Motion: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Motion: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Akili Unazo!, Jul 2, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,781
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280
  Wakuu leo katika kupitia maandishi ya gazeti la mwananchi nimekutana na kichwa cha habari kisemacho Wabunge wa viti maalum ni feki kikatiba hivyo waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera utaratibu wa bunge) Philip Marmo alisema utaratibu uemkua ukitolewa na CCM kama zawadi kwa wanawake hivyo anasema kama kuna uhitaji wa kuendeleza kutoa zawadi hizo bas litolewe pendekezo la kuingiza katika katiba.

  swali ni kwamba kwa miaka yote hii ya uhuru arobani na tano ni kweli kuna mambo serikalai yetu inafanya ambayo hayapo kikatiba?

  Wakuu nielimisheni maake mimi nilishakufaa siku nyingi ndo maana nataka urithi wangu wanipe niache kuona kinachoendelea.
   
 2. k

  kosamfe Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo tunavunja katiba? Kama tumefikia huko basi hali ni mbaya sana na hatuna watendaji wa kuwashauri kitaalamu wanasiasa wetu au wanasiasa wetu ni madikteta ambao hawakubali ushauri wa kitaalamu
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wamelifanya BUNGE letu kuwa kuubwa unnecessarily, mzigo mzito kwa walipa kodi wetu. Kazi yao kubwa kuunga mkono hoja.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pengine ndio maana post yako haileweki kumbe mtu mwenyewe ni mfu!
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Katiba hii hapa http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

  Katiba ya 1977 toleo la 2000

  SURA YA TATU


  BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

  SEHEMU YA PILI


  WABUNGE, WILAYA YA UCHAGUZI NA UCHAGUZI WA WABUNGE

  Wajumbe wa Bunge

  Wabunge

  Sheria ya 1984 Na.15 Ibara 13 sheria ya 1992 Na.4 Sheria 1992 Na.4 Ibara 18 Sheria ya 1995 Na.12 Ibara 9
  Sheria ya 2000 Na.3 ib.11

  66.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-
  (a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;
  (b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais, watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;

  (c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;
  (d) Mwanasheria Mkuu;
  (e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b)
  .
  (2) Rais na Makamu wa Rais kila mmojawao hatakuwa Mbunge.
  (3) Endapo Mkuu wa Mkoa atachaguliwa kuwa Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi au endapo Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi atateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Bunge litahesabiwa kuwa lina idadi ya Wabunge inayohitajika na shughuli zake zitakuwa halali ingawaje idadi ya jumla ya kawaida ya Wabunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, itakuwa imepungua kutokana na uchaguzi huo wa Mkuu wa
  Mkoa au uteuzi huo wa Mbunge anayewakilisha wilaya ya uchaguzi.
   
 6. N

  NAHUJA JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,020
  Likes Received: 15,585
  Trophy Points: 280

  Rest In peace ndugu yangu
   
 7. SHILINDE

  SHILINDE Member

  #7
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 23, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  [​IMG]

  Viti maalumu kwa tafsiri rahisi kabisa ni mpango mahsudi ambao unalenga kuwajengea uwezo kundi maalumu katika kushika nafasi mbalimbali katika ngazi ya maamuzi na uongozi.

  mpango huo unalenga sana katika kupunguza na kutokomeza dhana za ukandamizaji wa kijinsia na makundi maalumu kwa kuwapa fursa ya kupata nafasi za usawia katika maamuzi mbalimbali na uongozi.

  cha ajabu sasa tunawaona baadhi ya wawakilishi wetu kupitia viti maalumu wanaonekana kama hawajaielewa falsafa ya viti maalumu vizuri, maana mheshimiwa anapata fursa ya kuteuliwa mara ya kwanza….. tena kwa mara ya pili anapata bahati ya kuteuliwa tena….. lakini bado anakuwa hajajiamini na kujijengea dhana ya ushindani wajimbo. nilikuwa natoa tu kama angalizo kwamba inabidi serilikali iweke muda maalumu na kusiwe na firsa ya kujirudia mara mbili, na muwakilishi atayepata fursa ya kuteuliwa viti maalum afanyiwe majaribio baada ya kumaliza huo muda maalumu ili tuone kama dhana ya kmjenga katika kipindi alichopewa imemkaa?.

