Moto jirani na hosteli za UDSM wateketeza vibanda vya wafanyabiashara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeteketeza vibanda vya wafanyabiashara vilivyopo kando ya barabara ya kuelekea katika hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Moto huo ulianza leo Ijumaa Novemba 12,2021 saa 2 asubuhi lakini kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilifika eneo hilo kuzima moto huo.

MOTO CHUOPIC

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Khamis amesema moto umeanzia katika kibanda kimoja cha mama ntilie kabla ya kushika mabanda mengine.

"Banda lililokuwa likifuata ni la kuhifadhia magodoro, ulipoingia ndani ya kibanda hicho uliongezeka na kuwa mkubwa kabla ya kushika banda jingine la kuuza la mbao na kueleke sehemu ya kuosha magari," amesema Khamis.

MOTOOPICCCHUO

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Makaburi Kibangu, Moshi Khaftan amesema alipata taarifa ya moto huo ya saa moja na nusu asubuhi na kupiga simu Zimamoto.

#MWANANCHI
 
Wakati tunapeana pole ni na kutafuta chanzo, pia tuangalie wakati tunaweka vibanda na kufanya ujenzi kama tunatumia tahadhari ya kujikinga au kuepuka na madhara kama haya (Tanzania tuna Bahati) ila ukichunguza sana we are living dangerously...
 
Moto mkubwa umezuka leo Novemba 12,2021 saa moja asubuhi katika vibanda vya wafanyabiashara waliopo jirani na njia ya kuelekea hosteli za Mabibo Jijini Dar es Salaam na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara hao huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.

Chanzo: mwananchi_official

Lala salama Mkombozi wa Wamachinga.
 
Njia rahisi ya kuwafukuza wafanyabiashara hapo. Sasa wataambiwa wasubirie serikali iweke sawa miundombinu ndio imetoka hiyo. Tafuteni maeneo mbadala.
 
Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeteketeza vibanda vya wafanyabiashara vilivyopo kando ya barabara ya kuelekea katika hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Moto huo ulianza leo Ijumaa Novemba 12,2021 saa 2 asubuhi lakini kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilifika eneo hilo kuzima moto huo.

MOTO CHUOPIC

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Khamis amesema moto umeanzia katika kibanda kimoja cha mama ntilie kabla ya kushika mabanda mengine.

"Banda lililokuwa likifuata ni la kuhifadhia magodoro, ulipoingia ndani ya kibanda hicho uliongezeka na kuwa mkubwa kabla ya kushika banda jingine la kuuza la mbao na kueleke sehemu ya kuosha magari," amesema Khamis.

MOTOOPICCCHUO

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Makaburi Kibangu, Moshi Khaftan amesema alipata taarifa ya moto huo ya saa moja na nusu asubuhi na kupiga simu Zimamoto.

#MWANANCHI
Sabotage Plan.
 
Back
Top Bottom