uongozi wa CHADEMA. Wengine tunaamini migongano hiyo ya mawazo ni jambo jema na kichocheo cha maendeleo kama inakuwa haiishii kuleta chaos. Hongera CHADEMA kwa kumaliza mkutano wenu salama.
Hili ni Jambo jema badala ya kuongea unafiki wakati mambo yanaonekana... tunaomba utulivu uendelee ili nchi hii tuweze kuijenga!
 
CHADEMA wanastahili pongezi kwa kuonyesha ukomavu katika kupambanisha hoja hadi kufikia uamuzi walioutoa. Sasa hilo limekwisha na "SHETANI" umeshindwa sasa lete lingine kama kawaida yako.
 
Afadhali Mbowe amekuwa mkweli kwa kusema kile ambacho kila mwenye akili atimamu anajua kwamba kulikuwa na mgongano wa mawazo juu ya hili kwenye uongozi wa CHADEMA. Wengine tunaamini migongano hiyo ya mawazo ni jambo jema na kichocheo cha maendeleo kama inakuwa haiishii kuleta chaos. Hongera CHADEMA kwa kumaliza mkutano wenu salama.

Wingu la Zitto bado

na Irene Mark

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa baadhi ya wajumbe aliowateua katika kamati aliyoiunda kupitia sheria za madini aliyoitangaza Novemba 13, mwaka huu.
Matakwa hayo ya chama hicho cha upinzani ambacho kina mjumbe katika kamati hiyo, yalitangazwa jijini Dar es Salaam jana.

Akisoma tamko la chama hicho, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kuwaondoa watu hao katika kamati hiyo kwa sababu hawana sifa.

Alisema baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, mbali na kuwa watumishi wa serikali, pia wanahusika kwa namna moja ama nyingine katika kuishauri serikali na kuingia kwenye mikataba ya madini ambayo sasa inaligharimu taifa.

Mbowe aliwataja wajumbe hao kuwa ni Maria Kejo, ambaye ni Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Mkaguzi wa Hesabu kutoka Kampuni ya kimataifa ya Ukaguzi wa Hesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo.

Wajumbe wengine ni Peter Machunde kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), ambaye hata hivyo imeelezwa kuwa tayari ameshatangaza kujitoa katika kamati hiyo. Mwingine ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange.

Mbowe alisema kuwa iwapo Rais Kikwete atashindwa kufanya mabadiliko hayo, upo uwezekano mkubwa wa matokeo ya kamati hiyo kukataliwa, si na vyama vya siasa tu, bali pia na wananchi.

Mbowe alikuwa akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho kuhusu mwenendo wa wajumbe wa kamati hiyo, baada ya mzozo wa siku kadhaa uliokiandama chama hicho kwa madai ya kupinga uwepo wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Katika tamko hilo, Mbowe alikiri kuwapo kwa mgongano wa mawazo miongoni mwa viongozi wa CHADEMA kuhusu uwepo wa Zitto kwenye kamati na kusisitiza kuwa hayo ni maoni ya watu binafsi.

Pamoja na tamko hilo, CHADEMA ilimruhusu Zitto kuendelea kuwemo kwenye kamati kwa sharti la kujiondoa wakati wowote endapo mambo hayatakuwa shwari kwenye kamati hiyo.

Aidha, CHADEMA imeahidi kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo yenye wajumbe 12 chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani, huku ikisisitiza uwepo wa watu kutoka maeneo mengine ili kuongeza wigo wa uwakilishi.

Aidha, chama hicho kilichopo ndani ya ushirika wa vyama vingine vitatu vya upinzani, kimemtaka Rais Kikwete kurekebisha hadidu za rejea kwa kuongeza baadhi ya vipengele kwa masilahi ya wananchi wanaoishi jirani na migodi.

Chama hicho kinataka kamati ya madini kujadili tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na uchafuzi wa mazingira kwenye makazi ya watu jirani na migodi mikubwa ya madini.

Aidha, wameitaka kamati kujadili tuhuma za ufisadi na rushwa zinazohusu uandaaji na upitishwaji wa mikataba ya madini kati ya serikali na kampuni binafsi, pia mchango wa sekta ya madini kwa uchumi na maendeleo ya wananchi jirani na machimbo.

Kwa upande mwingine, CHADEMA imemtaka rais kuweka hadharani taarifa za kamati nne za madini zilizotangulia kabla ya kuanza kazi kwa kamati hii, ambayo kwa kiasi kikubwa imehusisha watumishi wa serikali na wanasiasa.

Akizitaja kamati za madini ambazo baada ya kazi waliyopewa taarifa zake zinaendelea kuwa siri ni kamati ya Jenerali Mboma ya mwaka 2001 na ile ya Brigedia Mang'enya ya mwaka 2003.

Kamati nyingine iliundwa mwaka 2004 chini ya uenyekiti wa Dk. Kipokola na ile ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Lawrenve Masha, ya mwaka jana. Kamati zote ziliundwa kwa kipindi cha miaka mitano bila matokeo yake kuwekwa wazi hadi sasa.

CHADEMA imemtaka Rais Kikwete kuahidi kuwa baada ya kamati hii kumaliza kazi yake, matokeo yatatangazwa hadharani ili kuondoa dhana ya matumizi mabaya ya fedha za umma kwa wajumbe wa kamati hizo.

