figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Familia kadhaa hazina mahali pa kuishi katika kata ya Serera wilaya ya Monduli baada ya moto kutelekeza nyumba walizokuwa wanaishi pamoja na maduka makubwa nane ya jumla hoteli na bar na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kwa wathirika wa tukio ilo.
Wakizungumza katika eneo la tukio mashuhuda na waathirika wa moto wamesema tukio ilo lilianza majira ya saa kumi na moja alfajiri na kwamba wamejitahidi kuuzima lakini juhudi zilishindikana kutoka na kukosa vifaa vya kuzima moto hivyo hakuna kilicho salimika na wengi wao wanadaiwa katika taasisi za fedha huku taarifa zisizo thibitishwa zinadai kuwa moto huo ulishababishwa na itilafu ya umeme.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli Isack Joseph amesema tukio ilo ni la pili kutokea wilaya humo katika kipindi kisicho zidi wiki mbili hivyo serikali inapaswa kuchunguza chanzo na kudhibiti ili kupunguza madhara wanayo yapata wananchi.
Akizungumza akiwa katika eneo la tukio mkuu wa wilaya ya Monduli Francis Miti amesema wilaya hiyo inakabiliwa na ukosefu wa magari ya zimamoto kwani inategemea gari moja tu ambalo ni la uwanja wa ndege wa manyara na hata hivyo gari ilo kwa sasa limeharibika.
Chanzo: ITV