  sina maaana ya kuvipinga viti maalumu, lakini je tunawasaidia au ndio tunawafanya wabweteke, binafsi nampenda sana mama kilango kwa ushupavu wake, na ninatamani sana wanawake wote wawe na ujasiri kama mama yangu huyu.

  jamani viti maalumu ni chombo cha kutupa fursa na kujiandaa, sio tubaki hapo hapo. nimeshtushwa sana kusikia habari kuwa kuna mama yangu mwingine ambae nilikuwa nadhani na yeye atajitosa jimbo tena, sasa ametangaza kuwania apendekezwe viti maalumu…..??.

  [​IMG]

  Pamoja na kuangalia yote hayo, watanzania tujitathmini tangu tumeanzisha viti maalumu je lile lengo letu tunafanikiwa? je wawakilishi wa viti maalumu wanaelewa kwa nini wamepata fursa ya kuwawakilisha watu maalumu katika viti hivyo maalumu??
   

  Attached Files:

 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wanajamvi,

  Nimejaribu sana kuangalia na kutafakari sana mfumo wetu wa viti maalum... sijachukua reference ya nchi yoyote kwani sioni sababu na hasa ukizingatia kwamba our country is unique, blessed na inapitia kipindi kigumu cha mpito kwa kuondokana na dhana zama kwenda dhana halisia...

  Ukiangalia hata mchakato unaotumika, kwangu mimi naona unanyima nafasi baadhi ya makundi hasa walio weledi kupita, kuchakachuliwa hadi kupata nafasi... teh current system [regardless of chama] imekua ni ya kupigia kura watu kutokana na popularity katika vyama rather than qualities.... si chadema, KAFU wala CCM walio na chakato wa kuridhisha kupata hawa watu... here are my proposals

  1. tupunguze idadi ya wagomea wa viti maalu kufikia asilimia kumi tu ya wabunge WAKUCHAGULIWA, kupunguza cost...
  2. tubakize nafasi za upendeleo kwa walemamu tu... hakuna sababu ya kuwa na viti maalum ya wanawake kwani WANAWAKE WANANWEZA, NA WANWEZESHDWA SANA TU SASA
  3. Nafasi za viti maalum zichanganuliwe kwa mtindo wa profession [au nyanja muhimu] kama vile afya, elimu, ulinzi na usalama, kilimo, sheria, madini, nishati, misitu, habari nk... ili kuongeza changamoto na profeissionalism kwenye bunge letu... huwa napata tabu sana kumsikiliza mwana kwaya komba na kuamini kama anaweza kuelewa mfumo mzima wa afya au nishati
  4. Rais abaki na nafasi zake 10

  Nasema hivi kwasababu kubwa moja.... siku zote tangu nipate akili, nimekua nikisikia matatizo yasiyokwisha, mfano mimba za wanafunzi, MSD na tatizo la madawa, umeme na maji... naamini kabisa, kuongeza professionals kwenye bunge kutabadilisha mfumo wa vikao na kuleta tija zaidi....

  siwadharau wasio na elimu kubwa lakini wakati umefika kubadili jinsi nchi inavyoendeshwa... nina imani kwamba hata awe kikwete, lipumba, slaa, nk... wote wanahitaji technical inputs kupanga sheria zruzi na zinazotekelezeka

  NAWASILISHA
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  umetisha kaka!.....
  nimekubali sana.nitarudi sasa hivi
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,457
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Tuufutilie mbali kabisa.....hauna maana...kwani wapiga kura ni wanaume tu majimboni? takwimu zinasema wanaume ni wachache kuliko wanawake sasa hawa wanawake wanaogopa nini kwenda majimboni?
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Quoted as a fair user
  Tatizo la mfumo wetu wa sasa ni kusikiliza kila presha group na kuwanyamazisha kwa viti maalum, kuna siku waweza sikia chama cha wala bata nacho kina kiti kimoja, chamudata kimoja, TFF kimoja, BASATA kimoja, TBF etc

  we only need 10% ya special seats and it is for special people sio tu akina dada basi, sanasana ni kwenda kuwavunjia ndoa zao tu
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tumeona wanachama na wapenzi wa Chadema na hata vyama vingine wamefanya kile walichokiita "kulinda kura". Tumeona wameweza uzito kuwa wanataka kujua matokeo ya uchaguzi walioufanya na hatimaye hata maeneo ambayo yalionekana yangekuwa tete kama Nyamagana, Iringa na Arusha Mijini watu wameng'ang'ania hadi matokeo yamekuja.

