Majoja
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 612
- 186
Tumeona janga lingine la moto kwenye soko la Sido Mwanjelwa Mbeya mjini. Kwenye luninga ITV jana jioni na leo asubuhi sote tumeona kilichotokea. Kilichonisikitisha sana ni kitendo cha askari aliyevaa kiraia akimrukia kwa teke la ninja mtuhumiwa ambaye tayari alikuwa amwekwa chini ya ulinzi. Mtuhumiwa huyu alikuwa amezungukwa na askari karibu wanne na mara kutoka kusiko julikana anatokea huyu askarai anamrukia mtuhumiwa.
Cha kusikitisha zaidi askari wengine badala ya kufuata sheria wanaingilia na kumpiga mtuhumiwa kwa mateke ngumi nakadhalika.
HILI NI KOSA LA JINAI. ITV inaoneka sehemu nyingi tu duniani na natumaini hata wakuu wa Polisi wameona hili. Hatua lazima zichukuliwe.
Naomba kutoa hoja.