Moto na maji ni vitu vyenye madhara majubwa katika jamii kama havijatumika vizuri.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Moto na maji ni vitu vizito sana, katika vitabu vitakatifu tunasoma kuwa Mwenyezi Mungu alitumia moto na maji kutoa adhabu kwa binadamu wasiomtii.

Moto ulitumika kuteketeza Sodoma Rutu alipona. Maji yalitumika kuleta gharika. Alipona Nuhu tu akiwa na familia yake kwenye safina.

Kuna mtu mzima mmoja aliniambia kuwa ukiota moto au maji itafakari ndoto yako, kuna ujumbe mzito Mwenyezi Mungu anakuletea kuhusiana na maisha yako.

Moto na maji ni vitu ambavyo tunavihitaji katika maisha ya kila siku. Lakini hitilafu ikitokea madhara yake ni makubwa sana.

Maoni yangu;
Watoto wafundishwe kanuni kuu za uokoaji wakati wa moto kuanzia darasa la tano. Askari wa zima moto wakushirikiana na wizara ya elimu wapite mashuleni angalau mara moja kwa muhula kutoa elimu.


Ikiwezekana wanafunzi wa shule za msingi wapewe msfunzo ya kuogelea kama sehemu ya curriculum itawasaidia kuokoa maisha yao na ya wengine.
 
Aliyepona kwenye gharika ya maji ni Nuhu, ni kweli kabisa elimu ya kupambana na majanga itolewe kwa watanzania hasa kwa kuanzia mashuleni na vyuo vyote
 
Back
Top Bottom