  Sasa kweli Chadema inapata viti vingi, na tetesi za ndani kura za Urais nazo zinatishia (hakuna cha 70- wala 80 percent) sasa Chadema itoe msisitizo wa kutaka kura zote zitangazwe mapema? Au wasubiri ile ya "kutangazwa na kuapishwa" hasa ukizingatia hadi jioni hii ya Jumatatu ni majimbo 31 ambayo yametangazwa rasmi kati ya majimbo 239.

  Je matokeo ya kura za Ubunge tu yanatosha kuwafanya waridhike?
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Nov 1, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  mwanakijiji justice delayed justice denied, hizi fujo zinazooneshwa StarTV zinadhihirisha kuwa kuna hitaji la kutangaza matokeo haraka sana!
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni kukaba kote kote kwa kweli ubunge na uraisi hakuna haja ya kuwaamini CCM.
  Brazil wako 201 mil wameshatangaza matokeo yao sisi watu 41mil imekuwa issue.
   
 15. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kaka nguvu ya umma ndio yenye kuamua. Hakuna kulala mpaka kiieleweke. Kitu cha msingi ni kushinikiza tume itangaze matokeo kwa wakati ili wasipate nafasi ya kuchakachua kura.
  Tunaipenda tanzania na tuna nia njema na Tanzania ndio maana tunataka mabadiliko yenye tija kwa Taifa letu
   
 16. A

  Adili JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 1,997
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Ilikuwa itangazwe kila kituo baada ya hesabu. Kusubiri ni ku-Mugabe matokeo!
   
 17. A

  AMETHYST Senior Member

  #17
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani uwajibikaji upande wa Tume ungeleta maana sana kuliko nguvu za umma hasa inapokuja kwa kura za urais..japo bad wananchi una sababu za kushinikiza NEC lakini sasa maandamano yanaanzishwaje kudai tume kwa matokeo ya urais wakati hata wabunge bado!
  Au wagombea urais waanzishe kasheshe ya kutaka kura zao zitangazwe?All in all nguvu ya umma imeonesha kuwa kumbe mabadiliko tanzania yanawezekana na wanancho wetu tuliowadhania wamelala ucingizi kumbe waliamka siku nyingi wakawa wamekosa kiongozi mwenye karismma kama Slaa wa kuonyesha Kanani!
   
 18. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu hili nalo ni la kujiuliza kwa umakini sana maana mpaka sasa kwa kiasi fulani ukiangalia utaona kwamba kuna moto mkubwa sana wa kutaka Makamanda wa Chadema kusimamia kura kuhakikisha kwamba hakuna haki ya mtu ambayo inaibiwa.

  Jambo nililoliona ni kwamba yanapotangazwa matokeo ya Ubunge kuna baadhi ya maeneo furaha ya ushindi inasababisha na hata morale ya ulinzi ipotee na watu warudi makwao. Sasa nakaa na kujiuliza je tunatakiwa kulinda kura zote za Chadema ama ni kura za Ubunge na Udiwani tu ndizo ambazo zinahitaji kulindwa?
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kweli swali zuri sana..
  Mkuu wangu JK kachemsha, kisha shindwa sasa swala kubwa ni CCM Mtandao kukubali matokeo na kuachia ndilo lisilowezekana..Maadam haiwezekani hivyo basi tutatangaziwa JK ameshindwa kwa asilimia 51 hiyo Ijumaa na msafara tayari kwenda uwanja wa Tiafa kuapishwa kama ilivyofanyika Kenya...
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo, ila sioni dalili za CCM kuachia!!!:doh:
   
Loading...