"Zimeundwa kamati nne ndani ya miaka mitano, huu ni ufujaji wa fedha za wananchi…mbaya zaidi matokeo ya kamati hizo yanafungiwa kwenye makabati na kubaki kuwa siri.

"Tunataka kuona tofauti ya kamati hii na zilizopita, rais asifunike kombe ili mwanaharamu apite, kwa sababu tulilipigia kelele jambo hili…tunakubali kuwa watch dogs (mbwa walinzi), kazi yetu ni kubweka tu, lakini tunaamini hali itabadilika," alisisitiza Mbowe.

Aidha, alitumia muda huo kuvionya baadhi ya vyombo vya habari vinavyopotosha umma kuhusu suala la kamati hiyo na uwepo wa Zitto kwa lengo la kuharibu kambi ya upinzani.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Ushirika wa vyama vya upinzani, Augustine Mrema (TLP), alisema umoja huo unamshauri Rais Kikwete kuunda tume huru kama alivyoahidi kutokana na ukweli kuwa kazi ya tume na kamati ni tofauti.

Aidha, ushirika huo uliunga mkono maazimio ya kamati kuu ya CHADEMA iliyokaa juzi na kumtaka Zitto kufanya kazi ndani ya kamati hiyo kwa uadilifu na kupokea ushauri wa kambi ya upinzani.

Katika kamati hiyo, yumo pia Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige, Dk. Harrison Mwakyembe, kutoka Kyela (CCM), John Cheyo (UDP) na mwanasiasa mkongwe, Iddi Simba.

Wengine ni Kamishna wa Sera katika Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa.

Hadidu za rejea za kamati hiyo inayotarajia kutoa ratiba ya shughuli zake leo, zinaonyesha kuwa itapitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo.

Aidha, kamati itapitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, itachambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na serikali na pia itakutana na ‘Chamber of Minerals' na wadau wengine na kutoa mapendekezo kwa serikali.
HII NI KWA KADA!
Kada hili ndio tamko la CHADEMA,na kama ukisoma kwa makini utangundua kwamba hawa watu wako pamoja licha ya kwamba kuna migongano ya kimawazo.Ndiyo demokrasia hiyo.Kila mtu anakubali Zitto aende kutoa mchango wake kwa manufaa ya nchi,lakini pointi walizoibua kikaoni si kwasababu Zitto kateuliwa kwenye kamati bali wanakamati wengine,pamoja na madhumuni ya kamati hiyo.If you're thinking is too shallow like you've already proven..then unaweza kupata shida kuilielewa hili.Mwanakijiji amekusomesha wee..! lakini ni wazi sikio la kufa halisikii dawa.Inawezekana mapenzi yako ama chuki zako vikapelekea wewe kuwa "branded" tofauti na ukweli.Tofauti na KADA halisi alivyo.Kwa mfano mimi kufikiri kuwa your thoughts were too shallow,ama pia kudhani kwamba wewe ni mpotoshaji uliopandikizwa,ama kujipandikiza mwenyewe kutokana na mapenzi yako binafsiUkweli ni kwamba hukujizatiti vya kutosha kabla ya kuibua hizo pointi zako rojo rojo kwamba Mbowe amekasirishwa na uteuzi wa Zitto.Zitto ni kijana wa CHADEMA,hivyo wanachadema wote,na sio Mbowe peke yake wako concerned na muenendo wake wa kisiasa kwasababu ofcourse utawa affect CHADEMA na upinzani kwa ujumla!Kama alivyosema Mbowe na Dk Slaa,hakuna anayetaka issue ya ufisadi ibadilike na kuwa issue ya kwanini Zitto yumo kamatini,kama nilivyotangulia kusema huko nyuma;"KARATA ALIYOICHEZA KIKWETE NI NZITO HIVYO NI VERY MUHIMU ISSUE HIZI ZIKAJADILIWA ILI MAMBO YASIENDE KAMA VILE AMBAVYO SOMEONE TAYARI AMESHATABIRI"Utabiri huo unaelekea kushindwa na ndio maana kuna watu kama"SHETANI"na "KADA WA CCM DHIDI YA UPINZANI"Ambao sasa wanataka kulazimishia mgawanyiko,hapo naona wamewahi mno,too early man..!wangesubiri kiduchu,sasa everybody knows that hii issue imesukwa?!mhn!Ama haiendi kama ilivyotabiriwa?Zitto naye inabidi aseme something,maana amekuwa kimya mno.Nauliza tena kabla hajaenda huko kamatini"TAFADHALI SANA AWE ANAJUA ANACHOKWENDA KUFANYA LASIVYO..I DONT KNOW!Yetu macho..!Wamepewa miezi mitatu nafikiri!Je pumba na chuya vitawekwa bayana?Naona tuendelee na mjadala then we'll find out!
 
Historia ni jambo jema na JF ndipo ulipo utajiri wa historia za siasa za Tanzania.....tulipofikia sometimes ni vizuri kuperuzi tulikotoka pengine tukajitafakari upya....kupitia michango ya wadau kwenye uzi huu unaweza kunyaka kitu japo kidogo..........tunaijenga Tanzania?..........:hail:
 
Mh mbowe yuko mikoani kuimarisha chama hao vinjanjaa kikao chao kimeratibiwa na ccm lkn wamechelewa.
 
Back
Top Bottom