Motivation thread ..weka inspiration story yako hapa ili vijana wenzako tujifunze

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
wakuu,habari nimeona nianzishe uzi huu maalumu kwa ajili ya kuwahamasisha vijana wa kitanzania kutokata tamaa ya kimaisha pamoja na magumu yanayotupitia ya kusaka chapaa,unaweza kuweka historia yako ulivyohangaika na maisha hadi ukafika hatua uliyofika hapo.

Kumbuka lengo ni kujifunza na kuimarishana katika kupambana na hali ngumu ya kimaisha

Mimi nakumbuka baada ya kumaliza chuo niliamua kutohangaika hata kidogo na suala la kutafuta ajira,nilijaribu biashara mbalimbali ikiwemo za kuuza mhindi na matunda ,lakini zote hizo sikuweza kuyamudu maisha

baada ya mwaka toka nianze harakati hizo,niliamua kufungua duka doko,yani kioksi cha kuuza vinywaji vikali na sigara,hasa sigara maana ndio lilikuwa lengo la kioksi hiko.

baada ya muda nikaanza kuona mafaniko yake kwani kwa mtaji wa laki 3 ndani ya miezi 9 hizi mtaji ulikuwa hadi milioni moja.

mbele ya kioksi nikaweka kijiwe cha kahawa,kwa hiyo nikawa navuta wazee ,wapenda mpira na wapenda siasa kuja kunywa kahawa lakini pia kikawa kama kijiwe chao cha kukutana na kadilishana mambo yao wanayoyashabikia,

kwa wakati huo niliajiri kijana mmoja ambaye tulikuwa tunasidiana,hadi kufikia hivi leo jumla ya mtaji wangu unafika zaidi ya milioni 7,kwani kioksi kimekuwa na kuwa min pub,kijiwe cha kahawa watu wamezidi kuongezeka kwani kwa siku naweza kuuza hadi kahawa ya laki mbili hadi tatu hii ni pamoja na kashata zake.

now nipo kwenye mpango wa kuanzisha kibanda cha chipsi karibu na pub yangu,

wengine karibuni
 
very inspirational.... hongera aiseee, hili game taiti sana, nimefaiti mno hadi sasa nimetulia kiasi japo malengo hayajatimia 100%, nipo kwenye 80% nikitulia ntaandika ushuhuda, vijana tupambane wakati tukiwa na nguvu..
 
very inspirational.... hongera aiseee, hili game taiti sana, nimefaiti mno hadi sasa nimetulia kiasi japo malengo hayajatimia 100%, nipo kwenye 80% nikitulia ntaandika ushuhuda, vijana tupambane wakati tukiwa na nguvu..
kweli mkuu
 
Hongera sana, siku zote mwanzo ni pagumu ila ukivumilia , unapenya .
Kila la kheri
 
Back
Top Bottom